Simbachawene: Mali nyingi za Mitume na Manabii zimesajiliwa kwa majina yao binafsi wakidaiwa Kodi wanadai ni mali za Kanisa

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,840
141,765
Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene amesema kuna tatizo kubwa kwenye umiliki wa mali katika makanisa kiasi cha kuleta changamoto kwenye ulipaji wa kodi.

Simbachawene amesema kuna mali kama Hospitali, Majengo na Magari zimeandikishwa kwa majina binafsi ya Wachungaji, Maaskofu, Mitume au Manabii lakini waumini wao huamini mali hizo ni za makanisa yao.

“Serikali inapokuja kudai kodi yake ndipo panatokea matatizo kwani viongozi hao wa dini hutaka kujificha kwenye kivuli cha Kanisa”, alisema Simbachawene katika Kongamano la Mitume na Manabii.

Chanzo: Wapo Radio

Nawatakia Dominica yenye baraka!
 
Mali zenyewe zinapatikana kwa kuwachangisha Waamini alafu Mwenye Mamlaka nazo anabaki ni Nabii.

Waamini hawahusishwi kwenye uendeshaji wao kazi yao ni kuchangishwa gharama za uendeshaji.

Kazi ya Nabii inakuwa ni kubuni tu majina ya sadaka.
Majina ya sadaka km vile ya kujimaliza, fungu la kumi, shukrani, sadaka ya madhabahu, zaka, kutegemeza parish n.k
 
Mbona kitu kiko clear labda serikali ndio inawagwaya, kama unaandikisha kwa jina lako lipa kodi kama ni taasisi ya dini basi sawa sasa inakuwa yeye kuchagua aende wapi, serikali tekelezeni sheria inavyotaka wala sio kulialia.Amenisikitisha Simbachawene, kama simba unalialia Swala/sungura itakuwaje.
 
Serikali inabidi idhibiti haya makanisa na mengi Yao yanapotosha watu, waige Rwanda
 
Halafu hao ndio wanaomba iundwe Tume ya maadili ya viongozi wa kiroho! Majizi na matapeli yanaomba yasimamiwe kimaadili.

Nunachokiiona mamlaka haina shida na utapeli wao as long as wanasifia na kuunga mkono viongozi wa kisuasa walioko madarakani. Hiyo Tume inakusudiwa kuwadhibiti viongozi wa kiroho wanaowakosoa viongozi wa kisiasa walioko madarakani.

Wizi na utapeli wa viongozi wa kidini kwa waamini wao naona ni ruksa ili mradi hawakosoi walio madarakani.
 
Huwa hawa mawaziri wanashangaza sana
Yaani Waziri anakuwa mwandishi wa Habari?
Sheria zinasemaje mpaka atoke na kuongea haya
Je anawaogopa au anataka apewe hela kidogo na yeye?

Huwa siwaelewi kabisa maana hapo ilikuwa afuate sheria kama kukwepa kodi sheria ifuatwe la sivyo wanatuacha kwenye maswali mengi sana
 
Kumaliza mzizi wa fitina hapa, suluhisho ni hili.

1. Kila taasisi ya dini ilazimishwe kuweka wazi mali inazozimiliki ili serikali ijue, waumini wajue na jamii ijue.

2. Kila kiongozi wa dini awajibike kuweka wazi mali zake kwa serikali na umma kila mwaka (Lengo ni kuepusha utakatishaji wa pesa na utapeli kupitia mgongo wa dini).

3. Mali yoyote iliyoandikishwa kwa jina la mtu ilipiwe kodi moja kwa moja, hakuna cha maongezi.

4. Mali yoyote iliyoandikishwa kwa jina binafsi na kukweka kulipa kodi kwa mgongo wa kidini itaifishwe mpaka mhusika atakapolipa kodi husika na marejeo ya adhabu.

5. Mali yoyote ya taasisi ya dini iliyokuja kumilikishwa kwa mtu binafsi kinyume na utaratibu, serikali iitaifishwe au kuirejesha kwa waumini wa dini.
 
Ushsuri mzuri!
 
Back
Top Bottom