Simbachawene apiga marufuku Polisi kukamata wananchi, bodaboda bila kufuata utaratibu, Uchaguzi Mkuu wa Huru na Haki 2020

Bandamwagaz

Member
Feb 19, 2020
18
36
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amepiga marufuku Polisi kukamata wananchi, bodaboda pamoja na kufanya operesheni ya aina yoyote kwa kukurupuka bila kufuata utaratibu.

Amesema ukamataji wa aina hiyo unaweza kusababisha uvunjifu wa amani badala ya kujenga amani nchini.

Pia Waziri huyo aliagiza kuwa, kila operesheni itakayopangwa kufanywa na Polisi Nchini, wanapaswa watoe taarifa kwa Mkuu wa Wilaya ili ajue nini kitafanyika kwa kuwa yeye ni Mwenyikiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo, na pia ndio utaratibu unapaswa kuwa hivyo.

Akizungumza katika Kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama cha Wilaya ya Mpwapwa, Mkoani Dodoma na baadaye kulisisitiza agizo hilo katika Kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya, Simbachawene alisema ukamataji usio na mpangilio hauna tija na unaweza kuvunja amani badala ya kujenga amani.

“Wananchi wanawalalamikia askari wetu sana kukamata bodaboda bila sababu, sio bodaboda tu hata kukamata kamata hovyo watu, ukamataji mwingine unakua kama kukomoana, hauna tija, hauleti amani, badala yake unasababisha amani itoweke,” alisema Simbachawene.

Aliongeza kuwa, “Yaani msako fulani unatungwa hauna kichwa wala mguu, hauna maelekezo yoyote ya Mkuu wa Jeshi la Polisi au chombo, ni watu tu wanajitungia wanaondoka na pikipiki yao wamepakiana wanaenda kufanya operesheni ambayo haina utaratibu.”

Alisema vyombo vya ulinzi na usalama ni vya wananchi, na operesheni yoyote haipaswi kufanyika bila Mkuu wa Wilaya kupewa taarifa ambapo ndio utaratibu unapaswa kuwa hivyo.

Pia Waziri Simbachawene aliupongeza uongozi wa Wilaya hiyo kwa kuwa karibu na wananchi kwa kusikiliza kero zao na kuifanya Wilaya hiyo kuendelea kuwa na amani na utulivu na wananchi kuendelea kuwa na imani na viongozi hao.

“Endeleeni kuwa karibu na wananchi, kwa kusikiliza kero zao na pia kuzitatua, na epukeni malalamiko ya hapa na pale yasiyokuwa ya lazima,” alisema Simbachawene.

Aidha, Simbachawene aliewaomba viongozi wa Wilaya hiyo kujipanga vizuri katika maandalizi ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.

“Mwaka huu ni wa uchaguzi, wananchi kupitia vyombo vyetu vya ulinzi na usalama na taasisi zote za utawala, mnapaswa kuwa na ushirikiano mkubwa ili kujenga msingi wa uchaguzi utakaokuwa wa amani na utulivu,” alisema Simbachawene.

Alisema mwaka wa uchaguzi haupaswi kuwa na vurugu, ni mwaka ambao unapaswa kuwa na utulivu kwasababu ni jambo zuri la kidemokrasia linafanyika.

“Rai yangu kwa wananchi, kuhakikisha kwamba tunapaswa kujenga utulivu kuanzia sasa kuelekea uchaguzi mkuu, hatupaswi kuwa na vurugu, ni mwaka ambao amani na utulivu wa nchi unajengwa kuanzia sasa, mshikamano wa vyombo vyetu ndio msingi wa kujenga uchaguzi utakao kuwa wa huru na haki ambao utafanya mwaka huu,” alisema Simbachawene.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya hiyo, Jabir Shekimweri alimshukuru Waziri huyo na kuahidi kuyafanyia kazi maelekezo yake aliyoyatoa katika kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na Kikao cha Baraza la Madiwani.

Naye Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mpwapwa (OCD), ASP Maulidi Manu alisema ujio wa Waziri huyo umewasaidia zaidi kwa kujipanga zaidi, na kufuata maagizo yote aliyoyatoa kwa Jeshi la Polisi Wilayani humo.

“Tumefarijika kwa ujio wa Mheshimiwa Waziri, maagizo yake aliyoyatoa tunaahidi kuyafanyia kazi,” alisema Manu.

Waziri Simbachawene, alifanya ziara ya siku moja kwa ajili ya kukutana na Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na Baraza la Madiwani Wilayani humo.

*Mwisho/-*
PIX%205.JPG
PIX%206.JPG
PIX%201.JPG
PIX%203.JPG
PIX%202.JPG
PIX%204.JPG

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila siku wanakamata hovyo kama mkuu wa kituo cha luguruni ndo imekuwa kitengo watu wanakusanywa wanalundikwa kutoka bila 150000 mahabusu unakaa hadi unachakaa.
Pale round about ubungo kila jioni saa 1 hadi 4 usiku kuna vijana kibao wanajifanya askari wanakamata pikipiki kila siku na na polis wako sheli kule wanapelekewa mgao bila wasiwas kabisa hii ishakuwa kitengo cha uingizaji hela.
 
Pale Ubungo nafikiri ndio makao makuu ya traffic Tanzania sasa hivi kwani hata aibu hawana wanaomba rushwa kama pesa ni zao
 
Polisi wamekuwa waonevu na waporaji hasa kwa bodaboda wamewageuza mtaji, kuna mshiriki mwenzangu walimfanyia kama ambush wamemzongazonga wee na vitisho vya kumpeleka polisi kumsearch wakamkuta na elfu 80 wakaichukua na kumuachia na majeraha ya kutosha ikiwemo kuteguka mguu, na kwa sababu ya kuepusha kuhangaika nao kwa kesi hiyo ya uporaji wa polisi kaamua kuwaachia tu maana hakuwa na kosa lolote
 
Binafsi huwa siridhishwi na utendaji wa polisi wetu, kwa kujigeuza kuwa juu ya sheria, taratibu hata busara na kuwwnyanyasa wanaowalipa mishahara.

Maelezo haya ya waziri, ukiyatazama kwa juu utaona kama ni jambo jema lakini ukifafikiri utajiuliza vitu vichache.

Mosi, ni jambo jema kwa kuagiza polisi kuacha kukamata watu bila busara kwani Mara nyingi vitendo vinavyofanywa ni kana kwamba hawa. Jamaa wameshushwa kutoka huko wanapojua. Wao kwani ubinadamu ni msamiati mgumu kwao.
Pili, Je uchaguz mkuu ujao una msukumo juu ya tamko hili? Kwa maana katika kipindi hicho wafanya siasa wetu utawashuhudia wakiwa na kila rangi hasa zile za kuvutia.
Vingine, bwana waziri ungechukua hatua hata sasa kwa kuzuru kituo chochote cha polisi uzungumze na mahabusu, kisha ungechukua hatua kuanzia kwa RPC, ingekuwa vyema.

Hata hivyo hatua yako na ugeni wako katika wizara inaweza kuonyesha dhamira yako ya kufanya mabadiliko katika jeshi hill, lakini nachelea kusema kuwa hii itapimwa zaidi na miezi michache ijayo ambayo utaendelea kuwa katika nafasi Huyo. Wengi huanza hivi lakini...
 
Kila siku wanakamata hovyo kama mkuu wa kituo cha luguruni ndo imekuwa kitengo watu wanakusanywa wanalundikwa kutoka bila 150000 mahabusu unakaa hadi unachakaa.
Pale round about ubungo kila jioni saa 1 hadi 4 usiku kuna vijana kibao wanajifanya askari wanakamata pikipiki kila siku na na polis wako sheli kule wanapelekewa mgao bila wasiwas kabisa hii ishakuwa kitengo cha uingizaji hela.

Aisee, hawa askari a.k.a Tigo na pikipiki zao wanakera hadi inapitiliza. Barabarani hawa ndio wanaongozwa
kuchukiwa na watu
 
Waziri, tusaidie hapa Mugumu Serengeti, kwani hawa polisi wamevuka viwango vya kuyakadiria mambo!
Mbali na kukamata hovyo; lakini wanakamata hata kama umepaki mbali na barabara, au hata nje nyumba yako. Ilimradi waione ni pikipiki.

Mbaya zaidi wakikosa ufunguo wanakata waya za stata, na kuwasha kienyeji, na kuondoka nayo!
Jamani huu sasa ni uharibifu wa mali za watu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya Matamko tumeshayazoea kila uchaguzi unapokaribia ili kuwapumbaza Wananchi

Uchiaguzi ukishapita mambo yanarudi palepale.
 
Kitendo tu kuita watu boda boda badala ya madereva pikipiki,ni kuwachukulia watu wasiojitambua.mtu kaamua asivae helmet,viatu,jacket halafu unataka asikilizwe.siasa za kishenzi zinaghalimu taifa.hana tofauti na aliyeagiza pikpik zisijae kituoni akidhani labda kuna aliyeonewa.
 
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amepiga marufuku Polisi kukamata wananchi, bodaboda pamoja na kufanya operesheni ya aina yoyote kwa kukurupuka bila kufuata utaratibu.

Amesema ukamataji wa aina hiyo unaweza kusababisha uvunjifu wa amani badala ya kujenga amani nchini.

Pia Waziri huyo aliagiza kuwa, kila operesheni itakayopangwa kufanywa na Polisi Nchini, wanapaswa watoe taarifa kwa Mkuu wa Wilaya ili ajue nini kitafanyika kwa kuwa yeye ni Mwenyikiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo, na pia ndio utaratibu unapaswa kuwa hivyo.

Akizungumza katika Kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama cha Wilaya ya Mpwapwa, Mkoani Dodoma na baadaye kulisisitiza agizo hilo katika Kikao cha Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya, Simbachawene alisema ukamataji usio na mpangilio hauna tija na unaweza kuvunja amani badala ya kujenga amani.

“Wananchi wanawalalamikia askari wetu sana kukamata bodaboda bila sababu, sio bodaboda tu hata kukamata kamata hovyo watu, ukamataji mwingine unakua kama kukomoana, hauna tija, hauleti amani, badala yake unasababisha amani itoweke,” alisema Simbachawene.

Aliongeza kuwa, “Yaani msako fulani unatungwa hauna kichwa wala mguu, hauna maelekezo yoyote ya Mkuu wa Jeshi la Polisi au chombo, ni watu tu wanajitungia wanaondoka na pikipiki yao wamepakiana wanaenda kufanya operesheni ambayo haina utaratibu.”

Alisema vyombo vya ulinzi na usalama ni vya wananchi, na operesheni yoyote haipaswi kufanyika bila Mkuu wa Wilaya kupewa taarifa ambapo ndio utaratibu unapaswa kuwa hivyo.

Pia Waziri Simbachawene aliupongeza uongozi wa Wilaya hiyo kwa kuwa karibu na wananchi kwa kusikiliza kero zao na kuifanya Wilaya hiyo kuendelea kuwa na amani na utulivu na wananchi kuendelea kuwa na imani na viongozi hao.

“Endeleeni kuwa karibu na wananchi, kwa kusikiliza kero zao na pia kuzitatua, na epukeni malalamiko ya hapa na pale yasiyokuwa ya lazima,” alisema Simbachawene.

Aidha, Simbachawene aliewaomba viongozi wa Wilaya hiyo kujipanga vizuri katika maandalizi ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.

“Mwaka huu ni wa uchaguzi, wananchi kupitia vyombo vyetu vya ulinzi na usalama na taasisi zote za utawala, mnapaswa kuwa na ushirikiano mkubwa ili kujenga msingi wa uchaguzi utakaokuwa wa amani na utulivu,” alisema Simbachawene.

Alisema mwaka wa uchaguzi haupaswi kuwa na vurugu, ni mwaka ambao unapaswa kuwa na utulivu kwasababu ni jambo zuri la kidemokrasia linafanyika.

“Rai yangu kwa wananchi, kuhakikisha kwamba tunapaswa kujenga utulivu kuanzia sasa kuelekea uchaguzi mkuu, hatupaswi kuwa na vurugu, ni mwaka ambao amani na utulivu wa nchi unajengwa kuanzia sasa, mshikamano wa vyombo vyetu ndio msingi wa kujenga uchaguzi utakao kuwa wa huru na haki ambao utafanya mwaka huu,” alisema Simbachawene.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya hiyo, Jabir Shekimweri alimshukuru Waziri huyo na kuahidi kuyafanyia kazi maelekezo yake aliyoyatoa katika kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na Kikao cha Baraza la Madiwani.

Naye Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mpwapwa (OCD), ASP Maulidi Manu alisema ujio wa Waziri huyo umewasaidia zaidi kwa kujipanga zaidi, na kufuata maagizo yote aliyoyatoa kwa Jeshi la Polisi Wilayani humo.

“Tumefarijika kwa ujio wa Mheshimiwa Waziri, maagizo yake aliyoyatoa tunaahidi kuyafanyia kazi,” alisema Manu.

Waziri Simbachawene, alifanya ziara ya siku moja kwa ajili ya kukutana na Kamati ya Ulinzi na Usalama pamoja na Baraza la Madiwani Wilayani humo.

*Mwisho/-*View attachment 1371201View attachment 1371202View attachment 1371203View attachment 1371204View attachment 1371205View attachment 1371206

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapa ndio jimboni kwake au?
 
Aliyejichinbia juu sn aneagiza polisi waue na wasisumbuliwe wakifanya hivo sasa simbachawene kukamata kuna shida gani wkz wanaruhusiwa kuua bila kuhojiwa?
Tengua kauli ya rais kwanza kuhusu uhalali wa kuua watz bila kuchukuliwa
 
Issue kama bodaboda ,ile ni ajira kama ajira nyingine hawa wangepewa utaratibu,mfano kuingia lango la city centre ,bodaboda unalipa 500 unaingia pale mapato ya jiji yangekusanywa.huu usafili unasaidia sana kama mtu una mambo yako ya haraka na kwa vijana ni ajira pia.
kuliko kuwakamata tena wale wakamataji wanafanya kumdandia mtu wakati yuko kwenye speed.
 
Pia Mh waziri awatete na wa daladala.

Leoasubuhi nimetoka pale buguruni sheli na daladala kwenda mbagala...aisee kuanzia pale temeke sudan konda akaanza kutoa rushwa buku 3 akaja kutoa tena mtongani akamalizia Rangi 3 ni kama elfu 9 imetoka nikamuuliza dereva kwanini wanatoa pesa kirahaisi na wakati gari ni mpya? Jibu nililopewa "Aah kaka hao bila kujipendekeza njia utaihama hii kwa faini bora utoe hiyo buku 3 uepukane na elfu 30"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom