Simba Sports Club (Wekundu wa Msimbazi) | Special thread

Jaman naomba mnisaidie hivi kwanin yanga wanapochorwa kweny cartoon wanachora ndala? Je nin link kat ya ndala na yanga? Anayejua please anisaidie.

kama kumbukumbu hainitupi, kuna mwaka yanga ilipata mgogoro uliopelekea
kutokea makundi mawili ndani ya klabu, moja lilijulikana kama yanga -kandambili na
kundi ka pili yanga- raiszoni (raise-on ililikuwa design ya viatu vyenye soli ndefu kwa kwenda juu).
hata hiyo kundi la yanga-kandambili liliibuka kidedea (ndio maana wakati mwingine inaitwa yaanga-kandambili)
 
Jaman naomba mnisaidie hivi kwanin yanga wanapochorwa kweny cartoon wanachora ndala? Je nin link kat ya ndala na yanga? Anayejua please anisaidie.

kama kumbukumbu hainitupi, kuna mwaka yanga ilipata mgogoro uliopelekea
kutokea makundi mawili ndani ya klabu, moja lilijulikana kama yanga -kandambili na
kundi ka pili yanga- raiszoni (raise-on ililikuwa design ya viatu vyenye soli ndefu kwa kwenda juu).
hata hiyo kundi la yanga-kandambili liliibuka kidedea (ndio maana wakati mwingine inaitwa yaanga-kandambili)
well said g.tajiri
na pont ya pili ni kwa sababu hawa jamaa mara nyingi tuawakanyaga kama kandambili sema leo refa alitunyima penalt ya wazi kabisa
 
well said g.tajiri
na pont ya pili ni kwa sababu hawa jamaa mara nyingi tuawakanyaga kama kandambili sema leo refa alitunyima penalt ya wazi kabisa

hahahahaha pole sana st. ivunga, itabidi mnyama azoee tu dozi kwa maana bado zinakuja nyingi tele lol
 
well said g.tajiri
na pont ya pili ni kwa sababu hawa jamaa mara nyingi tuawakanyaga kama kandambili sema leo refa alitunyima penalt ya wazi kabisa.

Hakuna siku Simba atafungwa halafu mkose visingizio, kateni rufaa tuwacharaze tena. Vile vile bado mnayo nafasi ya kujinasua katika ngao ya jamii hivi karibuni ambayo nayo bila shaka mtapakatwa tuu!
 
Jamani vipi kuhusu usajili wa Felix Mumba Sunzu kuja kucheza kwenye chama letu la wekundu wa Tanzania.
 
Mkuu umasiki wa mashabiki wa yanga ni upi?
DATA zilizopo mpaka mechi ya leo yanga ndo wameingiza mapato makubwa sasa wanaokwenda uwanjani ndo masikini au,?
Ni kwa sababu yanga ikicheza mashabiki wote wa Simba na yanga wanakwenda uwanjani,Simba inapocheza mashabiki wa yanga wengi hubaki nyumbani sababu ya asili yao kuwa wao hawana interest na mechi za Simba, na wale wachache wanaokuja uwanjani ni wale ambao wamejengwa na imani kuwa Simba lazima itafungwa hiyo wanakuja kuzomea.
 
Na hii ndo itakuwa first eleven ya wekundu wa Tanzania ya msimu wa 2011/12;
1. Juma Kaseja
2. Nassoro Cholo
3. Amir Maftah
4. Juma Nyoso
5. Derick Walulya
6. Jerry Santo
7. Salum Machaku
8. Patrick Mafisango/Mwinyi Kazimoto
9. Felix Sunzu
10. Haruna Moshi
11. Ulimboka Mwakingwe.
 
Usajili:Simba wamchomoa Walulya, wamrudisha Okwi Send to a friend
Wednesday, 20 July 2011 20:54
0digg

basena.jpg
Mwandishi Wetu
SIMBA imeliondoa jina la beki wake wa Uganda, Derick Walulya katika usajili iliowasilisha kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na badala yake imemrudisha kundini, Emmanuel Okwi.

Makamu Mwenyekiti Geofrey Nyange 'Kaburu' aliliambia Mwananchi jana kuwa, sababu kubwa iliyowafanya kumtoa Walulya ni majeruhi ambayo yatamuweka nje kwa miezi miwili.

"Okwi alikwenda kwenye majaribio sehemu mbalimbali, lakini ni kama ameshindwa, hivyo kwa sababu Walulya atakuwa nje kwa miezi miwili, tumeona ni bora nafasi hiyo achukue Okwi. Hata hivyo Walulya ataendelea kupata huduma zote za Simba kwani bado ni mchezaji wetu," alisema Kaburu.

Ukiondoa Okwi, wachezaji wengine wa kigeni wa Simba ni Jerry Santo (Kenya), Patrick Mafisango (Rwanda), Gervais Kago (Jamhuri ya Afrika ya Kati) na Felix Mumba Sunzu (Zambia).

Awali, Kocha Mkuu wa Simba, Moses Basena alisema hafahamu kinachomsumbua Okwi kwa sababu alijaribu kumtafuta mjini Kampala, lakini hakumpata.

Basena alikuwa mjini Kampala kwa mapumziko mafupi ya wiki moja baada ya kumalizika mashindano ya Kagame na hivi sasa yupo na kikosi cha Simba jijini Da es Salaam akikinoa kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu 2011/2012.

"Nilijaribu mara nyingi nilipokuwa Kampala kumpigia simu Okwi, lakini alikuwa hapokei simu zangu,"alisema kocha wa Simba.

Alisema,"Sijui ni nini kimemsibu kijana Okwi na sifahamu kwa nini alikimbia katika klabu ya Kaizer Chiefs alipokuwa amekwenda kufanya majaribio nchini Afrika Kusini, lakini Okwi kwa sasa ni mtu mzima na anajua afanyalo."

Hata hivyo; kwa mujibu wa gazeti la Daily Monitor la Uganda, kocha Basena alikiri kwamba Okwi yupo mjini Kampala.

Pia, kwa mujibu wa gazeti hilo, kocha wa Kaizer Chiefs, Vladimir Vermezovic alishangazwa na Okwi ambaye alivutiwa naye baada ya kufanya majaribio kwa wiki moja mwisho wa msimu uliopita, lakini Okwi hakuenda kwa mara ya pili kama alivyotakiwa kufanya na klabu ya Kaizer Chiefs mwezi uliopita.

Vyombo vya habari vya Afrika Kusini vimekuwa vikilizungumzia tukio hilo huku vingine vikisema Okwi yupo nchini Uturuki akifanya majaribio, lakini gazeti la Daily Monitor la Uganda lenyewe limesema Okwi alikwenda Afrika Kusini na kukaa siku moja Afrika Kusini kabla ya kumuambia wakala wake Ivica Stankovic kwamba anarudi nchini Uganda kwa mazishi ya ndugu yake.

Gazeti hilo la Uganda pia limemnukuu makamu mwenyekiti wa klabu ya Simba, Geofrey Nyange Kaburu akisema,"Tupo katika mchakato wa kumuuza Emmanuel Okwi katika klabu nyingine."

Pia, gazeti hilo limesema Okwi ambaye ana mkataba na Simba mpaka 2014 ameachwa kwenye usajili wa Simba msimu wa 2011/12.

Okwi alitakiwa afanye majaribio kwa mara ya pili na klabu ya Kaizer Chiefs ambayo ilionyesha nia ya dhati ya kutaka kumsajili mshambuliaji huyo hatari akiwa karibu na lango.

Wakati huo huo; Calvin Kiwia anaripoti kuwa beki chipukizi wa Simba, Shomari Kapombe ameitaka timu yake ya zamani Polisi Morogoro kuacha kumwekea vikwazo kwenye usajili wake kwani alishamalizana nao toka kumalizika kwa fainali za Ligi Daraja la Kwanza.

Hayo yamekuja baada ya klabu hiyo kuwasilisha barua katika shirikisho la soka chini, TFF kuweka pingamizi usajili wa kinda huyo.

Kapombe aliliambia Mwananchi jana jijini Dar es Salaam kuwa alishamalizana na timu hiyo toka pale Ligi Daraja la Kwanza hatua ya fainali ilipomalizika, lakini anashangaa uongozi wa timu hiyo umemwekea pingamizi kwenye usajili wake.

"Nilisaini fomu za kuichezea Polisi Morogoro mpaka Ligi Daraja la Kwanza hatua ya fainali itakapomalizika, lakini nashangaa wanataka nini tena kwangu wakati makubaliano yetu yameshamalizika,"alisema Kapombe.

Alisema anautaka uongozi huo uachane naye kwani tayari makubaliano yao yalishamalizika tangu kumalizika kwa Fainali za Ligi Daraja la Kwanza zilizofanyika jijini Tanga kuanzia Januari 30 hadi Februari 22 mwaka huu.

"Sina mkataba na Polisi Morogoro nawaomba waniache niweze kucheza mpira kama kazi yangu ambayo naamini ipo siku moja itaninufaisha na kuwa na maisha bora kama walivyo wengine," alisisitiza Kapombe.
 
Simba yashtukia hujuma nzito
7905.jpg
Mwenyekiti wa simba Ismail Aden Rage
MICHAEL MOMBURI
SIMBA imedai kushtukia hujuma nzito kuhakikisha kwamba inadhoofika katika mechi ya Ngao ya Hisani dhidi ya Yanga, Agosti 17 ndani ya Uwanja wa Taifa.

Uongozi huo umetamka kwamba utafanya maamuzi mazito leo Jumamosi itakapokutana Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo na tayari Mwanaspoti linajua kwamba watasusia mechi hiyo iliyopangwa kuchezwa usiku.

Msimamo huo wa Simba umekuja baada ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria, Maadili na Hadhi za Wachezaji, Alex Mgongolwa kutamka rasmi kwamba jopo hilo limeafiki kwamba mshambuliaji wa Afrika ya Kati, Gervais Kago haruhusiwi kuichezea Simba kwa kuwa hajahamishwa kwa taratibu za kimataifa.

Kwa mujibu wa Mgongolwa, straika huyo mwenye shabaha amehamishwa kwa njia ya ridhaa na si njia ya kulipwa kama taratibu za hapa za kimataifazinavyoeleza jambo ambalo hata Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah amekiri.

Lakini Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage aliiambia Mwanaspoti jana Ijumaa kwamba kuna hujuma za waziwazi za kuidhoofisha timu yake kuelekea kwenye mechi dhidi ya Yanga, Jumatano ijayo na kwamba yeye anatambua Kago ni halali yao.

"Kuna njia mbili za kuhamisha wachezaji kwanza kwa ridhaa na pili kulipwa, Kago vibali vyake vimetumwa moja kwa moja TFF lakini si kwa njia ya kompyuta, hivyo haimaanishi kwamba haruhusiwi kucheza ligi ya ndani."

"Vibali vilivyokuja vinamruhusu kabisa kucheza ligi ya ndani wakati hizo taratibu zingine zikiendelea, na ndio maana kamati hiyo ambayo hata mimi ni mjumbe tuliona kwamba uhamisho wa Kago hauna matatizo lakini baadae nashangaa tena kusikia TFF imetoa tamko jingine,"alisisitiza Mwenyekiti huyo ambaye ni mchezaji wa zamani wa Simba.

"Hiki kinachoendelea ni hujuma kama zilizotaka kufanyika dhidi ya Mwinyi Kazimoto kwenye mechi ya fainali ya Kombe la Kagame, hatukubali, tumewaambia watupe barua rasmi ya maamuzi na kifungu cha sheria waliyofanyia maamuzi.

Baada ya hapo tutakaa kikao cha Kamati ya Utendaji kesho(leo) Jumamosi na tutangaza maamuzi mazito ambayo naomba yawe siri kwanza, lakini yatatikisa nchi na kila mtu atashangaa, "alisisitiza Rage na kusema Simba iko tayari kwa lolote.

Lakini Mwanaspoti linajua kwamba Simba isiporuhusiwa kumtumia mchezaji huyo wa zamani wa Bangui FC inasusia mchezo wa Ngao ya Hisani, Jumatano iliyopita. Kago ameonyesha kiwango cha juu akiwa na Simba katika kipindi kifupi na kocha Moses Basena amemkubali huku mashabiki mazoezi wakimpa nafasi kubwa ya kuifunga Yanga na kutisha kwenye Ligi.
 
Ngassa: Tutawaziba mdomo Simba na Yanga
7904.jpg
Mrisho Ngassa
OLIVER ALBERT
MRISHO Ngassa wa Azam FC ametabiri kuwa msimu huu ndio mwisho wa ngebe na tambo za Simba na Yanga ambazo zimekuwa zikipokezana nafasi mbili za juu kila mara.

Azam imewasajili washambuliaji Kipre Tcheche wa Ivory Coast na Mghana Wahabu Yahaya kuongezea nguvu kikosi hicho kilichomaliza nafasi ya tatu msimu uliopita. Mbali na hao pia kuna mafowadi wazalendo kama John Boko na Ngassa.

Ngasa ambaye atajiunga na Seattle Sounders ya Marekani Februari mwakani; "Timu yetu msimu huu iko moto sana nafikiri kila moja ameiona, ina wachezaji wote wazuri kuanzia mabeki, viungo na washambuliaji na wote wanafanya kazi kubwa uwanjani hivyo ligi itakuwa kali sana.

� Utawala wa Simba na Yanga utakoma ligi ikianza, ni mwendo wa kazi tu kuhakikisha nafasi mbili za juu tunashika mojawapo, kwani wao waweze wana nini na sisi tushindwe tuna nini, hivyo watu wasubiri kuona, tutafunika sana,� alisema Ngasa ambaye aliweka rekodi ya Mtanzania wa kwanza kucheza dhidi ya Manchester United ya England.

Timu hiyo itafungua pazia la Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kucheza na Moro United kwenye uwanja wao uliopo Chamazi, Mbagala.
 
Ni kwa sababu yanga ikicheza mashabiki wote wa Simba na yanga wanakwenda uwanjani,Simba inapocheza mashabiki wa yanga wengi hubaki nyumbani sababu ya asili yao kuwa wao hawana interest na mechi za Simba, na wale wachache wanaokuja uwanjani ni wale ambao wamejengwa na imani kuwa Simba lazima itafungwa hiyo wanakuja kuzomea.
Upo sahihi sana mkuu
 
Back
Top Bottom