Simba, Yanga... Kulikoni Klabu zetu?

Morani75

JF-Expert Member
Mar 1, 2007
613
19
Heshima mbele Wakuu!!! Duh yaani kama mshabiki mkubwa sana wa timu za nyumbani imenisikitisha sana pale ambapo timu zetu za Yanga (kupigwa 2-1 tena nyumbani bao moja kapa) na Simba (kupigwa 7-1) na kutolewa katika mashindano ya vilabu barani Afrika.
Wapenzi wenzangu wa soka letu la Bongo hebu nisaidieni manake nimekuwa naangalia lakini sioni penye utupu au ni Makocha?? Najua klabu zetu nyingi hazina pesa lakini mbona hizi mbili kidogo ndio zinajitutumua mpaka kuleta makocha wa Ulaya (Serbia) and yet tunapigwa mabao tu n vilabu vya nje?? Au ni wizara/taasisi za michezo ndio zinatuangusha?????
 
nakumbuka mchazaji mmoja wa senagal alipotoa comment zake baada game ya tz na senagal taifa dar.....wachezaji wenu wazuri sana wanacheza kila mtu anavyojua kwa uwezo wake..hawachezi kitimu na pia hawana nguvu za kugombania mpira na kumiliki mpira...kutoa pasi na mbinu za kufunga.................ni hilo tuu...........
 
Hawa waliopo hawafundishiki...cha msingi utaratibu makini uwekwe kuanzia kwa vijana wadogo hapo tu ndo itakuwa pona yetu otherwise kila mtu atakuwa anakuja kujipatia umaarufu kupitia Tanzania.
Ni hayo tuu..
 
Duh, manake jamaa wamekuwa hawafundishiki..... Unajua nakumbuka zamani kulikuwa na Yanga Kids, Simba kids nk, siku hizi naona mambo yamekuwa mambo ukizingatia pia kuwa hata zile parastatals zilizokuwa zina timu za soka nyingi zimekufa (oooops zimebinfsishwa) zikiwemo Sigara tumebakiwa na maafande wetu wa Prisons, Polisi lakini hawa nao inaonekana kama nguvu ya Simba na Yanga inawamaliza manake hata kama wanaweza kuipiga Simba mabao still wanaishia kwenye ligi tu huko nje hata nguvu ya kwenda hawana... sasa hili nalo ni uwezo wa Simba na Yanga ndani au ndani wanabebwa na Makocha/TFF lakini nje since hakuna wa kuwabeba wanaishia..............

Lazima kuna mchawi mahali jamani.....
 
Kwanza kabisa nampongeza mto mada,suala hili ni la msingi lijadiliwe tena kwa kina na sio kulipapasa jujuu.Katika soka letu hapa TZ bado kuna tatizo kubwa ambalo halijatafutiwa ufumbuzi.Taifa star kafungwa Kenya,Simba kafungwa,Yanga nao ndio walewale.

Hivi wasomi tulionao wameshindwa kufanya tafiti juu ya suala hili?Kwa sababu hapa lazima kuna tatizo.Haya kama Taifa Star walipelekwa mpaka Bungeni,Wameleta makocha wakigeni lakini mambo naona ndio yanazidi kuwa mabaya.Na suala hili lakuleta makocha wa kigeni nadhani washika dau katika soka wamekulupuka lakini naamini hawakufanya tafiti kwanza kabla ya kuwaleta hawa wazungu.

Kocha unaemleta hajui kiswahili,yeye anajua kiingereza tena sio kile original,namaanisha sio lugha yao ya awali,mchezaji kiingereza hajui,hapa unategemea nini kitafanyika kama sio mparaganyiko wa mambo.

Kuwachukua makocha wa kigeni mimi sidhani kama itatusaidia kupandisha soka letu,haya mawili ningependekeza yafanyike kwanza,(i)makocha hawa wakifika TZ,wapelekwe shule kwanza wajifunze kiswahili hivyo itasaidia kufundisha kiswahili,mchezo kidogo unaweza kunoga,(ii)kama hiyo itakua haitoshi wachezaji wetu wafundishwe kiingereza kwanza,mimi naona lugha ni tatizo.Nasema hivyo kwa sababu kiingereza tusidanganyane ni kigumu,wewe chuku hata wanaomaliza mlimani wasikilize kiingereza chao ndio utaona lugha hii WATZ bado tuko nyuma,sembuse hawa Form 4,hapa tunadanganyana,soka haiwezi kupanda kwa mfumo huu.Tutabakia kichwa cha mwendawazimu kama alivyosema mzee wa Ruksa.LUGHA JAMANI.

Au kwa nini tusiwapeleke makocha wetu wakaenda kusoma huko halafu wakaja kutufundishia vijana wetu?Hii kasumba ya wageni mbona tunarudi kwenye ukoloni?Naliacha kwenu wadau na mseme.
 
a.97....., asante kwa kuliona hilo Mkuu!! Kwa kweli sasa hivi tuaachia mambo ya soka yaende mrama (ndicho kilichobaki na chenye kuweka waTz wengi sana kwenye mshikamano wetu, angalia vijiweni), lazima tuangalie kulikoni...Bendera being a long time coach na mtu anayelijua soka nilitegemea sana kuwa anegtutoa kimasomaso waTz katika hili la soka lakini naona yupo kimya (au ni mimi ndio sioni??)

Wadau, kweli kuna ligi kubwa za kuangalia (Premier, Bundesliga, Serie A etc) lakini jamani maji yakimwagika (nadhani ndio tuendapo huko) basi cha kutuweka pamoja ni michezo na sisi Bongo ni Soka mtu wangu..... Angalia Irak, Kenya na mechi yetu ya last week etc!!!

Naomba kuwakilisha....
 
kila mtanzania ana klabu either spain, england au italy.
na ukitembea mtaani utakutana na watanzania weeeengi wamevaa jezi za timu za ulaya na ukiwacheki mgongoni utakuta majina ya wale wachezaji wa ulaya mara fabregas, mara delpiero mara kaka, mara rui costa so ni kuwa wameshachoshwa na uozo uliokomaa wa vilabu vya hapa nyumbani.

waswahili wanasema "hata mbuyu ulianza kama mchicha" ila mi ninavyoona mchicha huu wa bongo umedumaa, so ni bora ukatwe na tupande zao jingine.

mi nashauri ni bora sasa tujaribu mchezo mwingine, kama wenzetu wakenya walivyokomaa na mbio.
 
Mpira Wetu Utakuwa Hivyo Hivyo Milele Maana Wa Tz Tumejawa Na Football Fitna Tuu Ajili Ya Simba Na Yanga Kushinda Mechi Zao..na Kujinufaisha Wenyewe..........si Kukuza Soka
 
Duh.... Kaaz kweli kweli lakini naona Mzee Tenga ameamua kukata mzizi wa fitina katika yale niliyosema ya kuwa na timu chipukizi..... Hii ni kwenye Majira la leo:

Tenga azitaka Simba, Yanga kujali vijana
Na Sophia Ashery

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetoa somo kwa klabu za Simba na Yanga kuhakikisha zinatengeneza vikosi vya timu zake ikiwa ni pamoja na kutengeneza wachezaji vijana.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Rais wa TFF, Leodger Tenga, alisema kwa kufanya hivyo kuna uwezekano mkubwa wa klabu hizo kuwa na maendeleo makubwa ya kisoka ikiwa ni pamoja na kupunguza mzigo wa magoli katika mashindano ya kimataifa wanayocheza.

Tenga alisema licha ya klabu hizo kuchukua muda mrefu kupata mafanikio kama klabu za nchi nyingine, kuna uwezekano mkubwa wa kufanya vizuri kama uongozi wa klabu hizo ukiimarisha vikosi vyake.

Alisema kwa kutambua umuhimu wa maendeleo ya soka ya klabu hizo ambapo mara kwa mara wamekuwa wawakilishi wa mashindano ya kimataifa, inatakiwa viongozi wa klabu hizo kuhakikisha zinatilia mkazo uandaaji wa vikosi imara vya timu za vijana.

"Tunajua kuwa, bado tunahitaji kufanya vema kwa timu zetu zinazowakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa, lakini jambo la muhimu ni kuimarisha kwanza timu zetu," alisema Tenga.

Alisema kama klabu zitafanya vema katika mashindano mablimbali ya kimataifa, hata timu ya taifa itafanya vema kwa kuwa inawatumia wachezaji hao hao ambao wanahitaji kuimarishwa.

Akizungumzia ushiriki wa timu hizo katika michezo yake ya kimataifa iliyopita, Tenga alisema amefurahi kuona viongozi wa timu hizo wamekubali kushindwa.

Alisema alifurahishwa na kauli za viongozi hao wakisema wamezidiwa kiwango na timu nyingine jambo ambalo ni la kiufundi badala ya kulalamika kuwa, wanaonewa wakati kiwango chao kinaonekana.
 
hata iweje soka la bongo litabakia hivyo hivyo, hata kuwe na timu ya watoto wachanga mwisho wake yatakuwa ni yale yale tu, kwa sababu sio tu kuwa wachezaji ni wabovu, bali hata uongozi wenyewe wa soka ni uharo mtupu....
 
...Vilabu vikongwe hivyo, lakini ndio hivyo tena migogoro kila kukicha, kila uongozi unaoingia madarakani either unamaliza muda wake kwa kashfa na tuhuma kibao, au unapinduliwa,.

Nachelea vilabu hivi vikongwe kuja kutwa na yalovisibu vilabu vingine vikongwe vya enzi hizo mfano Gor Mahia, AFC leopards-Kenya, 'moto' Small Simba, 'Kisk' Kikwajuni au 'Kuala' Miembeni za Unguja!...

Simba na Yanga wabadilike mfumo wao wa kujiendesha badala ya kutegemea pesa za milangoni na wafadhili! si mnawakumbuka wafadhali wa enzi hizo kina Jabbir Shikamkono, mzee Kiluvia, Shafi Bora, Naushad Mohd, yani mfadhili akijitoa/akisusa na basi gogoro jipya linaibuka,

aaarrrgghh...
 
Mpira Wetu Utakuwa Hivyo Hivyo Milele Maana Wa Tz Tumejawa Na Football Fitna Tuu Ajili Ya Simba Na Yanga Kushinda Mechi Zao..na Kujinufaisha Wenyewe..........si Kukuza Soka
hasahasa utopwinyo Sasa hivi Bado wanendeleaje kugawa utamu tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom