Simba, Utouh wasota nje ukumbi kwa kukosa vitambulisho | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Simba, Utouh wasota nje ukumbi kwa kukosa vitambulisho

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, May 11, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  May 11, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  BAADHI ya viongozi wanaoshiriki semina elekezi mjini hapa jana wameshindwa kuingia ndani ya ukumbi na kusababisha Rais Jakaya Kikwete aingie kabla ya wao na viongozi hao kuendelea kusota nje ya ukumbi huo.

  Kitendo hicho kilitokana na maofisa wa usalama kuwazuia kwa muda nje ya ukumbi baadhi ya viongozi na kuwalazimisha kurudi mjini kwa ajili ya kufuata vitambulisho vya kuingilia.Ukumbi wa St Gasper uko umbali wa zaidi ya kilomita sita kutoka katikati ya Mji wa Dodoma ambako semina elekezi kwa viongozi wa serikali na wakuu wa idara mbalimbali, ilifanyika.

  Katika ukumbi huo kila mshiriki alitakiwa kuvaa kitambulisho maalumu wakati wote, lakini baadhi ya viongozi wakiwamo mawaziri walikaidi agizo hilo jana na kukumbwa na aibu hiyo.Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Watoto, Sophia Simba alikuwa mtu wa kwanza kuzuiwa kuingia ndani ya ukumbi licha ya kuwabembeleza, lakini maofisa hao waligoma.

  Simba alikaa nje kwa zaidi ya dakika 30 kabla ya kuwasiliana na wasaidizi wake ambao walimletea kitambulisho na kuruhusiwa kuingia ndani ya ukumbi huku akiwa amechelewa.

  Mtu mwingine ambaye alipata wakati mgumu alikuwa ni Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh ambaye alizuiwa kuingia ndani ya ukumbi kwa muda muafaka licha ya kueleza kuwa hakuwa ameandaliwa kitambulisho.


  Wakati huohuo,semina hiyo ilianza jana kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa Msuya kutoa mada na alikuwa akielekeza njia bora ya kuwa na ushirikiano mzuri kati ya viongozi wa kisiasa na watendaji.

  Kwa mujibu wa mpangalio katika semina hiyo Msuya alitakiwa kuwasilisha mada yake juzi, lakini ilishindikana baada ya mada ya uchumi iliyokuwa chini ya watu wa Benki ya Dunia kuchukua muda mrefu zaidi na kusababisha mada nyingine zichelewe kuanza.

  Msuya huenda akamaliza malumbano kati ya viongozi wa serikali na watendaji ambao wamekuwa wakigongana mara nyingi kutokana na wengi wao kutojua mipaka zao.Kiongozi mwingine mstaafu ambaye yupo katika orodha ya watoa mada ni spika mstaafu waBunge la Muungano, Mstaafu Pius Msekwa ambaye naye amepewa nafasi ya kuzungumzia masuala ya uongozi.

  Msekwa pia atazungumzia suala la Muungano ambalo pia linatarajia kujadiliwa kwa kirefu pamoja na namna bora ya kuboresha Muungano huku baadhi ya wajumbe wakitabiri kuwa ajenda hiyo huenda itatolewa kesho au kesho kutwa kwa kuwa Muungano ni suala ambalo liko chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais ambaye tangu juzi yupo safari nje ya nchi.
   
 2. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #2
  May 11, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  Endelea kutupasha؛‎ hivi hakuna mada juu ya hizi kero na namna ya kuziondoa: makazi duni hasa kwa wakazi wa mijini, masoko hafifu ya mazao ya kilimo, watanzania wengi kupata elimu duni, mishahara duni ya wafanyakazi, huduma duni kutoka kwa sekta za uma kama polisi, uhamiaji, hospitali, TRA, bandari eapot etc.
   
Loading...