Simbachawene: Polisi inalishughulikia shambulio la kutumia silaha kwa Tundu Lissu kama uhalifu mwingine na upelelezi unaendelea

Baada ya kushindwa kwa jaribio la kishamba hilo waliotumwa watakuwa walishatangulizwa Ili kuficha siri ya masters,japo Mungu si athuman,ulipa hapahapa kwingine ni hukumu.
 
Lowasa ni mgonjwa atafia ikulu atupe gharama za uchaguzi,sasa yeye na wao nani mgonjwa.Kupiga push-up ni kumkufuru Mungu,Mungu apendi kujiinua.
 
Akijibu swali la mtangazaji wa ITV Midle kuhusu uchunguzi ulipofikia kwenye tukio la kushambuliwa Tundu Lisu mbunge by then mh Simbachawene amesema yapo matukio mengi ya kutumia silaha yanayochunguzwa na hilo la Tundu Lisu siyo special ni uhalifu kama mwingine hivyo yote yanashughulikiwa kwa usawa.

Simbachawene amesema ifike mahali watanzania waelewe jukumu la polisi ni kulinda raia wote na mali zao kwa usawa na isionekane fulani ni muhimu kuliko fulani.


Chanzo: ITV
Kama ni hivyo kwani Samia au Kikwete au Majaliwa wakiwa wanapita mabarabara mnatusumbua sumbua na vingora vyenu kututaka tuweke V8 zetu pembeni hadi hao wapite ?
 
Tukio la Lisu,na Lowasa ni kwetu sisi tulio hai Mungu alitaka kutuonyesha uKuu wake,Ili litimie neno lililonenwa na Nabii Isaya "Hakika nalikujua ungali tumboni mwa mama haki"
Waliotaka Lisu aondoke wengi wao wametangulia wao kabla yake.
Huwezi ukakosoa uumbaji wa Mungu na ukabaki salama
 
Wewe

Unadhani Tundu ni special sana kuliko vijana na wamama waliouliwa arusha na sehemu zingine na watu wasiojulikana?

Watu wote ni sawa hivyo tulirni na kama mna ushahidi nenda polive upeleke kwa yule unamtetea.
Wewe kama ulifungua geti kuruhusu magaidi subiria karma yako itakufikia.
Unaweza ukadhani umevaa nguo kumbe Jamii inakuona upo uchi Hakuna Siri chini ya jua.
 
Ili kukata mzizi wa fitina na ili kumnyamazisha Lissu, kwani serikali inayoaamini haihusiki na shambulio la Lissu isiunde tume huru kuchunguza tukio hili?

Kama waneweza kuunda kamati kuchunguza mauaji yaliyofanywa na Polisi huko Mtwara, kwanini wanashindwa kufanya hivyo kwa tukio la Lissu kushambuliwa?

Ushauri: Kama ni sahihi kisheria, Tundu Lissu sasa ni wakati muafaka kwa wewe kuandika maelezo juu ya taarifa ulizonazo kuhusiana na tukio hilo na uziwasilishe kwa Raisi, Waziri Mkuu, Waziri wa Mambo ya Ndani , IGP na nakala kwa umma.

Na pia kama una majina mahususi ya watuhumiwa, yaweke wazi kwa Raisi na wasaidizi wake.

In other words, handle this issue in a more formal way.

Wasipofanyia kazi maelezo yako ikiwezekana na ya dereva wako(alichoshuhudia), endelea kuwatuhumu kama unavyofanya sasa.
 
Serikali hii iunde Tume?! yale ya Mto Mara na kinyesi cha n'gombe umeshayasahau mara hii..

Hizo tume za serikali ni utapeli mtupu wanachezea pesa za walipakodi, kama hawataki naona bora wakae kimya tu.
 
Kushambuliwa kwa Lissu kulitusikitisha wengi, mbali na Lissu mwenyewe kuitakia mabaya Tanzania wakati huo. Lakini kitendo cha wahathirika wa tukio lile kukataa kutoa ushirikiano, kilinipa, kinanipa maswali mengi kujua lengo.

Mleta mada unaweza kutoa sababu za msingi za kumficha shahidi muhimu aliyeshuhudia tukio lile, ?inasemwa alikuwa na mwenzake kwenye gari wakati anashambuliwa !
 
Kaenda Tanzania mwaka 2020 kufanya kampeni kazunguuka, kazuruula karibu nchi yote, bila hata kuguswa. Baada ya kuona kashindwa kaondoka zake. Kapitia pale uwanja wa ndege wa Dar huku akiweka mikono yake mfukoni na kupiga mluzi.

Kalafu ndiyo anadai wanataka kukuua. Kwa ufupi aliyekuwa anakupa umuhimu na airtime bila kujua, hayupo tena. Hivyo huna umuhimu ule tena, siyo MAARUFU tena ila alichobakia nacho ni upayukaji tu.
 
Ili kukata mzizi wa fitina na ili kumnyamazisha Lissu, kwani serikali inayoaamini haihusiki na shambulio la Lissu isiunde tume huru kuchunguza tukio hili...

Ndugu yangu Salary Slip, miaka yoote binafsi nimeyasema haya lakini naonekana mpumbavu...kama Lissu au CDM wanajua nani mhusika na mchoro wote wanasubiri nini kuutangazia umma na kuomba msaada kisheria kimataifa?

Miaka yoote TL yuko Belgium, na anajua sheria..kwanini asiombe jumuiya y kimataif a iishinikize GOT kufanyia suala lake uchunguzi?
 
Kushambuliwa kwa Lissu kulitusikitisha wengi, mbali na Lissu mwenyewe kuitakia mabaya Tanzania wakati huo. Lakini kitendo cha wahathirika wa tukio lile kukataa kutoa ushirikiano, kilinipa, kinanipa maswali mengi kujua lengo...
Kwenye mauaji ya kishamba yaliyofanyika Mtwara na kumpora hela mfanyabiashara ni waathirika gani waliohojiwa ili kuwezesha wale askari 7 majambazi kukamatwa ?
 
Ndugu yangu Salary Slip, miaka yoote binafsi nimeyasema haya lakini naonekana mpumbavu...kama Lissu au CDM wanajua nani mhusika na mchoro wote wanasubiri nini kuutangazia umma na kuomba msaada kisheria kimataifa?...
Serikali ya Tanzania ijichunguze yenyewe ? Unakumbuka tuliomba uchunguzi wa kimataifa kuhusu jambo hili , uliona wapi serikali yako ikikubali ?
 
Serikali ya Tanzania ijichunguze yenyewe ? Unakumbuka tuliomba uchunguzi wa kimataifa kuhusu jambo hili , uliona wapi serikali yako ikikubali ?

sasa mnajua kabisa serikali haiwezi kukubali haya mnaiomba au kuibembeleza ya nini?.... miaka yoote mmekosa solution mpaka leo tunawasikia mkiomba serikali ichunguze....hakuna njia nyingine yakulichunguza suala hili na majibu kuwekwa hadharani na wahusika kushitakiwa hata mahakama za nje au malalamiko kwenda balozi mbalimbali na wahusika wakapigwa vikwazo?
 
Sasa hapo hapo kwenye maswali na mashaka yako ndipo umuhimu wa tume huru unapokuja.
Kushambuliwa kwa Lissu kulitusikitisha wengi, mbali na Lissu mwenyewe kuitakia mabaya Tanzania wakati huo. Lakini kitendo cha wahathirika wa tukio lile kukataa kutoa ushirikiano, kilinipa, kinanipa maswali mengi kujua lengo.

Mleta mada unaweza kutoa sababu za msingi za kumficha shahidi muhimu aliyeshuhudia tukio lile, ?inasemwa alikuwa na mwenzake kwenye gari wakati anashambuliwa !
 
Ndugu yangu Salary Slip, miaka yoote binafsi nimeyasema haya lakini naonekana mpumbavu...kama Lissu au CDM wanajua nani mhusika na mchoro wote wanasubiri nini kuutangazia umma na kuomba msaada kisheria kimataifa?.....

Miaka yoote TL yuko Belgium, na anajua sheria..kwanini asiombe jumuiya y kimataif a iishinikize GOT kufanyia suala lake uchunguzi?

Ni jukumu la serikali yeyote halali duniani kulinda watu na mali zao. Lissu alishambuliwa kwa risasi, serikali ilikuwa na wajibu wa kuchunguza kwa kina wahusika wa tukio hilo. Serikali haijafanya uchunguzi huo kwa muda wote huu kwasababu moja kuu; nayo ni kuwa walikuwa wahusika wa shambulio hilo hivyo hakuna haja ya uchunguzi kwani wanawafahamu wahusika!!!
 
Mlelewa Ubelgiji anatafuta kila mbinu ili aendelee kupewa hela na Amsterdam
Na pesa tunazokopa kama Serikali, na misaada ya mapesa kibao tunayopewa toka World Bank, IMF na European Union, si mapesa hayohayo ya Amsterdam? Khy hata sisi kama Taifa tunapitisha bakuli kuwa sisi masikini ili tupate hayo mapesa? Jamani, tuwe tunatulia kidogo kabla ua kuandika vitu hapa JF.

Tulio wengi, tumezoea wizi na kutishiwa maisha na Vibaka tu, wanaotuibia simu na laptop zetu kwenye foleni za magari, kuvamiwa usiku na wakachukua TV nk. Lakini hatujawahi kushambuliwa na risasi zaidi ya 30 na karibu nusu yake zikatuchana miili yetu kama Ndugu Lisu. Tunapata wapi ujasiri wa kuhoji kauli zake za wasiwasi? Wakati huohuo..mpaka leo hatujasikia watuhumiwa wala washukiwa waliokamatwa. kwanini asiwe na wasiwasi na utawala wa nchi? Anapomuomba Mh Rais atangaze rasmi kwa Public, Lisu anataka apewe assurance toka kwa Mtawala, ili awe na amani. Sidhani kama ni sahihi kudharau woga alionao Ndugu Lisu na sidhani kama kuna shida kwa Mheshimiwa Rais kutangaza hivyo, wala halitamshushia hadhi yeyote zaidi ya kumsafisha, kama kiongozi apendaye amana na usawa zaidi ktk jamii yetu ya Kitanzania.
 
Back
Top Bottom