Simba wanapaswa kufungua masikio yao pindi wanapoambiwa udhaifu wao kama waambiwavyo kuhusu ubora wao

pakacha77

Member
Aug 12, 2022
91
98
Ukweli japo ni mchungu lakini ni tiba tosha ya maradhi ndugu zetu wa upande wa pili yaani Simba SC kuna kitu kinachowatafuna ambacho mpaka sasa hawakijui wanakimbilia kuwatuhumu makocha, wachezaji na hata viongozi wao ingawa kuna uwezekano wa hao niliowataja wakawa sababu lakini sababu kuu ni Kibri Kwanini nasema hivyo ? Nasema hivyo kwa sababu hawa jamaa wanaamini wao wana timu bora kuliko nyingine na wanaamini kuwa wao wana hati miliki ya kushinda kila Mechi sababu watakayokwambia kuwa wao ni timu kubwa wapo nafasi ya 11 Afrika na watashiriki Super Cup,na kwa sababu hii huwafanya kupenda kusikia wachambuzi wanaosifia ubora wao kuliko udhaifu wa timu yao pia hupenda kusikia udhaifu wa Yanga kuliko ubora wa Yanga na ndio maana wao wakishinda wachezaji wao wana uwezo Yanga wakishinda wamenunua mechi hasa Yanga inapocheza na timu ndogo na inapocheza dhidi yao ,Azam au timu yoyote kubwa na Yanga kupata ushindi utasikia Yanga wameloga hawa jamaa hawaamini kabisa kuwa Yanga wanaweza kushinda mechi kwa ubora wa kikosi Chao na benchi Bora la ufundi lililopo hawa jamaa ukiwaambia Yanga ndio timu Bora kwa sasa Tanzania watakwambia mbona mlitolewa michuano ya klabu bingwa Afrika na kudondokea Shirikisho wanashindwa kutambua hata timu ulimwenguni huweza kupata matokeo kama waliyopata Yanga. Ndugu zetu baada ya Rais Samia Suluhu kuahidi motisha ya fedha kiasi cha shilingi milioni 5 kwa goli wao ndio walioamini ndio wangeweza kunufaika na motisha hiyo na si Yanga ukiwauliza wao ni timu kubwa na wana rekodi nzuri kuliko Yanga ktk michuano hiyo ni kweli wao ndio wana uwezo wa kutumia uwanja WA nyumbani na si Yanga na wakaingia na kigezo eti kwa kuwa hakuna timu kutoka Tz iliyowahi kuifunga Mazembe basi hata Yanga wangeshindwa kufanya hivyo at the end of the day anajua nini kilichotokea wao waliojiaminisha na ubora wao kutokana na Kibri chao wamekula Chuma tatu na Yanga waliochukuliwa poa wamempa mtu Chuma tatu na Kwa matokeo haya Kwa sababu hawakutegemea mashabiki wao huishia kutoa shinikizo kwa uongozi wa timu yao kwa kuwatuhumu baadhi ya wachezaji au kocha nini madhara ya shinikizo ni kwamba uongozi utalazimika kufanya maamuzi magumu ya kufukuza kocha na wakumbuke akija kocha mpya atakuja kufanya implementation ya falsafa yake so it is long process kwa wachezaji kuendana nae na timu itaendelea kuzorota yote haya Kwa sababu ya Kibri ukiwakuta mashabiki wa hii timu wanapohojiwa mara baada ya timu yao kupata matokeo hasi utasikia haiwezekani Simba ni timu kubwa kocha hafai au mchezaji fulani hafai kuchezea Simba ni kibri Tu Yaani hawa watu wana kuliko hata hao wakina Mamelodi na Al Ahly wengine walidiriki kusema eti Raja ni timu ndogo Tu hawawezi kuwafunga kigezo wao watashiriki Super Cup na Raja hawatashiriki sababu eti walishawahi kumfunga Al Ahly ambae alikuwa bingwa kipindi kile sembuse hao Raja walishindwa kutambua ubora wa Raja hata pale walipoweza kuwatandika Vipers tano bado kwao ilikuwa sio ishara mbaya wakasema Vipers ni timu ndogo ttu tutawalipia kisasi .Amkeni nyinyi madunduka team performance is dynamic process and not static msijivunie Sana na nafasi ya ubora wa timu yenu mkumbuke hata Yanga kipindi cha akina Kamussoko, Ngoma,Tambwe nk chini ya Manji ilishawahi kushika nafasi ya ubora ngazi ya klabu Afrika juu ya Simba ingawa Yanga hawakuweza kufikia nafasi ya 11 waliyonayo Simba msivimbe Sana kujiona wakubwa kupitiliza hayo Tu ni maoni yangu mkiyafanyia mtanishikuru
 
Back
Top Bottom