SIMBACHAWENE:- Uchaguzi MEYA Dar. kabla ya March 25.

Brigedia Chan-ocha

JF-Expert Member
Mar 7, 2014
1,353
2,846
Ametangaza leo akiwa jijini Arusha, amesema kwamba, uchaguzi huo ni lazima ufanyike kabla ya tarehe 25 mwezi huu wa Tatu, na amesema yeye kazi yake siyo kusema mjumbe fuluni (kwa jina) anaqualify kupiga kura ila yeye kazi yake ni kutoa taratibu na kufuata sheria za nchi, wenye dhamana ya kujua ni mjumbe gani apige kura ni Vyama vyenyewe na Kwa kushirikiana na Tume ya uchaguzi.

Vile vile, ameongelea kuhusu gazeti la Raia Tanzania lililoandika habari za kipuuzi kwamba yeye amekuwa akifanya mazungumzo na UKAWA kwa siri kuhusu uchaguzi huo, amesema, huo ni upuuzi na amishazoea kuhusu hayo, akitolea mfano wa Mwandishi mmoja mkoani Singida aliyewahi kumtuhumu kuwa ameshikwa ugoni, wakati kwa wakati na siku hiyo alikuwa na mkewe wake mkoani Singida pamoja na dada yake kitendo kilichomsikitisha sana Mke wake na mkewe kuapa kutoamini habari zozote za magazeti.
 
Back
Top Bottom