Simbachawene: Toka mpiga debe hadi Naibu waziri

Simba kweli kuna muda aliwahi kujaribu kuwa mtu wa maana pamoja na kina Ane kilango, ...
Lakini naona , kama alivyosema jamaa mmoja hapo juu kaamua kurudia kazi yake ya zamani ya upiga debe kwa kuipigia
debe CCM.

Tena wakati mwingine huwa anaamua tu kuwabishia kina Tundu Lissu, sui kwanini!?
Nakumbuka Tundu Lissu alipothibitisha kisheria kuwa kuvaa skafu yenye bendera ya taifa alikofanya mbunge mmoja wa
ccm bungeni....hilo ni kosa la jinai kwa mujibu wa sheria zetu, na Lissu akashauri jamaa ashugulikiwe kisheria au bunge
litamke kuwa sheria hiyo imefutwa!

Ajabu ya dunia Simbachawene alikuwa amekaimu kiti cha spika ......akasema eti Lissu amepitwa na wakati sababu hilo
swala raisi alishatamka kuwa watu waachwe wavae bendera za taifa!!!!!

Hapo ndipo nikamdharau sana sana bwana huyu, tamko la raisi lina tengua sheria???

Mchango mzuri + signature yako pia ni nzuri.
 
Huyo ni zaidi ya mchwa uliza wakurugenzi wa halmashauri alipokuwa mjumbe wa kamati ya laac yeye na saiba wake chitalilo mbunge wa buchosa enzi hizo,bila milion moja kama rushwa taarifa ya halmashauri haipiti.
Tusubiri tuone lakini hatima yake siyo njema labda aokoke sasa hivi na kutubu dhambi.
 
Dah, umenikumbusha huyo jamaa Gerard aliyegongwa na gari alilokuwa analipigia debe. Ilikuwa miaka ya kati ya 92 na 95, nilikuwa namfahamu huyo jamaa. RIP Gerard rafiki yake SImbachawene na hongera Simbachawene kwa kutokata tamaa. Kumbuka ulikotoka na jitahidi kuwatumikia watanzania kwa uadilifu ili uwakomboe wengi toka kwenye umaskini
 
Anayo bar yake pale vingunguti relini ,mara nyingi yuko hapo wakati wa mapunziko ya bunge!
...Mjasilia mali wa ukweli...Haya ngoja tuone akimaliza mwaka tukaona bar imekuwa hoteli ya ghorofa 3 lazima atakuwa ametuibia...:loco:
 
Hii ndio aina ya watu wanaotakiwa kama ameweza kujituma mwenyewe kutoka huko hadi Ubunge hadi Unaibu Waziri, atajituma katika kuutumikia Umma wa Watanzania katika nafasi hiyo. Ukienda kule Titanic Bar, Vingunguti Dar - utamkuta wakati ambao sio wa Bunge, he is simple and interacts with any body. Sio nyie mkisha kuwa wabunge mnabadili marafiki !!! Nilipata bahati ya kukutana naye Bagamoyo mwaka 2008 kabla sijajilipua, niliona kama ni Material Leader.
 
Topic: Simbachawene: Toka mpiga debe hadi Naibu waziri


- Ingekuwa nchi zilizoendelea huyu ni a hero kwa wananchi wa chini sana maana anakuwa kama Rais wa zamani wa Brazil na Poland, yaani kutokea chini sana sio kuwa na death sentence, inawezekana ATUNGIWE TU VITABU VYA HISTORIA YA MAISHA YAKE ILI UWE MFANO KWA WENGINE, KAMA VILE VITABU VYA KINA MIKE TYSON KULE US!

- SO HE IS MY HERO TOO!


William.
 
Mimi nafikiri Jk ameona labda ajaribu madeiwaka maana maprofesa na madoctor wote aliowapa ulaji wameshindwa kumsaidia.
 
Dah, umenikumbusha huyo jamaa Gerard aliyegongwa na gari alilokuwa analipigia debe. Ilikuwa miaka ya kati ya 92 na 95, nilikuwa namfahamu huyo jamaa. RIP Gerard rafiki yake SImbachawene na hongera Simbachawene kwa kutokata tamaa. Kumbuka ulikotoka na jitahidi kuwatumikia watanzania kwa uadilifu ili uwakomboe wengi toka kwenye umaskini

Haya ndiyo maneno lakini siyo kwamba ooooo mpiga debe! Huyo alikuwa mpiga debe sasa siyo kajikomboa tumtake awakomboe wengine. Amepigana kwa juhudi hadi amekuwa msomi lakini watu hawataki! Big UP Simba kama Simba jana.
 
Usihangaike na CV Ya Mh. Simbachawene cha zaidi ni Degree ya sheria toka chuo kikuu huria, lazima atakuwa ni kichwa au degree zenyewe za chuo hicho ni nyepesi kwa sababu wakati anajisomea chuo hicho huria alikuwa ni mpiga debe katika mabasi ya shemeji yake George Chove , mabasi ya urafiki. Alikuwa akipiga debe lake Stand ya zamani Dodoma pale Nyuma ya SIDO. Alichokuwa anawaudhi wasafili ni ile tabia yake ya kuwahi mizigo ya abiria na saa ingine kuwabeba na kuwaingiza katika basi lake la Urafiki hasa wanawake alikuwa anawabeba akiwashika sehemu zingine ambazo walikuwa hawapendi,


Siku moja mpiga debe mwenzie akiitwa Gerard alisagwa na basi siku hiyo Simbachawene alilia kama motto mdogo. Hata hivyo wadau wengi hawashangai sana kwani Josep Starling alikuwa shoe shiner hadi Rais wa Urusi ile ya zamani kabla ya kusambalatishwa na marekani.

Sitegemei utendaji ulio tukuka kwa huyu mpiga debe
 
...Mjasilia mali wa ukweli...Haya ngoja tuone akimaliza mwaka tukaona bar imekuwa hoteli ya ghorofa 3 lazima atakuwa ametuibia...:loco:

Uzuri tayari vitega uchumi vyake tunavijua tayari vikiongezeka tu tunajua tayari kachumia tumbo
 
apige debe sasa katika kutetea haki na maendeleo ila akipigia debe unafiki na uzandiki wa ccm atakuwa mpiga debe aliehamia sehemu ya biashara haramu
 
Nadhani wanaofahamu wanaweza kunisahihisha. Kumbukumbu zangu zinanionesha kuwa huyu jamaa amesoma Full Technician Course (FTC) Chuo cha ufundi Arusha idara ya mitambo (mechanical engineering). He didnt get his degree from no where!
 
kwa hiyo kama alikuwa mpiga debe?
Si alikuwa anajishughulisha apate kipato cha kumkimu mahitaji yake ya shule?

Kwa binadamu lazima awe na mahala pa kuanzia, sio wote wamezaliwa na vijiko vya dhahabu, wengu wanaanza chini kwenda juu.....

Cha kuhofia ni utendaji wake........je atamudu?
 
Hata mimi nashindwa kuwaelewa watz kama alivyosema Riz1. Huyu ni mtu wa kupongeza kwa juhudi zake; na tunatakiwa kuwatia moyo vijana kwamba kwa kutumia juhudi na maarifa inawezekana kufika mbali.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom