Simba Sports Club (Wekundu wa Msimbazi) | Special thread

Amani kwenu wanamsimbazi ....

Kilichotokea kwa majirani zetu na mtani wetu wala hayatuhusu kinachotuhusu ni hiki cha kwetuu....yeaaaaah walete waarabu wote najua leo wale waarabu fekii watajazana kwa wingi wala hatuna shida nao ....bhasi bhana usiku baada ya kupata free mb ikabidi nizame youtube kuwacheki hawa jamaaa ,twende sawa kuna huyu jamaa wa kuitwa Bance hakimbii Sana, mtoe kwenye orodha ya kuwasumbua Simba katika pace na dribbling..... Ila anahitaji ulinzi muhimu Muda wote wa mchezo(tyt man making).... Hapa hahitaji kuwa chini ya Mlipili, Juuko, Kotei wala Kwasi katika making ya usalama wa Simba SC.... Hapa anahitaji kuwa chini ya Erasto Nyoni.

Height, weight na hata experience kidogo wanashabihiana (Bance na Nyoni).

Bance ni enegic player, tumemshuhudia akiwa na Jezi ya timu ya taifa ya Burkinafaso katika nyakati tofauti za career yake..... Nyoni Ni mult- function player hakuna asiyejua uwezo wake katika majukumu... Nakuona huyu ndiye mtu sahihi kama center half wa kupiga story na Arastid.

Uwezo mkubwa wa kupiga mita nyingi kutoka usawa lilipo goli, uwezo mkubwa wa kucheza high balls..... Hizi ndio silaha zake Mara nyingi, kupiga mashuti na kucheza Mipira ya kutengwa inayoelekezwa kwenye eneo alilopo.

Set pieces zimekuwa sumu Sana kwa Simba SC msimu huu, Aina ya makosa katika kucheza na ku clear mistake imediatly zinazotokana na Faulu, Kona na krosi, zinaweza kutengeneza salama ya Simba katika eneo la ulinzi haswa katika kipindi hichi Cha uchakavu wa gloves za Manula.

Hadithi za Simba dhidi ya waarabu Mara nyingi huvutia, hivyo basi wacha tuote Moto tusubiri saa 12 make kimvua kishaanza manyunyu


a6fdc57b4a8f8408e3146d3c61e2e336.jpg
8a5ca49b560559d41b93296cd8ce72dc.jpg
 
Back
Top Bottom