Simba Yamtimua kocha mkuu, Dylan Kerr na kocha wake wa makipa Iddi Salim

Deo Corleone

JF-Expert Member
Jun 29, 2011
16,975
13,146
Kama kawaida ya mambumbumbu
Coach katolewa kafara,Coach ametuaga huko Twitter.

=====================

Kwa masikitiko makubwa klabu ya Simba inawaarifu umma kupitia vyombo vya habari.uamuzi wake wa kuvunja mikataba yake na makocha wake - kocha mkuu Dylan Kerr kutoka uingereza na kocha wake wa makipa Iddi Salim.

Katika uamuzi wake uliofanywa mchana huu na kikao cha kamati ya utendaji, ambapo makocha hao waliitwa, klabu ya Simba na walimu hao kwa pamoja wamekubaliana kuvunja mikataba ya ajira zao kwa faida ya pande zote mbili.

Kwa sasa kocha msaidizi wa Simba Jackson Mayanja atakuwa na timu.huku mchakato wa kumpata kocha mkuu ukiendelea.
Mwisho uongozi unawashukuru walimu hao kwa huduma waliyoitoa katika kipindi chote cha uwepo wao klabuni.

Imetolewa na Haji S.Manara
Mkuu wa mawasiliano wa klabu ya Simba.
Simba nguvu moja
 
Last edited by a moderator:
Simba yetu jamani...inaelekea wapi,...

tatizo la simba wala sio kocha, hawa miunguwatu..wanaojiita viongozi wa simba ndo wanaharibu club....

Kiukwel itatuchukua muda sana kupiga hatua na kuwa club ya kimataifa kama uendeshaji wenyewe ndo wa hovyo kiasi hichi.
 
Last edited:
HUU NI UPUMBAVU WA HALI YA JUU, wa kufukuzwa ni Aveva na wale machotara wake! Wananiboa sana hawa jamaa, yaani, aaaarrrggghhh, sijui NIIFANYAJE HII MIJITU! Yenyewe ndo mibovu, hata huyo Jackson Mayanja awe chonjo tu! Toka huu uongozi uingie madarakani, HAMNA walichofanya na hakuna dalili!
Nafikiri sasa bora wanachama kuingia msituni, liwalo na liwe tu!
 
Kocha alilalamika sana aina ya wachezaji alio letewa
hasa kiongera...

badala ya kumruhusu kocha asaini wachezaji anao wataka...
mnamchagulia wachezaji bomu na kumlaumu...mambo kienyeji kabisa

Wameamua Kumrudisha Mganda Mosea Basena Awe Kocha Mkuu Akiasaidiwa Na Mganda Mwenzie Jackson Mayanja Na Kuna Uwezekano Pia Yule Kocha Wa Viungo Nae Ni Mganda Richard Amatre Nae Akajumuishwa Kikosini. Kuna UZI Wa Amavubi Nimeandika MATATIZO MAKUU Ya Simba Sports Club Hebu Utafute Mkuu Uusome Kwani NIMETEMA NYONGO Yangu. Sina Wasiwasi Na Basena Pamoja Na Mayanja Hasa Kutokana Na Uwezo Wao Mkubwa Na Vile Vile Sina Tatizo Na Kocha Mkuu Dylan Kerr ALIYETIMULIWA Kwani Amekibadili Mno Kikosi ILA Tatizo La Simba 97% Lipo Kwa UONGOZI MZIMA Ila WAMEAMUA KUTAFUTA KICHAKA CHA KUFICHA MAOVU YAO KWA KUMSUKUMIZIA MAKOSA YOTE KOCHA Kerr.
 
Kama kawaida ya mambumbumbu
Coach katolewa kafara,Coach ametuaga huko Twitter.
Tatizo la Simba wala si kocha, huenda hata sio viongozi peke yao. Ni shinikizo la pamoja la wanachama na wachezaji kutaka mafanikio ya papo hapo ilhali timu ilikuwa ndio kwanza inaimatishwa. Kibadeni alipowataka viongozi na wanachama wampe mwaka mmoja ajenge timu kutokana na ninachoweza kukiita kizazi cha dhahabu (golden generation) cha wachezaji wa wakati ule, wala wakamwona adui; wakamtimua. Amebaki Ndemla na Mkude pekee, ambao kila msimu wanachanganywa na wachezaji wapya. Huo mshikamano (combination) utapatikana lini? Kuanzia hapo, kila uongozi humpa kocha masharti magumu ya mafanikio ilhali wachezaji si wa viwango. Kwa kuwa wanaotafutwa ni walimu wa gharama nafuu, hubahatisha kukubali masharti hayo ili kuhanga njaa, na wanapofukizwa huwa hawajutii sana isingekuwa kwa kuharibiwa CV zao; wabakiwa wanayajua mapema.
Ushauri wangu ni kubaki na Simba hii, kisha kumpa malengo ya angalau misimu miwili Mwalimu Mayanja, pamoja na uhuru wa kusajili anavyoona yeye. Hivyo ndivyo Mtibwa wanavyofanikiwa licha ya kuwa na makocha wala wachezaji wa kigeni. Ila Simba wajue tu kwamba tofauti na makocha wote waliowatimua, huyu Mayanja uwezo wake umepimwa hapahapa Bongo na unakibalika pamoja na kueleweka. Timu ikifanya vibaya chini yake utakuwa ni ushahidi usiowacha shaka kwamba tatizo sio kocha.
 
tatizo sio kocha hata sababu zao zinachekesha wachezaji wanaosajiliwa sasa hawana hadhi ya kuchezea simba wengi viwango vyao ni vya chini kwa kifupi kamati ya usajili ya simba imeshindwa kazi yake pamoja na mapungufu tuliyonayo bado walishindwa kurekebisha mapungufu hayo kwenye dirisha dogo wamekalia siasa viongozi inabidi muwajibike badala ya kutoa watu wengine kafara isitoshe kocha alisema kipindi hiki cha kombe la mapinduzi anatumia kuangalia kiwango cha wachezaji hasa wanamtimua wa nini wakati viwango vyenyewe ndio hivyo
 
...they are hired to be fired!?!ila hizi timu zetu nadhani ni zaidi ya hiyo kauli...
 
HUU NI UPUMBAVU WA HALI YA JUU, wa kufukuzwa ni Aveva na wale machotara wake! Wananiboa sana hawa jamaa, yaani, aaaarrrggghhh, sijui NIIFANYAJE HII MIJITU! Yenyewe ndo mibovu, hata huyo Jackson Mayanja awe chonjo tu! Toka huu uongozi uingie madarakani, HAMNA walichofanya na hakuna dalili!
Nafikiri sasa bora wanachama kuingia msituni, liwalo na liwe tu!
Kweli mkuu bora tuingie mstuni tu....hakuna jinsi.....kila siku wanasimba tumekuwa watu wa kulia tu....
 
...they are hired to be fired!?!ila hizi timu zetu nadhani ni zaidi ya hiyo kauli...
Duuuuuuih! Bongo noooma aiiiseeee, sijui yule TUTUSA Van Gaal angekuwa anafundisha timu mojawapo kati ya simba na yanga saivi angalikuwa wapi??!!
Safari njema Dylan Kerr, msalimie classmate wako Jose Mourinho
 
Back
Top Bottom