Shadida Salum
Journalist at JamiiForums
- Sep 11, 2020
- 69
- 104
Michezo miwili ya nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi imepigwa leo hii katika Dimba la Amani visiwani Zanzibar. Mchezo wa awali uliwakutanisha miamba wa michuano hiyo Azam FC dhidi ya Yanga.
Mchezo huo umemalizika kwa Yanga kufanikiwa kufuzu fainali baada ya dakika tisini za mchezo kumalizika kwa sare ya 1-1 na kulazimika kwenda kwenye hatua ya mikwaju ya penati ambapo Yanga SC wameshinda kwa mikwaju 5-4.
Kwingineko Simba imetinga fainali za mashindano hayo baada ya kuitandika Namungo bao 2-1 .
Fainali ya mashindano hayo itawakutanisha watani wa jadi Simba SC na Yanga CS siku ya tarehe 13 Januari 2021 katika Dimba la Amani Visiwani Zanzibar.
Mara ya mwisho Simba na Yanga kukutana katika fainali za kombe la Mapinduzi ni 2017 ambapo Simba alishinda kwa mikwaju ya penati.