Simbachawene ampongeza CGP kwa mabadiliko makubwa Magereza, azindua mashine ya kuchimbia 'excavator' ya milioni 331

Bandamwagaz

Member
Feb 19, 2020
18
36
_Na Mwandishi Wetu, MOHA, Morogoro._

*WAZIRI* wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amesema kasi ya utendaji kazi wa Kamishna Generali wa Jeshi la Magereza Nchini, (CGP) Suleiman Mzee, imemfurahisha kutokana na mabadiliko makubwa ya maendeleo kwa kipindi cha muda mfupi tangu alipoteuliwa kuliongoza Jeshi hilo.

*Akizungumza katika hafla* ya kuzindua mashine ya kuchimbia excavator iliyofanyika Gereza la Mbigili, Wilaya ya Mvomero, Mkoani Morogoro, leo, Waziri Simbachawene alisema Jeshi la Magereza lilinufaisha wachache katika kipindi cha nyuma, lakini tangu kuteuliwa kwa CGP Mzee, mafanikio makubwa yameanza kuonekana.
" *CGP tangu ateuliwa kwa* muda mfupi tuu, amenunua matipa matatu, basi la timu ya mpira na mashine hii excavator kwa fedha zilizopatikana ndani ya Jeshi, haya mambo yalikuwa ni ndoto jamani, utendaji kasi yake mzuri na anania ya kuleta mabadiliko zaidi ndani ya Jeshi hili la Magereza, nimefurahishwa sana na utendaji kazi wake na fikisheni pongezi zangu," _alisema Simbachawene._

*Aliongeza kuwa, askari* na maafisa wa Jeshi hilo Nchini, hawapaswi kumpinga, wanapaswa kumuelewa na kumuunga mkono na kuendana na kasi yake katika kipindi hiki ambacho Jeshi limeingia vitani kwa ajili ya kufanyika kwa mabadiliko makubwa.
Pia aliwataka askari Magereza kuendelea kufanya kazi usiku na mchana, na kila mtu akitoka kazini ajiulize nini amefanya kwa siku hiyo, kwa hatua hiyo itawezesha jeshi kubadilika zaidi katika uzalishaji na pia maisha ya askari nayo yatabadilika.

*Aidha, Waziri* Simbachawene katika hafla hiyo, ameitambulisha kauli mbiu mpya ya Jeshi hilo nchini ambayo inasema Magereza Tanzania, Fikra Mpya, Mtazamo Mpya, Kuchapa Kazi kwa Bidii na Kujitegemea.

*Kwa upande wake Mkuu* wa Magereza Mkoa huo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi hilo (SACP), Ismail Mlawa, alimshukuru Waziri Simbachawene kwa jitihada zake za kuliletea mabadiliko Jeshi hilo, na pia anamuomba Mheshimiwa Rais John Magufuli amrudishe katika Wizara hiyo baada ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.

*Mheshimiwa Waziri,* tunakushukuru sana kwa kuja kuzindua mashine hii mpya, na pia hizi ni jitahada zako pamoja na Afande Kamishna Generali wa Jeshi hili, tunaamini nawe umechangia kupatikana kwa mashine hii pamoja na vifaa vingine, tunakuombea urudishwe kuiongoza Wizara hii hata baada ya uchaguzi, alisema Mlawa.

*Naye Mkuu wa Gereza la* Mbigili, lililopo Wilayani Mvomero, Mkoani humo, SSP Muyengi Burilo, akisoma taarifa ya Gereza hilo pamoja na mashine hiyo mpya iliyonunuliwa, alisema mashine hiyo imenunuliwa shilingi milioni 331,060,800 na itakuwa inachimba visima, kungoa miti, kuchimba mitaro na pia itatumika kukodisha katika Taasisi mbalimbali za Serikali.

*Mwisho/-*
IMG_-tfmdy5.jpg
IMG_-orxlid.jpg
PIX%208.JPG
811A9889.JPG
IMG_m27u0q.jpg
 
Kwa kweli CGP mpya anastahili pongezi nasikia huko magereza zoezi la kujilisha wenyewe limefanikiwa ni miezi mitatu sasa hakuna pesa ya chakula kwa wafungwa iliyotolewa na serikali hongera sana CGP mzee
 
Nilijua jeshi la magereza wameunda hiyo "excavator"..... kumbe ni ya kununua! Zinduzi nyingine jamani.....haya, tutafika tu.
 
Sio kama napinga jamani kama machadema mlivyosema ila dah, kibongo bongo bado sana jamani, waziri anaenda kuzindua excavator moja, tena ya mchina? Hii hata CGP hakutakiwa kuzindua, ingezinduliwa na mkuu wa gereza tu.

Mimi sio chadema jamani narudia tena!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom