Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,339
- 45,659
Wiki iliyopita wakati Mo Dewji akiwa katika Press Confrence ya kukabadhi Bilioni 20 za ununuzi wa hisa zake asilimia 49 za klabu ya Simba alimshukuru January Makamba kwa ushauri mkubwa ambao amekuwa akimpatia katika uendeshaji wa Klabu ya Simba.
January Makamba huwa anamshauri nini Mo Dewji katika kuindesha Klabu ya Simba ikiwa ametizama kwa macho yake Simba ikiondoka mikononi mwa wananchi kwa bei sawa na bure?
Makamba bado anataka aaminiwe na wazalendo kuupata Urais siku mmoja ikiwa watu anaofungamana nao ni wakina Mo Dewji?!
Mo Dewji kuichukua nusu ya Simba kwa bilioni 20 ni sawa na kuokota dodo chini ya Mnazi, Simba sio ya bei chee kiasi hicho.
Mtu yeyote Mwenye akili ndogo kabisa za biashara anafahamu vyema Mo ananufaishwa sana na Simba kibiashara kuliko uwekezaji wake kwa klabu hii Kubwa na Kongwe nchini japo yeye mwenye anasema hapati chochote katika kuwekeza "machozi, jasho na damu kwa Simba"