Simiyu: Kairuki aagiza uchunguzi wa matumizi ya Tsh. Milioni 470 zilizoisha kabla ya mradi kukamilika

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,023
1,609
Waziri wa TAMISEMI, Angellah Kairuki, ameagiza TAKUKURU kuchunguza matumizi ya shilingi milioni 470, zilizotolewa na serikali kujenga shule mpya ya Sekondari Mwanduitinje, iliyopo jimbo la kisesa wilaya ya Meatu, ambapo fedha hizo zimeisha kabla ya mradi kumalizika ujenzi wake.

Waziri Kairuki ametoa agizo hilo baada ya kufika shuleni hapo akiwa katika ziara yake ya kikazi, ambapo Kaimu Mkuu wa Divisheni ya Miundombinu, Maendeleo ya Miji na Vijijini Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Mwita Joram, aliiomba serikali nyongeza ya fedha shilingi milioni 264 ili kukamilisha mradi huo, hali iliyoonesha kumshtua Waziri huyo na kuagiza uchunguzi ufanyike haraka ndani ya siku saba kubaini kama kuna ufisadi.

"Tunachotaka majengo haya yakamilike, hatuwezi tukawa tumemwaga hela yote halafu tukayaacha hivi, ndiyo maana nikasema hebu Afisa wetu wa TAKUKURU aingie kazini kwa siku saba na nitaomba hiyo ripoti inayojitegemea, halafu na Mkaguzi wetu Mkuu wa Ndani na yeye pia aweze kufanya uchunguzi ," ameagiza Waziri wa TAMISEMI.

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Kisesa, Luhaga Mpina, amesema mkwamo wa mradi huo unawaathiri wanafunzi wanaotembea umbali wa kilomita 17 kwenda shuleni. Hivyo ni muhimu hatua za haraka zichukuliwe ili Januari 2023, shule hiyo ianze kazi mara moja.

Chanzo: Nipashe
 
Waziri wa TAMISEMI, Angellah Kairuki, ameagiza TAKUKURU kuchunguza matumizi ya shilingi milioni 470, zilizotolewa na serikali kujenga shule mpya ya Sekondari Mwanduitinje, iliyopo jimbo la kisesa wilaya ya Meatu, ambapo fedha hizo zimeisha kabla

Chanzo: Nipashe
Hii Wizara imekosa Waziri kabisa
 
Wanakuwaga na mikwala, ufanyike uchunguzi, haiwezekani hela ya Serikali ipotee, camera na waandishi kibao, wakitoka hapo kila kitu kunafia hapo, utasikia tena siku Mkaguzi Mkuu wa Serikali akitoa ripoti, wala hatutasikia yoyote akiwajibishwa.
 
Waziri wa TAMISEMI, Angellah Kairuki, ameagiza TAKUKURU kuchunguza matumizi ya shilingi milioni 470, zilizotolewa na serikali kujenga shule mpya ya Sekondari Mwanduitinje, iliyopo jimbo la kisesa wilaya ya Meatu, ambapo fedha hizo zimeisha kabla

Chanzo: Nipashe
Pale mla rushwa anapoagiza mla rushwa mwenzake achunguzwe.
 
Mtu pekee nimemuona nchi hii yupo serious na kazi ni MAJALIWA KASIMU MAJALIWA

Hawa wengine walamba asalii

Asali ni tanguu

Huwezi kumnyima mwenzako asilambe asaliii
 
Waziri wa TAMISEMI, Angellah Kairuki, ameagiza TAKUKURU kuchunguza matumizi ya shilingi milioni 470, zilizotolewa na serikali kujenga shule mpya ya Sekondari Mwanduitinje, iliyopo jimbo la kisesa wilaya ya Meatu, ambapo fedha hizo zimeisha kabla ya mradi kumalizika ujenzi wake.

Waziri Kairuki ametoa agizo hilo baada ya kufika shuleni hapo akiwa katika ziara yake ya kikazi, ambapo Kaimu Mkuu wa Divisheni ya Miundombinu, Maendeleo ya Miji na Vijijini Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Mwita Joram, aliiomba serikali nyongeza ya fedha shilingi milioni 264 ili kukamilisha mradi huo, hali iliyoonesha kumshtua Waziri huyo na kuagiza uchunguzi ufanyike haraka ndani ya siku saba kubaini kama kuna ufisadi.

"Tunachotaka majengo haya yakamilike, hatuwezi tukawa tumemwaga hela yote halafu tukayaacha hivi, ndiyo maana nikasema hebu Afisa wetu wa TAKUKURU aingie kazini kwa siku saba na nitaomba hiyo ripoti inayojitegemea, halafu na Mkaguzi wetu Mkuu wa Ndani na yeye pia aweze kufanya uchunguzi ," ameagiza Waziri wa TAMISEMI.

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Kisesa, Luhaga Mpina, amesema mkwamo wa mradi huo unawaathiri wanafunzi wanaotembea umbali wa kilomita 17 kwenda shuleni, hivyo ni muhimu hatua za haraka zichukuliwe ili Januari 2023, shule hiyo ianze kazi mara moja.

Chanzo: Nipashe
Heading na content havisomani
 
Back
Top Bottom