Simbachawene aagiza Afisa Biashara wa H/shauri ya Dodoma na Kaimu wake wasimamishwe Kazi

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
6,042
10,787
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. George Simbachawene amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma kuwasimamisha kazi mara moja Kaimu Afisa Biashara wa Manispaa ya Dodoma Bw. Elias N. Kamara na Bibi Donatila D. Vedasto (Afisa Biashara) kuanzia leo tarehe 30/12/2015 kwa kosa la kusababisha urasimu katika utoaji wa leseni za biashara.

Kutokana na hali hiyo Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kumuondoa kwenye nafasi yake Kaimu Afisa Biashara wa Manispaa na Msaidizi wake na nafasi zao kukaimishwa kwa watu wengine ili kupisha uchunguzi dhidi ya tuhuma zilizotolewa dhidi yao.

Agizo hili limetolewa na Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais -TAMISEMI baada ya kupokea malalamiko mengi kutoka kwa wafanyabiashara ambayo yalionyesha kuwepo kwa mazingira ya rushwa.

Katika uchunguzi ambao umefanyika katika Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma imegundulika kuwa kulikuwa na maombi ya leseni 750 ambayo yalikuwa hayajashughulikiwa bila sababu za msingi na hali hiyo ilipelekea kuikosesha Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kiasi cha shilingi Milioni 75.

Aidha, Mhe. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI ameagiza Mamlaka za Serikali kote nchini kuhakikisha wanatoa leseni za biashara bila urasimu wowote na muombaji apate leseni ndani ya siku 2 au 3 anapoomba leseni.

Mhe. Simbachawene ametoa agizo kwa Maafisa biashara wote nchini kuacha urasimu katika kutoa leseni na kujiepusha na vitendo vya rushwa.

Imetolewa na:
Rebecca Kwandu
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Ofisi ya Rais - TAMISEMI
 
Safi sana, yaaani ukifika kufatilia maombo yako unakuwa kama unawaomba vile wakati
ni haki yako na umeilipia. Tanzania , hakuna "customer care " kwa watendaji wengi.
 
Yaanzishwe magereza maalumu kama yale ya Quantananmo kwa watumishi wa umma wakati wakisubiria uchunguzi ufanyike.
 
Bado watoaji wa vibali vya ujenzi, hasa Halmashauri ya Jiji Mbeya. Inachukua miezi 3 kupata kibali cha ujenzi.
 
Duh..... Kwa mwendo huu wa kauli mbiu ya awamu ya 5 ya hapa kazi tu.
Kwa mwendo huu wa fukuza fukuza wanayoiendesha baraza jipya la mawaziri, upo uwezekano mkubwa hadi itakapofika Desemba ya mwaka 2016, tusije shangaa kukuta idadi hadi nusu ya wafanyakazi wote wa serikalini na kwenye mashirika ya Umma wakajikuta weshatimuliwa kazi!
 
Vinzuri kwani alizoea kupoke rushwa. Vile vile kuwe na database ya hawa wafanyakazi wanaofukuzwa kwa rushwa na wizi, itasaidia kupunguza rushwa na wizi wakijua itawapa reference mbaya kwenye ajira zijazo.
 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. George Simbachawene amemuagiza Mkurugenzi wa
Manispaa ya Dodoma kuwasimamisha kazi mara
moja Kaimu Afisa Biashara wa Manispaa ya
Dodoma Bw. Elias N. Kamara na Bibi Donatila D.
Vedasto (Afisa Biashara) kuanzia leo tarehe
30/12/2015 kwa kosa la kusababisha urasimu
katika utoaji wa leseni za biashara.

Kutokana na hali hiyo Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais TAMISEMI amemuagiza Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kumuondoa
kwenye nafasi yake Kaimu Afisa Biashara wa
Manispaa na Msaidizi wake na nafasi zao
kukaimishwa kwa watu wengine ili kupisha
uchunguzi dhidi ya tuhuma zilizotolewa dhidi yao.

Agizo hili limetolewa na Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi
ya Rais -TAMISEMI baada ya kupokea malalamiko
mengi kutoka kwa wafanyabiashara ambayo
yalionyesha kuwepo kwa mazingira ya rushwa.

Katika uchunguzi ambao umefanyika katika
Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma imegundulika
kuwa kulikuwa na maombi ya leseni 750 ambayo
yalikuwa hayajashughulikiwa bila sababu za msingi
na hali hiyo ilipelekea kuikosesha Halmashauri ya
Manispaa ya Dodoma kiasi cha shilingi Milioni 75.

Aidha, Mhe. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais –
TAMISEMI ameagiza Mamlaka za Serikali kote
nchini kuhakikisha wanatoa leseni za biashara bila
urasimu wowote na muombaji apate leseni ndani ya
siku 2 au 3 anapoomba leseni.
Mhe. Simbachawene ametoa agizo kwa Maafisa
biashara wote nchini kuacha urasimu katika kutoa
leseni na kujiepusha na vitendo vya rushwa.

Imetolewa na:
Rebecca Kwandu
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Ofisi ya Rais - TAMISEMI
30 Desemba, 2015
 
Ni shidaa. Kwa hiyo mtu akilalamika tu tayari unasimamishwa kazi. Ni lini uchunguz unakua umefanyika ili kutofautisha majungu na tuhuma za kweli?!Hadi miez6 ipite kuna watu watakua wameathirika sana!
 
CHUNGULIA NA MAOMBI YA KUTAKA VIWANJA PIA. DODOMA NI TATIZO NDIYO MAANA WATU WANACHOKA NA KUVAMIA MAENEO YA PEMBENI. HALAFU WANAKUJA KUBOMOLEWA..KODI ZINACHOSHA KULIPA PANGO @ MWEZI !
 
Wanajifanyaga mamwinyi sana hao maafisa.
Usikute walizilimbnikiza izo wakisubili rushwa maana ndo zao
 
CHUNGULIA NA MAOMBI YA KUTAKA VIWANJA PIA. DODOMA NI TATIZO NDIYO MAANA WATU WANACHOKA NA KUVAMIA MAENEO YA PEMBENI. HALAFU WANAKUJA KUBOMOLEWA..KODI ZINACHOSHA KULIPA PANGO @ MWEZI !
Sasa nenda CDA kuomba hati. Wanakuambia gharimia michoro itengenezwe na manispaa upate hati. Gharama n mamilioni. Viwanja waliisha gawa tangu miaka ya tisini eti hadi leo michoro haijapitishwa. Huku majumba yamejaa ploti zote. Ebu mheshiwa waziri husika amrisha hao CDA watoe hati vinginevyo kuna majipu yameiva yatumbuliwe haraka watu tupate hati zetu kwani hakuna sababu ya msingi inayotolewa.
 
Ni shidaa. Kwa hiyo mtu akilalamika tu tayari unasimamishwa kazi. Ni lini uchunguz unakua umefanyika ili kutofautisha majungu na tuhuma za kweli?!Hadi miez6 ipite kuna watu watakua wameathirika sana!
Umeambiwa kuna maombi zaidi ya 700 yamekaliwa na watu wanakula mshahara huku wafanya biashara wakihangaika. Unahitaji uchunguzi upi.?
 
Back
Top Bottom