Simba wavamia zizi na kuua ng'ombe walionona pekee na kuacha ng'ombe wazee na wagonjwa!

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,606
1,956
NOVEMBA 18, 2019

Kundi Simba kutoka Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (SENAPA) mkoani Mara, wamevamia zizi la mkazi wa Kijiji cha Robanda, Samwel Mahewa na kuua ng’ombe 20, huku wengine 8 wakipotea.

Ng’ombe wote wameelezwa kuwa na thamani ya Sh milioni 15.4.

Tukio la kuuawa ng’ombe hao, lilitokea Novemba 3, mwaka huu saa 7.00 usiku katika Kitongo cha Momorogoro kila ng’ombe mmoja akithaminishwa kwa thamani ya Sh 550,000.

Akizungumza na MTANZANIA mwishoni mwa wiki, Mahewa alisema simba walivamia zizi lake na kuua ng’ombe 17 hapo hapo na kujeruhi wengine watatu ambao walikufa baadaye.

Alisema ng’ombe 8 walikimbia kutoka ndani ya zizi mpaka sasa hawajafamika waliko, licha ya juhudi kubwa za kuwatafuta bila mafanikio.

Alisema ndani ya zizi kulikuwa na ng’ombe ambao baadhi ni wazee na wengine walikuwa hawaoni, lakini jambo la ajabu simba hawakuwaua, bali walikuwa wanaua na kula wale walionona.

“ Nimepata hasara kubwa,ng’ombe hawa nilikuwa nawategemea katika kilimo,sijui nitaanzaje maisha haya,”alisema.

Ofisa Maliasiili Wanyamapori Wilaya ya Serengeti, John ole Lendoyani alithibitisha kuuawa ng’ombe hao na kumtaka Mahewa kujaza fomu ya kifuta machozi.

Alisema mchakato ukikamilika atalipwa kifuta machozi cha Sh 50,000 kwa kila ng’ombe na kutoa wito kuimarishwa ulinzi na kujenga mazizi imara.

*Mtanzania*
 
Ila viwango vya serikali ni upuuzi mtupu! Wewe ukimuua Simba unatakiwa kulipa millions ila Simba wakiua mifugo yako wanatakiwa kukulipa kifuta jasho cha Wekundu watano.....!

Next time wauweni hao Simba then mtawalipa hao Sijui SERENGETI kifuta jasho cha 100,000/ kwa kila Simba mtakayekua mmemuuwa!!
 
Ukimuua simba tena bahati mbaya unalipishwa milioni 30 la sivyo jela
Simba akiua mnyama wako eti unapewa kileta machozi zaidi elfu 50!
This is Tanzania!
 
Bado nawashangaa wakina Kevin Richardson wakicheza na simba na kujifanya marafiki zao, sijawahi wala sitakuja kumuamini mnyama wa porini hata siku moja.
 
50,000 ni sawa na Heinekein 10. Hiyo bei sio fair kabisa.

Waziri husika inabidi aingilie kati, maana Simba wangeuawa hao ingekuwa kesa ya uhujumu...
 
Back
Top Bottom