Simbachawene: Sitakubali kung’oka uwaziri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Simbachawene: Sitakubali kung’oka uwaziri

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jun 3, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jun 3, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  [TABLE="width: 879"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]
  na Happiness Mtweve, Dodoma

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]
  NAIBU Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene amesema hatakubali kung’oka katika wadhifa huo kwa uzembe, ubadhirifu, urasimu na ufisadi unaofanywa na wafanyakazi katika wizara hiyo, na badala yake atawawajibisha mara moja.


  Simbachawene alitoa kauli hiyo mjini hapa juzi alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Dodoma.

  Alisema kumekuwepo na tatizo la baadhi ya watumishi kuingiza siasa kazini na kuharibu kazi, ili watu wengine wanaofanya vizuri waonekane hawafai baada ya kuibuka tatizo la nchi kuwa gizani na kuwalazimu mawaziri kutakiwa kujiuzulu na kusema kuwa hatang’oka madarakani kwa mtindo huo.


  Simbachawene alisema watumishi hao wamekuwa wakishindwa kutekeleza majukumu yao kwa uaminifu na kuibua mianya ya rushwa kwa kuwacheleweshea kuwaunganishia umeme wananchi kwa makusudi.


  Naibu waziri huyo alionekana kuibeza taarifa iliyotolewa na Meneja wa Mkoa wa TANESCO ambayo inaeleza mafanikio na juhudi zilizopatikana kutokana na utendaji kazi wao, ambapo alisema taarifa hiyo ni ya uongo na haina ukweli wowote ndani yake.


  “Nashangaa eti mnasema kuna mafanikio, hakuna lolote, mmelala tu, wala hakuna kazi mliyoifanya, siku tatu tu nilizokaa hapa Dodoma nimefuatwa na watu zaidi ya watano ofisini kwangu wakinilalamikia urasimu mnaoufanya huku wengine wakiwa wamekaa miaka miwili wakisuburi kuunganishiwa umeme bila mafanikio.


  “Hapo mnaweza mkajisifu mmefanya kazi kweli, tusidanganyane na tutaonana wabaya kama mtu atashindwa kusimamia kazi yake vizuri, lazima wananchi wapate umeme mpaka vijijini,” alisema Simbachawene.


  Alisema uongo wa taarifa ya meneja huyo unatokana na idadi ndogo ya wananchi waliounganishiwa umeme mkoani hapa, ambayo haiendi sambamba na idadi ya wananchi wenye mahitaji hayo.


  Pamoja na hayo, alisema TANESCO Mkoa wa Dodoma bado haijaenda sambamba na mabadiliko ya teknolojia na kuwataka wajiulize wamechelewa wapi kufanya mabadiliko hayo.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Jun 3, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Tunahitaji Katiba Mpya Haraka Kabisa; Wabunge wasiwe Mawaziri Inaonyesha Wabunge - Mawaziri wanaona Utamu na

  Kuondolewa Uwaziri kunawafanya kuwa vichaa au punguani, Sasa Simbachwene anaapa hata fanya makosa katu, hajui

  Rais ajae ni Miaka miwili ijayo? Na anaweza asimchague sio kwa sababu sio Mchapa kazi; kwasababu ameshauriwa kuwa

  Kuna anayefaa kwa nyadhifa hiyo zaidi ya huyo Simbachwene?

  * Kufanya Kosa ni Ubinaadamu, Kurudia hilo kosa ndio kubaya!!!
   
Loading...