Sarah Simbaulanga: Mwanamke wa kwanza kuiba pesa ndefu katika historia ya benki zote nchini

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Hivi huyu mwanamama alimaliza kifungo chake? Mnakumbuka kosa lake na jinsi ambavyo kesi yake ilikuwa ni kama simulizi la kutosadikika.

Hivi akisikia yanayofanyika hivi sasa huko aliko si anaona aliwahi kidogo tu..

-------------------

The case of Sarah Simbaulanga, a National Bank of Commerce (NBC) employee who stole Shs 31.0 million in foreign exchange (mostly travellers cheques) astonished Tanzanians because of the sum of money involved in the theft, the apparent ease with which it was carried out and, the biggest surprise of all, the immediate admission of guilt after the lady had been arrested. The accused looked very calm in the dock. "Yes" she said "it is true" to the five counts she was facing. The Principal Resident Magistrate asked her twice if she really understood the charges against her. She confirmed her plea of guilty.

The evidence presented to a packed court in Dar es Salaam was, in abbreviated form, as follows:
Between October 19th and 29th 1987 Simbaulanga and an accomplice named Toroha (whose extradition from Kenya is being demanded by the Tanzanian authorities) stole from the NBC 1,100 travellers cheques worth US$ 390,000 and 200 travellers cheques worth £20,000.

Simbaulanga and Toroha had been friends since the early seventies when she had been at Kisutu Secondary school in Dar es Salaam. She and Toroha hired two rooms at the Skyway Hotel on the night of October 29-30. Simbaulanga had managed to obtain four passports for herself and her three children. They travelled on an Air Tanzania plane to Nairobi on October 31st.

They then used some of the travellers cheques to buy five KLM tickets to London. On November 1st and 2nd they made twelve different transactions using $246,000, The Police are still trying to trace the remaining travellers cheques.

The accused then bought five tickets to Nairobi on November 5th, and in Nairobi they carried out further transactions with new travellers cheques they had bought in London. Toroha bought four mini-buses and a pick-up and registered them under the name of his wife Elizabeth. Later three other suspected accomplices were arrested Simbaulanga's NEC Controller, a KLM Sales Manager and a businessman. On February 10th Simbaulanga was sentenced to 35 years imprisonment, seven years on each count, to run concurrently. But, on February 16th, the Prosecution appealed the case and asked the High Court to issue an order for the sentence to run consecutively.

Subsequently, Simbaulanga was sentenced to 28 years in prison. The case was one of many referred to later by SHIHATA under the heading ‘Tanzania's thriving theft industry' in which it quoted a whole spate of thefts by servants of the NBC from branches all over the country. It estimated the total loss at over Shs 60.0 million.

Source: Tanzanian Affairs » Issue 30

Saa 7 kamili mchana, siku ya jumapili ya tarehe 1.11.1987, Watanzania, kila pembe ya nchi, walipigwa butwaa na kushikwa na bumbuwazi kubwa baada ya Radio Tanzania Dar Es Salaam kutangaza, katika taarifa ya habari, kwamba mwanamke aitwae SARAH MARTIN SIMBAULANGA (35) mfanyakazi wa NBC alikuwa amekwapua mamilioni ya fedha na alitoroka nchini akiwa na watoto wake watatu na laaziz wake, Mfanyabiashara TOROHA MOHAMED TOROHA(40).

Tukio hilo la kipekee na la aina yake liliwaacha midomo wazi wananchi hasa kwavile enzi hizo halikuwa jambo la kawaida kwa mwanamke kuwa "mpigaji" wa kiwango cha kutisha cha fedha!.

Tukio hilo liliongelewa mno sehemu mbalimbali hasa maofisini, majumbani, mashuleni, makambini, masokoni, mahotelini, vilabuni nk huku wengi wakimlaani vikali mwanamke huyo na kusikitika nchi kuibiwa fedha hizo. Kwa wengi, ilikuwa ni simanzi kubwa sana na haikushangaza basi pale Mkutano Mkuu wa Baraza la Kuu la Vijana uliokuwa ukifanyika Singida kutoa wito kuwa uongozi wote wa juu wa NBC "Ufyekelewe mbali"!.

Ofisi ya DCI, mara moja, ilituma taarifa (Interpol) nchi mbalimbali ili zisaidie kuwakamata "mabandido" hao.

Hatimaye, majira ya saa 9 alasiri, siku ya Ijumaa, tarehe 13.11.1987, Bw. TOROHA akabambwa kwenye ofisi ya magari ya Toyota jijini Nairobi, Kenya akiwa kwenye mishemishe ya ununuzi wa magari.

"Mandata" walipombana aeleze kuhusu aliko Bi. SARAH, Bw. TOROHA hakuwa na namna zaidi ya kuwapeleka chumba na. 322 cha hotel maarufu ya Jacaranda. "Mandata" hao, wakiwa na TOROHA, waliingia chumba hicho kininja na kumkamata Bi. SARAH kiulaiiini!.

Jijini Dar Es Salaam, NBC ilimfukuza kazi Bi. SARAH kwa kutoonekana kazini kwa siku 5 mfululizi. Aidha, kamatakamata ilianza ambapo wafuatao walikamatwa na kuhusishwa na wizi huo: Bw. ROMANIUS PETER NDANZI(43), Mdhibiti wa Fedha za Kigeni, NBC "Foreign Branch", Bw. ERNEST JOHN MWENEWANDA(40), Meneja mauzo KLM, HAROON DAUD(35), Mfanyabiashara. Washtakiwa hawa, tarehe 19.11.1987, walifikishwa Kisutu kwa "Pilato" Mh. JUMA MUSTAPHA JIBREA. Waliomba dhamana wakanyimwa. Wakakata rufaa Mahakama Kuu. Tarehe 5.1.1987, Jaji LUHEKELO KYANDO, aliwanyima dhamana na kueleza, kwa uchungu na uzalendo, kwamba:
*"Kiini cha kesi hii ni moja ya matukio ambayo yameshtua sana umma kuona kwamba mamilioni ya fedha yanaibwa. Ni maoni yangu kuwa itakuwa kinyume na hisia za jamii ikiwa mahakama itachukua msimamo tofauti na usiokuwa na mwelekeo wa hisia sahihi kuhusu vitendo hivi"*.

Msimamo huu uliakisi kilichoelezwa na aliyekuwa Waziri wa sheria, Mama JULLIE MANNING, tarehe 17.1.1976, kwamba: *"Ingawa Mahakama hazipendelei upande wowote, hiyo haina maana kwamba zisijali nini kinatokea nchini"*.

Serikali ilituma Kenya Hati ya kuomba SARAH na TOROHA warudishwe nchini(Extradition) kwani nchi hizi zina makubaliano hayo ya aina hiyo. Hati hiyo iliwasilishwa na SP PETER MWANGI mahakamani saa 2.30 asubuhi ijumaa, tarehe 15.1.1988 mbele ya Hakimu Mwandamizi, Mh JOSEPH MANGO na kisha maombi hayo yakaanza kusikilizwa.

Tarehe 29.11.1987, mahakama hiyo ikatoa uamuzi kuwa, kwa kuzingatia ushahidi uliotolewa, SARAH arudishwe Tanzania kujibu mashtaka lakini ikamuachia huru TOROHA. Baada tu ya kuachiwa, mbio alizotimua TOROHA, hata USAIN BOLT angesubiri!.

Siku ya jumanne, saa 6 mchana, tarehe 2.2.1988, SARAH alikabidhiwa kwa maafisa wa Tanzania mpakani Namanga na kukimbizwa "wanguwangu" na magari 5 ya polisi hadi Dar Es Salaam.

SARAH alifikishwa mahakama ya Kisutu saa tatu asubuhi, siku ya Jumatano, tarehe 10.2.1988 chini ya ulinzi mkali. Mahakama hiyo ilikuwa imefurika mno huku barabara ya Bibi Titi ikifungwa kwa muda kwani wananchi wengi walitoroka makazini kwenda kumuona SARAH anafananaje na kusikia aliwezaje kuiba kitita chote hicho!.

Mbele ya Hakimu Mwandamizi Mh. JOSEPH MASANCHE, Bi. SARAH alisomewa mashtaka 5 na SSP EDWIN ABRAHAM MAN. Bi. SARAH alikuwa akitetewa na Dr. MASUMBUKO ROMAN LAMWAI, mmoja wa mawakili bora kabisa kuwahi kutokea nchini.

Bi. SARAH aliushangaza umati uliofurika, pale bila kupepesa macho, kutingisha pua wala kutikisa maskio, alipokiri mashtaka yote 5! Hakimu MASANCHE nae pia alipigwa butwaa na ikabidi amuulize kama ameelewa vizuri mashtaka ambapo "alikomaa" na kusema anaelewa na anakiri ni kweli alienda makosa hayo!.

Mh MASANCHE, baada ya kusikiliza pande zote 2 kuhusu adhabu, akasoma hukumu iliyochukua robo saa tu ambapo alimuhukumu SARAH kwenda jela miaka 7 kwa kila kosa na makosa yote kwenda pamoja hivyo angetumikia miaka 7 tu na pia akamuamuru arudishe fedha hizo mara moja. Mh MASANCHE alin'gaka- *"Hakuna kitu kibaya kama wizi wa fedha za kigeni ambazo Taifa linazihitaji sana"*.

Upande wa mashtaka hakuridhika na adhabu hiyo "kiduchu" hivyo ukakata rufaa Mahakama Kuu kuomba adhabu hiyo iwe kwa kufuatana na sio kwa pamoja. Aliyekuwa Jaji Kiongozi, Mh. NASSOR MZAVAS ndiye aliyesikiliza rufaa hiyo huku jamhuri ikiwakilishwa na Bw. KULWA SATO MASSABA na Dr. LAMWAI akimuwakilisha SARAH.

Saa 4 asubuhi, Ijumaa ya tarehe 19.2.1988, Mh MZAVAS alitoa hukumu. Baada ya kuisoma hukumu hiyo kwa dakika 45, huku umati ukisubiri kwa hamu, Mh. MZAVAS "aliinama na kujifanya kama anajikuna" kisha "akampiga SARAH mvua 28"! SARAH hakuamini macho yake na kubaki amebun'gaa! Mh. MZAVAS akamalizia- *"Hii ni hasara ya kiuchumi ambayo inaiathiri nchi. Fedha hizo kidogo za kigeni nchi ilizofaulu kujiwekea akiba kwa kujikidhi sana, ndio inalolifanya kosa la kuiba fedha za kigeni kutisha. Wizi huu ulipotangazwa na RTD, Mahakama pia ilisononeka na kufadhaika sana kwa kuibwa kwa fedha hizo za kigeni kwani Mahakama nayo ni sehemu ya jamii"*.

"Upigaji" huu wa ulikuwa umepangwa na wapenzi hao wawili, SARAH na TOROHA. TOROHA alikuwa ni kijana mtanashati aliyezaliwa Mbegani, Bwagamoyo mwaka 1948. Baba yake aliwahi kufanya kazi Ikulu na kisha akawa Afisa wa ubalozi Japan na Uholanzi miaka ya mwanzoni ya Uhuru na alikuwa na uwezo wa kifedha. Mwaka 1967, baada ya kuzinguliwa na siasa ya Ujamaa ambapo nyumba yake ilitaifishwa, aliacha kazi na kutimkia Ujerumani na kufanya biashara ya mkahawa na duka la vinyago.

Mwaka 1979, Bw. TOROHA, akiwa kijana wa miaka 31, alimuoa Mkenya, Bi. ELIZABETH WANJIRU na wakaishi Ujerumani, Uingereza, Ufaransa, Italia na Kenya.

TOROHA alikuwa akija nchini mara mojamoja hivyo akaanza urafiki na Bi. SARAH aliyekuwa binti mdogo mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Zanaki jijini. SARAH, baadaye, aliajiriwa NBC na kupanda vyeo hadi kuwa Msimamizi, Idara ya Fedha za Kigeni.

TOROHA aliingia nchini tarehe 11.10.1987 na kufanya "mchongo wa upigaji" na "Mpango wa kando" wake, Bi. SARAH. Ili kufanikisha dili la upigaji na kusepa nje ya nchi bila kushtukiwa, Bi. SARAH alishirikiana na maafisa wasio waaminifu wa "Immigration" na kubadili majina yake na ya wanawe na kupata "passports" mpya tarehe 28.10.1987. "Passport" ya SARAH yenye Na. 220130 ikawa na jina KHADIJA ALI MKIMBAU. "Passports" za wanawe zikawa na majina mapya 1.HAPPINESS SIMBAULANGA-(JAMILA ISMAEL HASSAN), 2. SIMBA SIMBAULANGA- (HALFAN ISMAIL HASSAN), 3. BLANDINA SIMBAULANGA-(JENIPHER ISMAEL HASSAN).

Kisha, SARAH "akapiga" hundi za kusafiria 1,100 zenye thamani ya $ 390.000 na hundi 200 zenye thamani ya £ 20.000. Fedha hizo 'alizipiga' mara 3 kati ya tarehe 19.10.1987 na 29.10.1987. Kwa wakati huo, hizo zilikuwa ni fedha nyingi sana. Baada ya mchongo kukamilika, SARAH na TOROHA walichukua vyumba 2 katika hotel maarufu sana ya Skyway iliyokuwa makutano ya Ohio na Samora. Chumba kimoja kilikuwa chao na kingine cha watoto wa SARAH ambako walilala kwa usiku mmoja wa Ijumaa, tarehe 30.10.1987. Usiku wa Ijumaa hiyo, SARAH na TOROHA walienda ukumbi wa White House "kushangilia ushindi" ambako bendi ya Marquis du Zaire chini ya Babu Seya iliwapagawisha vilivyo!.

Tarehe 31.10.1987, TOROHA, kin'gast chake SARAH na watoto wake 3 walikwea pipa la ATC kwenda Kenya. Walipotua tu Jomo Kenyata International Airport, wakatumia hundi zenye thamani ya $ 2700 kununua tiketi 5 za KLM na wakaenda Amsterdam na kisha London. Wakiwa London UK, waliofanya "transactions" nyingi "Baclays bank" na tarehe 2.11.1988 wakanunua tiketi 5 za KLM ili waondoke kuelekea Kenya tarehe 5.11.1987. Tarehe 3 na 4 ilikuwa ni "kujirusha" tu nchi ya Malkia ie *Kazi na Bata*!.

Tarehe 5.11.1987 walikwea KLM na kufika Kenya tarehe 6.11.1987. Nchini Kenya walifanya matanuzi na manunuzi ambapo TOROHA alitumia $ 260,000 kununua magari (mini-bus 4 na pick up 1) na yote akayasajiri kwa jina la SARAH. TOROHA, alipokuwa akitaka kununua magari mengine ndipo aliponyakwa na mamwela katika ofisi za Toyota tarehe 13.11.1987! .

Huu ndio mkasa wa Bi. *SARAH MARTIN SIMBAULANGA* @khadija ALLY MKIMBAU uliokuwa wa aina yake na wa kipekee!

IMG-20190105-WA0001.jpeg

IMG-20200227-WA0000.jpg

BAADHI YA MICHANGO ILIYOTOLEWA NA WADAU
Mwanakijiji (nimeamua kuita jina kamili)...

Huyu mama alinisikitisha sana kwani alikua na watoto wake wawili walikua wadogo sana wakisoma primamry moja wilaya ya kinondoni na walikua very cool, wapole na wana nidhamu ya hali ya juu... nina imani walipata shida sana kwani enzi zile haya mambo yalikua very rare... siku hizi ukiwa mtoto wa fisadi ni pride, JAMII IMEOZA

Nakumbuka hata jinsi kesi yake ilivyokua movie kwenye gazeti la mfanyakazi (kama sikosei), maana tulikua tunaamshwa tukanunue gazeti ili baba asome hii kesi ndio tuwahi shule... enzi zile hata gazeti tulikua tunapata kwa foleni

Pia kesi yake inakumbusha jinsi kesi zilivyokua zinaweza kuendeshwa kwa haraka, siku hizi kesi zote za wizi watu hawafungwi, kesi inaenda four eyars inakauka tu

cest la vie

 
Hivi huyu mwanamama alimaliza kifungo chake? Mnakumbuka kosa lake na jinsi ambavyo kesi yake ilikuwa ni kama simulizi la kutosadikika.. Hivi akisikia yanayofanyika hivi sasa huko aliko si anaona aliwahi kidogo tu..

Namkumbuka huyu mama, alikuwa mwajiriwa wa bank ya NBC miaka hiyo kabla wahuni hawajaitoa zawadi kwa makaburu. milioni 60 zilim.
 
Those were good old days, nakumbuka I was young then, lakini huyu mama nilimuona kama Jambazi wa hali ya juu. Lakini sasa wizi umekuwa sifa ukipata kazi nzuri after two years bila kujenga nyumba ya kifahari Jamii inakuona umezubaa. Its sad very sad.

The question is how did we get here? And can we ever go back to the good old days?
 
Nani anajua huyu mama yuko wapi sasa? nakumbuka tulishangaa sana miaka ile mwanamke kuiba pesa kama ile!!!

Sio mwanamke tu, kipindi kile kuiba pesa ilikuwa ni jambo la aibu, yaani watu walikuwa wanakushangaa na sio wanakuadmire sahizi mtu ukiiba watu wanakusifia (hawajui kwamba hizo ni pesa zao wenye),

Kweli akili zetu zipo kwenye reverse gear for some time now, tunazidi kuwa mazuzu as days goes on (mind evolution yetu ina-move from brightness to foolishness).
 
Ninachokumbuka ni kuwa huyu Mama alikuwapua dola za marekani nyingi sana akataka kutoroka nazo nje ya nchi ila kabla hajafanikiwa dili likafumuka wakawa wanafukuzwa mpaka walipo kamatwa na hela mkononi. Nakumbuka kuna wakati yaliwahi toka mashati ya ujiuji (Kitambaa kama cha magauni ya CHARANGA kwa wanaoyakumbuka) yenye picha za dola za marekani tukawa tunayaita SIMBAULANGA.

Kweli kabisa mwanakijiji huyu mama aliwahi, maana enzi zile wizi ulikuwa haulindwi wala kusukiwa mikakati IKULU kama ilivyo sasa ambapo angechukua kiualaini na kuzikuta nje zinamsubiri badala ya kukimbia na bulungutu.
 
Pia inaonyesha kina nani wana time warp ya picha ya Tanzania kwa kupitwa na vitu muda mrefu sana hivyo kumbukumbu waliyonayo ni nostalgia ya vitu walivyoviacha zamaniiiiiii, ndo unakuta mtu anasema "Masikini Simbaulanga," utashangaa anahurumia mwizi kumbe ni self-sympathy ya ile time-warp.


Kama huna kumbukumbu ya zamaniiiiii basi una matatizo, au mwenzetu umefuta kumbukumbu yako yote unaishi katika sasa tu?
 
Namkumbuka huyu mama akiitwa Sarah Martin Simbaulanga. Kusema kweli mimi ni mmoja walio frommhurumia kukamatwa. Nilimuona kama sterling fulani wa bonge la movie.

Pesa alizihamishia kwa king'asti chake Mombasa, ambaye kiumri ni ki benten, Toroha Mohamed Toroha, wakanunua mabasi ya coaster kibao ambayo nayo yalitaifishwa.

Hata aliyoyafanya Kasusura was an action movie. Kitendo cha kudakwa kirahisi ni kama sterling kauwawa, kwa kawaida Sterling huwa hauwawi.

P
 
ukishawajua ndio nini:coffee:tujuzeni jamani alikuwa nani na alifanya nini katika historia ya nchi yetu.

Hakufanya jema mkulu, huyu mama alikuwa mwizi,aliiba, aliiba fedha nyingi, alikuwa pale NBC Foreign branch sasa hivi ni makao makuu ya NMB Post mpya. Alishirikiana na kijana mmoja wa kiarabu jina lake nimesahau kigodo.Back then ilikuwa fedha nyingi approximately 60ml
 
Embu tupe data kidogo Mkuu...sijui km namfaham sana so far as navyojua ni mwanamama aggressive aliyetumia kalamu yake vizuri kuiibia serikali!...sina hakika na kumbu kumbu zangu!

Huyu mama aliiba pesa milioni 30 enzi hizo zikiwa interms of cash na travellers cheque, akakimbilia Nairobi..ambako alikamatwa akiwa na mshirika wake TOROHA Mohamed TOROHA. Walirudishwa nyumbani ambako kwanza mali zao zote zilikamatwa yakiwemo mabasi etc na baadaye walishitakiwa mahakamani.

Walihukumiwa miaka 35 na kwa kuwa makosa yote yalitendeka kwa mara moja wakala miaka 7. nadhani hawa watakuwa wameshaachiwa na atakuwa uswahilini.

Kiukweli ile kesi ilikuwa ni mfano wa kesi za mwanzoo za kifisadi lakini ajabu ni kuwa siku hizi mafisadi hawakamatwi kirahisi na hata wanaokamatwa serikali inashindwa kuwa convict.

Nadhani Sara Martin Simbaulanga na Toroha Mohamed Toroha, watakuwa wanasikitika sana kuona wenzao siku hizi wanaiba and the go away with it.
 


Nadhani Sara Martin Simbaulanga.....na Toroha Mohamed Toroha..watakuwa wanasikitika sana kuona wenzao siku hizi wanaiba and the go away with it...


ndiyo point niliyotaka kuleta.. kwanini tulikuwa very serious wakati ule..? Leo kuna mama mwingine anatuhumiwa kuiba bilioni 1.3 na hakuna watu wanaoshtuka!
 
Namjua vizuri sana mama Sarah Martin Simbaulanga ni mlokole na ni mlalahoi anaonekana maeneo ya Mwenge mara chache chache.

Anajutia sana kitendo alichofanya wakati ule, Mwenyewe anasema haukuwa utashi wake bali aliponzwa na mpenzie Toroha Mohamed Toroha.

Amemrudia Mungu na anaendelea kuishi kwa amani tu.
 
Back
Top Bottom