Queen V
JF-Expert Member
- Jan 19, 2012
- 776
- 1,330
Mbunge wa Kibakwe katika Wilaya ya Mpwapwa Jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, George Simbachawene alifanya mahojiano na Radio A FM ya Dodoma alipoalikwa kuzungumzia Builders Expo inayofanyika Jijini Humo.
Katika mahojiano hayo, Simbachawene amemsifia Rais Magufuli kwa kusema unapozungumzia yanayotokea hivi sasa nchini, lazima uanze kwa kumtaja Magufuli. Amesema kuwa Watanzania kwa pamoja tuliwaza tu endapo tungapata Rais wa namna hii na sasa Mungu ametupa tulichokitaka.
"Hii ni awamu ya vitendo na si maneno tu. Nchi yetu ilikuwa haijajengwa vizuri, hatuna miundombinu inayoendana na wakati tulionao wala inayoenda kulingana na maendeleo ya watu. Angalia wenzetu tuliopata uhuru pamoja nao. Tumewasaidia South Africa kupata uhuru wao, tumepata uhuru sawa na Malaysia, Singapore na hatukupata uhuru mbali sana na Ghana, Nigeria lakini wametupita miundombinu." alisema Simbachawene.
"Kutokana na dunia ya sasa kuwa kama kijiji, watu watakimbia nchi na kwenda kuzuri. Tanzania ina amani, watu wakarimu, wapole na rasilimali nyingi lakini tuna miundombinu ya kuendana na hali ilivyo sasa? Hapana!" aliongeza Simbachawene.
Aliendelea kueleza kuwa ni dhahiri tulikuwa tunahitaji Rais wa kujenga nchi na kila awamu huwa na vipaumbele vyake. Amani tunayo, ardhi nzuri tunayo, tuna madini, mbuga za wanyama na tunashangilia. Lakini nchi inajengwa?
"Dodoma squatter zilitaka kuingia. Dar imekuwa squatterized hadi kupanga tena huwezi! Mwanza vivyo hivyo. Kwanini tuna rasilimali nyingi lakini nchi haijengwi interms of miji, mabarabara, reli, airway wakati ni lazima uwe na mambo haya ndio nchi iitwe nchi? Hata ukiwa na nafasi nzuri lazima ujenge nyumba."
"Sasa nchi hii inajengwa kweli kweli. Baada ya miaka 5 au 10 ya Rais Magufuli tutajikuta Tanzania hata kama tunasema Rais sio rafiki wa mtu(Rais hapaswi kuwa rafiki wa mtu, anapaswa kuwa rafiki wa nchi zaidi na si kundi wala mtu) tuna maendeleo makubwa." Alisisitiza.
Aidha kuhusu suala la Serikali kuhamia Dodoma, Simbachawene ambaye alikuwa Waziri TAMISEMI kabla ya kujiuzulu wadhifa anasema iIlikuwa ngumu kukubaliana kuhamia Dodoma kwani baadhi ya Mawaziri walipinga sana walilalamika kuhusu kuacha familia na mali zao zilizopo Dar es Salaam.
Aliendelea kueleza, “Rais Magufuli alisema hiiiiiii mtahamia tu na hii ni process, inapofeli analaumiwa aliyeanzisha lakini inapofaulu ndipo mnajua kuwa kiongozi wenu ni jiwe”
Anasema haukuwepo mpango ulioandikwa ukapitishwa kuhusu Serikali kuhamia Dodoma lakini uamuzi ulishakuwepo toka 1973, miaka 40+ baadae ndo unatekelezwa, hivyo hakukuwa na maana ya kujadiliana na watu.
"Serikali yote iko Dodoma amebaki Rais wetu. Na yeye anaendelea kujenga pale Ikulu ya Chamwino Dodoma hivyo tunaamini Rais anaingia muda si mrefu." alimalizia Simbachawene.