Simba Sports Club (Wekundu wa Msimbazi) | Special thread

Ninaona umuhimu mkubwa sana wa Simba SC kuweza kucheza michuano ya CAF Champions league kila mwaka. Itasaidia sana kukuza viwango. Ukishazoea kucheza na hizi timu za TPL, unaweka tafsiri finyu kwamba timu yetu iko juu.
Ndio maana naomba tuendelee kushiriki hii ligi kupambana na wababe wengine. Ukitaka kuwa mbabe, pambana na wababe wengine sio kupambana na wadhaifu halafu ukajiona mbabe. Utaadhirika.
 
Binafsi kama nimefurahia matokeo ya droo ya saoura vs al ahly. Sababu ni kwamba Saoura kama angeshinda leo ingefanya group liwe open zaidi, maana nae angekua na points 3, ikumbukwe tutawafuata kwao, lakini al ahly angeshinda ugenini angetupiga sana gap na isitoshe game ijayo tunaenda kwake

the Legend☆
 
Binafsi kama nimefurahia matokeo ya droo ya saoura vs al ahly. Sababu ni kwamba Saoura kama angeshinda leo ingefanya group liwe open zaidi, maana nae angekua na points 3, ikumbukwe tutawafuata kwao, lakini al ahly angeshinda ugenini angetupiga sana gap na isitoshe game ijayo tunaenda kwake

the Legend☆
Kweli....kundi linapokua open zaidi linakua gumu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
"Itakuwa mechi ngumu lakini hatujaja hapa kuzuia, tumekuja hapa kujaribu kutengeneza nafasi kama ilivyo kwa michezo yetu mingine na kujaribu kufunga."- Kocha Patrick Aussems kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya AS Vita Club ambao utachezwa leo Jumamosi. Simba SC Tanzania on Twitter
 
Dakika 20 za mwanzo tucheze kwa tahadhari ili tuwaone udhaifu wao na ubora wao tusikurupuke kuwashambulia,tukishajua ubora ni upi tucheze kwa tahadhari Sana na tukishajua udhaifu ni upi tutumie huo mwanya kushtukiza kutafuta goli kupitia udhaifu wao

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nidhamu yetu ilikua mbovu tumefunguka ugenini...soka la Africa kila timu nzuri ikiwa kwao Enyimba mwaka uleb2003 tupo nae kwenye makundi alifunguka misri akapigwa 6-1alivyocheza na ismailia...angalau badae Enyimba alikua bingwa na alicheza final na Hawa Hawa ismailia na akafungwa goli moja misri final first match...funzo ni Kwamba kwa mpira wa Africa ukiwa ugenini kushinda ni ngumu sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Simba inahitaji kubadilika sasa, inacheza mpira wa taratibu sana na kumiliki mpira bila malengo ya ushindi.
Simba ilimiliki mpira kuliko AS Vita lakini imefugwa.
Kuna haja ya benchi la ufundi kubadili mtindo wa uchezaji wa timu.
Simba ianze kufanya mazoezi ya kucheza mpira wa kasi na pasi ndefu mwanzo mwisho.
Mpira wa pasi nyingi unaanza kupitwa na wakati ndio maana timu ya taifa ya Brazili na Uholanzi zinafungwa sana karne hizi.
Tuishukuru timu ya AS Vita, imetuonesha namna ya kucheza mpira na kuacha mpira wa mazoea.
Mpira wa kasi unachezwa sana na vijana wachezaji kama Zana hawawezi kuumudu.
Tuchukue Somo alilotupa AS Vita na tulifanyie kazi, kama tunataka kicheza mpira wenye mafanikio uwanjani.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tukumbushane rekodi [nzuri] za Simba

*1978:* Simba 1—8 Enyimba
*1980:* Al Ahly 9—0 Simba
*1984:* Petle Atletico de Angola 6—0 Simba
*1989:* Simba 2—8 Solfa ya Gabon
*1991:* Yanga 4 —0 Simba. Simba hawakurudi second half
*1996:* All Hilaly 5—0 Simba
*1999:* Sesco 4—0 Simba
*2005:* Simba 0—4 Enyimba
*2007:* Enyimba 5—0 Simba
*2012:* Liboro de Angola 5—0 Simba
*2019:* As vita 5—0 Simba
Uzi tayari!

Kukasirika kunaruhusiwa.
Povu rukhsa.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
65 Reactions
Reply
Back
Top Bottom