Simba yatia aibu usajili wa Yusufu Mhilu, inategemea tena TFF iibebe kama kwa Morrison

kwenye hili unamsikiliza mchambuzi au kiongozi wa Kagera?
Kagera wangekua wasafi hivyo katika hili suala wasingesema hatutoshitaki kokote,

Pia mimi nimeelezea nilivyosikia, na mwisho nimetoa mawazo yangu, ila wewe kwakua ni mwana Yanga unataka tuongelee vibaya upande usioupenda, sidhani kama ukija katika mtazamo huo tutafika kokote katika kujadili
 
Mimi nadhani mchezaji mwenyewe (Muhilu) alipoona labda ada ya kusajiliwa ni kubwa tofauti na iliyopo kwenye mkataba kuna uwezekano aliingia tamaa akaamua awaoneshe Simba masharti ya mkataba, na simba kwa upuuzi wakashindwa kufata makubaliano na Kagera wakaona wawazunguke Kagera ili kama kuna uwezekano wampe Muhilu pesa ili akaununue mkataba, then kagera kuona hivyo wakaona dili lao linaingia mchanga ndio wakaamua kulitibua

So hapo ni Muhilu mwenyewe ndio amejiweka kitanzini kwa ninavyohisi mimi, maana ukiangalia sababu ya Muhilu kuamua kwenda TFF ni haina mashiko, nahisi ni tamaa tu ya kupata pesa nyingi ndio imemsababishia yote haya

Ila Simba wanatakiwa washitakiwe na Kagera, maana kulimaliza kimya kimya ni kuendelea kulea upuuzi kama huu
Mwizi ni mwizi TU sio lazima akamatwe na aliyemuibia. Ilipofikia hata mimi kwa niaba ya mpira naweza kuishitaki Simba TFF na FIFA kwa kosa la kumtambulisha mchezaji mwenye mkataba na timu yake.
 
Kagera wangekua wasafi hivyo katika hili suala wasingesema hatutoshitaki kokote,

Pia mimi nimeelezea nilivyosikia, na mwisho nimetoa mawazo yangu, ila wewe kwakua ni mwana Yanga unataka tuongelee vibaya upande usioupenda, sidhani kama ukija katika mtazamo huo tutafika kokote katika kujadili
Kosa limeshatendeka kilichobaki ni kosa la kumtambulisha mchezaji mwenye mkataba na timu yake adhabu yake ni ipi? Nothing more nothing less.
 
Hapa kwa kweli Simba wamepepesa na iwapo Kagera wakiamua kusimama kidete bila kuchoka mpaka FIFA watapata haki yao na ziada kidogo. Huwezi kumtangaza mchezaji ambaye bado ana mkataba halali na timu yake bila kwanza kumalizana na hiyo timu yake. Na kitendo walichofanya Simba ni kosa kubwa na kukosa weledi hasa kwa timu inayojua taratibu za uhamisho mpaka wa kimataifa na inayojinasibu kila siku kuwa inataka kuwa klabu kubwa Afrika kama Al haly, Mamelodi, n.k.

Lakini yote kwa yote ni vyema Simba na mchezaji mwenye Mhilu wakajirudi wakawafuata Kagera wakazungumza nao na kufikia makubaliano ambayo yatazinufaisha pande zote tatu Simba, Mhilu na Kagera katika hali ya "win win situation". Mazungumzo siku zote huondoa sintofahamu zote na kuleta maelewano ya kudumu lakini kesi inapofika mwisho huacha makovu na huzaa uadui wa kudumu kati ya aliyeshinda na aliyeshindwa.
 
Hata kama Simba na Mhilu wakienda Kagera Sugar kulimaliza bado hakufuti kosa la kumtambulisha Muhilu kabla ya wakati. Fanya utakavyofanya kosa limeshatendeka. Hata mwenyekiti wa Simba Mzee Mangungu amevuliwa nguo, maana nae hajui cha kusema na pengine hawakumshirikisha kwenye upuuzi huu.
 
Kagera wamesema mpaka sasa bado wanajadiliana na Simba na hawajaamua kushitaki lakini vichambuzi uchwara na utopolo wameshaanza kuishutumu TFF wachukue hatua, hivi TFF inaweza kuchukua hatua bila klabu husika kulalamika? Mbona hao wachambuzi hawazungumzii Plujim kutaka kwenda FIFA kutookana na pesa anazoidai yanga wamebaki kukomalia mambo ya Simba au wanafikiri wakiikomalia Simba nafasi ya ubora ya utopolo itaongezeka.
 
it is not over till is over, Simba wasingemtangaza na kumtambulisha kuwa ni mchezaji wao hadi pale ambapo wamemaliza mabishano ya uhamisho.

Kosa kama hili likiachwa lipite litavuruga hukumu za makosa kama haya siku zijazo (presidency), na hata adhabu yake atatumiwa kwa makosa mengine yajayo. Ili kutenda haki kwenye soka leo na kesho lazima tuangalie FIFA, CAF, na CECAFA wanatoa adhabu gani kwa timu ikimtangaza mchezaji mwenye mkataba halali na timu nyingine.
makosa ya kutolipa wachezaji na makocha mbona huyazungumzii
 
Mimi nimemsikiliza Farhan Kiamu yule mchambuzi wa michezo Clouds, alisema amelifatilia hilo suala na kilichotokea ni hiki, nanukuu

"Simba walimalizana na Muhilu na walikua tayari wamewasiliana na Kagera Sugar na offer ya usajili ilikua imekubaliwa na pande zote mbili

Lakini walipokua hatua ya mwisho ikaja kugundulika kuwa kwenye mkataba wa Muhilu kuna kipengele kinachosema kama unataka kumchukua mchezaji huyu inabidi uchukue mshahara wa Muhilu uuzidishe mara muda wa mkataba uliobakia na timu ya Kagera,

So walipochukua mshahara wa Muhilu anaoupokea Kagera wakazidisha mara 12 (mwaka mmoja) ikaonekana pesa ni ndogo tofauti na kiasi walichokubaliana na Kagera ili wauvunje mkataba, so simba wakaona walitaka kupigwa na ndipo hapo wakasimama na mkataba unavyosema

Kitu hicho kikafanya kutokuelewana kati ya viongozi wa kagera na Simba ndio maana kagera wameamua kuja kutafuta public sympathy ili wasaidiwe na nguvu ya umma" mwisho wa kunukuu

Ila yote kwa yote Simba bado wanaingia matatizoni maana walikosea kumtangaza mchezaji bila kukubaliana na timu aliyotoka
Mhilu alikwenda tff kudanganya hana mkataba na Kagera ili uweje?
 
Timu kubwa zinanunua wachezaji wa nje kwa bei kubwa lakini wanataka kuzidhulumu timu zetu ndogo kwa hela ndogo kununua wachezaji wenye uwezo mkubwa uwanjani kuliko wachezaji wa nje akina Chikwendwe, Sarpong, Kahata, nk. Huu ni mtihani wa kwanza wa Karia tangu urudi tena TFF.
Ukiinflate soko la ndani automatically utaua vilabu vidogo kwa sababu vitashindwa kabisa kusajili wachezaji.

Kagera Sugar siku zote they have issues with Simba toka wapande ligi kuu sijajua ni kwanini
 
Hata kama Simba na Mhilu wakienda Kagera Sugar kulimaliza bado hakufuti kosa la kumtambulisha Muhilu kabla ya wakati. Fanya utakavyofanya kosa limeshatendeka. Hata mwenyekiti wa Simba Mzee Mangungu amevuliwa nguo, maana nae hajui cha kusema na pengine hawakumshirikisha kwenye upuuzi huu.
Ni kweli hata mimi siungi mkonona hamna namna Simba wanaweza kuficha hii aibu. Ila nimetoa ushauri tu namna ya kulimaliza hili suala kiungwana kabisa bila kumuacha Mhilu akiwa majeruhi. Washauri wabovu inaonekana wameshauri Mhilu aende akavunje mkataba TFF lakini wanashindwa kujua kuwa suala la kuvunja mkataba lilipaswa kuanza kabla ya kutambulishwa na si vinginevyo. Kosa limeshatokea Simba na Mhilu wamechemsha wazi wazi ndio maana nikashauri kiutu uzima waende wakakae chini na Kagera wayamalize kiustaarabu na sio kijanjanja kwa Mhilu kununua mkataba kwani ndio wanazidi kuharibu kabisa.
 
Kagera wamesema mpaka sasa bado wanajadiliana na Simba na hawajaamua kushitaki lakini vichambuzi uchwara na utopolo wameshaanza kuishutumu TFF wachukue hatua, hivi TFF inaweza kuchukua hatua bila klabu husika kulalamika? Mbona hao wachambuzi hawazungumzii Plujim kutaka kwenda FIFA kutookana na pesa anazoidai yanga wamebaki kukomalia mambo ya Simba au wanafikiri wakiikomalia Simba nafasi ya ubora ya utopolo itaongezeka.
Muhilu katambulishwa au hakutambulishwa na Simba kama mchezaji wao? jibu hilo kwanza acha umbayuwayu!! Kwa maslahi ya mpira, kama Kagera hawatalalamika mtu yeyote anaweza kulalamika.
 
Back
Top Bottom