Simbachawene: Kuna Mawaziri walipinga kuhamia Dodoma lakini Magufuli ni 'jiwe' amewahamisha

Queen V

Queen V

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2012
Messages
659
Points
1,000
Queen V

Queen V

JF-Expert Member
Joined Jan 19, 2012
659 1,000

Mbunge wa Kibakwe katika Wilaya ya Mpwapwa Jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, George Simbachawene alifanya mahojiano na Radio A FM ya Dodoma alipoalikwa kuzungumzia Builders Expo inayofanyika Jijini Humo.

Katika mahojiano hayo, Simbachawene amemsifia Rais Magufuli kwa kusema unapozungumzia yanayotokea hivi sasa nchini, lazima uanze kwa kumtaja Magufuli. Amesema kuwa Watanzania kwa pamoja tuliwaza tu endapo tungapata Rais wa namna hii na sasa Mungu ametupa tulichokitaka.

"Hii ni awamu ya vitendo na si maneno tu. Nchi yetu ilikuwa haijajengwa vizuri, hatuna miundombinu inayoendana na wakati tulionao wala inayoenda kulingana na maendeleo ya watu. Angalia wenzetu tuliopata uhuru pamoja nao. Tumewasaidia South Africa kupata uhuru wao, tumepata uhuru sawa na Malaysia, Singapore na hatukupata uhuru mbali sana na Ghana, Nigeria lakini wametupita miundombinu." alisema Simbachawene.

"Kutokana na dunia ya sasa kuwa kama kijiji, watu watakimbia nchi na kwenda kuzuri. Tanzania ina amani, watu wakarimu, wapole na rasilimali nyingi lakini tuna miundombinu ya kuendana na hali ilivyo sasa? Hapana!" aliongeza Simbachawene.

Aliendelea kueleza kuwa ni dhahiri tulikuwa tunahitaji Rais wa kujenga nchi na kila awamu huwa na vipaumbele vyake. Amani tunayo, ardhi nzuri tunayo, tuna madini, mbuga za wanyama na tunashangilia. Lakini nchi inajengwa?

"Dodoma squatter zilitaka kuingia. Dar imekuwa squatterized hadi kupanga tena huwezi! Mwanza vivyo hivyo. Kwanini tuna rasilimali nyingi lakini nchi haijengwi interms of miji, mabarabara, reli, airway wakati ni lazima uwe na mambo haya ndio nchi iitwe nchi? Hata ukiwa na nafasi nzuri lazima ujenge nyumba."

"Sasa nchi hii inajengwa kweli kweli. Baada ya miaka 5 au 10 ya Rais Magufuli tutajikuta Tanzania hata kama tunasema Rais sio rafiki wa mtu(Rais hapaswi kuwa rafiki wa mtu, anapaswa kuwa rafiki wa nchi zaidi na si kundi wala mtu) tuna maendeleo makubwa." Alisisitiza.

Aidha kuhusu suala la Serikali kuhamia Dodoma, Simbachawene ambaye alikuwa Waziri TAMISEMI kabla ya kujiuzulu wadhifa anasema iIlikuwa ngumu kukubaliana kuhamia Dodoma kwani baadhi ya Mawaziri walipinga sana walilalamika kuhusu kuacha familia na mali zao zilizopo Dar es Salaam.

Aliendelea kueleza, “Rais Magufuli alisema hiiiiiii mtahamia tu na hii ni process, inapofeli analaumiwa aliyeanzisha lakini inapofaulu ndipo mnajua kuwa kiongozi wenu ni jiwe”

Anasema haukuwepo mpango ulioandikwa ukapitishwa kuhusu Serikali kuhamia Dodoma lakini uamuzi ulishakuwepo toka 1973, miaka 40+ baadae ndo unatekelezwa, hivyo hakukuwa na maana ya kujadiliana na watu.

"Serikali yote iko Dodoma amebaki Rais wetu. Na yeye anaendelea kujenga pale Ikulu ya Chamwino Dodoma hivyo tunaamini Rais anaingia muda si mrefu." alimalizia Simbachawene.
 
VAPS

VAPS

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2012
Messages
2,443
Points
2,000
VAPS

VAPS

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2012
2,443 2,000
Hawa wasomi na wanasiasa waliopata fursa muhimu walipaswa kutulia na kutumia fursa walizopata kuwekeza viwanda nk kwani wana connection za uhakika. Ajabu kutwà kucha kujipendekeza kwa mtukufu wapewe vyeo/ Ajira.Nani kawalaani hawa!?
 
Tajiri Kichwa

Tajiri Kichwa

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2017
Messages
1,724
Points
2,000
Tajiri Kichwa

Tajiri Kichwa

JF-Expert Member
Joined Apr 2, 2017
1,724 2,000
Naona kakumbuka kuimba na kuabudu ..ikiwa waumini wameshajaa...huyu teuzi hapati tena
 
T

Timiza

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2017
Messages
4,902
Points
2,000
T

Timiza

JF-Expert Member
Joined Nov 29, 2017
4,902 2,000
Dodoma haina tija ktk kuinua uchumi wa taifa. Aahamie haraka anaweza asirudi 2020 siasa ni upepo akaishia kuiona kwenye tv
 
T

Timiza

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2017
Messages
4,902
Points
2,000
T

Timiza

JF-Expert Member
Joined Nov 29, 2017
4,902 2,000
Jengeni taasisi imara, acheni kujenga mtu imara.
Waliowahi kuwa kwenye system wakapuuxa kujenga taasisi imara walidhani hayawahusu walipuuza walipoambia,Leo wako nje wakisomeshwa no
 
utukufu mwanjisi

utukufu mwanjisi

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2017
Messages
2,089
Points
2,000
utukufu mwanjisi

utukufu mwanjisi

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2017
2,089 2,000
Simbachawene anaelewa anachokisema ndo mana kaongea hivo mana huwez ukaitaja Tanzania nw bila jina la magufuli
 
M

mpimamstaafu

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Messages
1,852
Points
2,000
M

mpimamstaafu

JF-Expert Member
Joined Jul 18, 2018
1,852 2,000
Wewe ulikubali?
 
samurai

samurai

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2010
Messages
5,926
Points
2,000
samurai

samurai

JF-Expert Member
Joined Oct 16, 2010
5,926 2,000
Simbachawene toka umekuwa kiongozi katika taifa hili mpaka leo tulitegemea uwe mfano wa kuigwa kwa kuajiri watanzania wasiopungua 1000 kwenye ajira rasmi na wengine deiworker lakini umegeuza siasa ajira sasa..

Ni vyema pia ukapeleka hoja binafsi bunge livunjwe tufanye kazi tuache maneno..
 
samurai

samurai

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2010
Messages
5,926
Points
2,000
samurai

samurai

JF-Expert Member
Joined Oct 16, 2010
5,926 2,000
Vipi ulipata nafasi ya kuuliza kwanini tunahamia dodoma kwa haraka hivyo?? Namaanisha concrete reason na sio ndoto ya Mwalimu na sababu zake za 1970...
 
M

MABAKULI

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Messages
1,046
Points
2,000
M

MABAKULI

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2015
1,046 2,000
Ungesema jiwe haliwezi kuja Dodoma kwani kubeba vote 20 sio mchezo ikiwa na 1.5 tr kwenye sandarusi
 
M

Mashilla

Member
Joined
May 14, 2019
Messages
50
Points
125
M

Mashilla

Member
Joined May 14, 2019
50 125
Haha nchi ya kutukuza. VP mbona hamuongelei upande was pili? Kuhamia Dom kumeisaidiaje nchi kiuchumi?
 
C

charles mususa

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2009
Messages
249
Points
225
C

charles mususa

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2009
249 225
Akakazane na baa yake pale Vingunguti.
 
W

Waluhwanoyena

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2018
Messages
387
Points
500
W

Waluhwanoyena

JF-Expert Member
Joined Sep 19, 2018
387 500
Ni Wizsra na wafanyakazi wa chini ndo wamehamia Dodoma kwenye mabanda ya mabati, Mawaziri bado wako Dar karivu na mteuzi wao hawataki kumwacha peke take maana atakuwa lonely atakosa wa kumsifia kwa juhudi anazofanya. Mkuu wao alikuwa ahamie, December lakini hadi Leo yuko Dar karibu na mdogo wake. Mleta mada anatafuta kurudishiwa uwaziri ameukosa siku nyingi wenzake wakila bata.
 
mhuri25

mhuri25

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2016
Messages
943
Points
1,000
mhuri25

mhuri25

JF-Expert Member
Joined Sep 3, 2016
943 1,000
Hawa wasomi na wanasiasa waliopata fursa muhimu walipaswa kutulia na kutumia fursa walizopata kuwekeza viwanda nk kwani wana connection za uhakika. Ajabu kutwà kucha kujipendekeza kwa mtukufu wapewe vyeo/ Ajira.Nani kawalaani hawa!?
Wakati mwingine jaribu kuwa unaunga hata mguu hoja.. sio kila kitu unakitizama in negative way..
 
nyabhingi

nyabhingi

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2010
Messages
13,746
Points
2,000
nyabhingi

nyabhingi

JF-Expert Member
Joined Oct 12, 2010
13,746 2,000
Huwa nashindwa kumtofautisha na musiba
Halafu kwenye ripoti ya mererani huyu alitajwa kusaini mkataba wa kilaghai but yuko huru
 
Nyangomboli

Nyangomboli

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2010
Messages
2,871
Points
2,000
Nyangomboli

Nyangomboli

JF-Expert Member
Joined Nov 24, 2010
2,871 2,000
Hawa wasomi na wanasiasa waliopata fursa muhimu walipaswa kutulia na kutumia fursa walizopata kuwekeza viwanda nk kwani wana connection za uhakika. Ajabu kutwà kucha kujipendekeza kwa mtukufu wapewe vyeo/ Ajira.Nani kawalaani hawa!?
Mtu akisema ukweli wa moyoni mwake kwako wewe ni kujipendekeza?
 
K

Kisampido

Senior Member
Joined
Jun 19, 2013
Messages
131
Points
195
K

Kisampido

Senior Member
Joined Jun 19, 2013
131 195
Mbona Na yeye anampinga Mh Rais ujenzi kituo cha afya mtera kwenye majengo waliyoyaacha wachina anataka veta Na ametamba Kwamba hakitajengwa kituo cha afya pamoja Na kuwa Mh Rais alitoa maagizo kijengwe kituo cha afya kabaki kulumbana Na DIWANI wa mtera mpka hawasalimiani none sense ili lijamaa.
 

Forum statistics

Threads 1,303,870
Members 501,152
Posts 31,495,706
Top