Simiyu: Akamatwa na Kobe zaidi ya 400 wakiwa kwenye mabegi 3

Kwani amekamatwa airport au akivuka mpaka wa nchi je kama alikuwa anapeleka mkoa mwingine kuanzisha zoo labda aliona mambo ya vibali yanachukua muda mrefu akaamua afanye yake.
 
Hiyo sheria haijaanza jana walk juzi
Ni ya kitambo sana

Ova
Kama ya kitambo itakuwa imepitwa na wakati,sheria sio msahafu, hizi sheria nyingine zinatakiwe zifanyiwe marekebisho na ziboreshwe,kwa Tanzania kobe sio viumbe vilivyo kwenye hatari ya kutoweka yapasa milango ifunguliwe watu wafanye biashara na huko ndio kumuinua mnyonge,kutokana na urasimu ndio maana wengine huamua kufanya kinyume na taratibu zilizowekwa.
 
Huu mwaka nafikiri kobe wametotolewa kwa wingi huku mashambani Morogoro wapo wapo tu wadogo wadogo wengi...

Wamuhoji live on TV atupe mchongo wa wateja wake, tuanze kuwaokota na sisi 😂

Everyday is Saturday................................:cool:
siku zote kobe wanathamani kubwa, nchi za mashariki ya mbali ni chakula pendwa tena cha heshma
 
Write your reply...Kuna mahali hata ukitaka kobe buku 2 wiki moja unawapata hebu niambie soko liko wapi mimi nipeleke kukamatwa na nyara ukafungwa ni uzembe kabla hujaanza safari unatanguliza ufagio mbele ya safari kusafisha njia naongea nikiwa na uzoefu wa kusafirisha magendo
 
Kuna jambo huwa linanipasua kichwa sana kuhusu thamani ya bidhaa au mali haramu. Yaani unakuta bidhaa haiuzwi kihalali mfano dawa za kulevya au nyara kama meno ya tembo, lakina unakuta jeshi la polisi wanatutangazia kuwa tumekamata pembo za ndovu au dawa ya kulevya yenye thamani ya milioni500 au vyovyote vile. Swali ni kuwa thamani ya bidhaa ya haramu mnaitoa wapi? Ukinikamata na bidhaa ya magendo mfano sukari kutoka Zambia au vipondozi sijalipia kodi utakuwa na uhalali wa kutaja thamani yake kwa kuwa bidhaa hizo zina bei halisi katika soko pia zinauzwa hadharani na kwa bei halisi. Mnanikera kwa kweli wakamata bidhaa haramu kwa tathimini zenu za kutunga. kudadeki zenu.
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom