Simbachawene: Sitakubali kung’oka uwaziri

Status
Not open for further replies.

Chenge

JF-Expert Member
Oct 5, 2011
1,073
377
Simbachawene: Sitakubali kung’oka uwaziri


na Happiness Mtweve, Dodoma

SAM_1112.JPG

amka2.gif
NAIBU Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene amesema hatakubali kung’oka katika wadhifa huo kwa uzembe, ubadhirifu, urasimu na ufisadi unaofanywa na wafanyakazi katika wizara hiyo, na badala yake atawawajibisha mara moja.
Simbachawene alitoa kauli hiyo mjini hapa juzi alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Dodoma.
Alisema kumekuwepo na tatizo la baadhi ya watumishi kuingiza siasa kazini na kuharibu kazi, ili watu wengine wanaofanya vizuri waonekane hawafai baada ya kuibuka tatizo la nchi kuwa gizani na kuwalazimu mawaziri kutakiwa kujiuzulu na kusema kuwa hatang’oka madarakani kwa mtindo huo.
Simbachawene alisema watumishi hao wamekuwa wakishindwa kutekeleza majukumu yao kwa uaminifu na kuibua mianya ya rushwa kwa kuwacheleweshea kuwaunganishia umeme wananchi kwa makusudi.
Naibu waziri huyo alionekana kuibeza taarifa iliyotolewa na Meneja wa Mkoa wa TANESCO ambayo inaeleza mafanikio na juhudi zilizopatikana kutokana na utendaji kazi wao, ambapo alisema taarifa hiyo ni ya uongo na haina ukweli wowote ndani yake.
“Nashangaa eti mnasema kuna mafanikio, hakuna lolote, mmelala tu, wala hakuna kazi mliyoifanya, siku tatu tu nilizokaa hapa Dodoma nimefuatwa na watu zaidi ya watano ofisini kwangu wakinilalamikia urasimu mnaoufanya huku wengine wakiwa wamekaa miaka miwili wakisuburi kuunganishiwa umeme bila mafanikio.
“Hapo mnaweza mkajisifu mmefanya kazi kweli, tusidanganyane na tutaonana wabaya kama mtu atashindwa kusimamia kazi yake vizuri, lazima wananchi wapate umeme mpaka vijijini,” alisema Simbachawene.
Alisema uongo wa taarifa ya meneja huyo unatokana na idadi ndogo ya wananchi waliounganishiwa umeme mkoani hapa, ambayo haiendi sambamba na idadi ya wananchi wenye mahitaji hayo.
Pamoja na hayo, alisema TANESCO Mkoa wa Dodoma bado haijaenda sambamba na mabadiliko ya teknolojia na kuwataka wajiulize wamechelewa wapi kufanya mabadiliko hayo.

 
Huyu alitakiwa mpaka sasa awe amelala muhimbili mochwali anasubiliwa kuagwa, kwa kitendo alichokifanya huko Singida, anabahati tu kuwa mwenye mke ni mpole, kama ningekuwa mimi haki yake ilikuwa risasi ya kichwa ili akaindalie makazi ccm yao huko kuzimu.
 
Huyu jamaa mwenye mke amekosea, angem-gecha usoni, iwe alama nzuri ya uzinzi wake milele amina.
 
JF mbona mnatuchanganya: thread moja inasema ni simbachawene nyingine ni Josephat Joseph Fisichamwene. Ipi tuiamini?
 
Kaongea maneno hayo juzi na jana kafumaniwa kweli dunia tambala bovu leo unavaa suti kesho kaniki.
 
sasa JF imekuwa kichwa cha stupid thinkers na genge la wazushi mbona mara twaambiwa kafumaniwa mara tena hajiuzulu
 
Status
Not open for further replies.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom