Simba Sports Club (Wekundu wa Msimbazi) | Special thread

Wawa ni beki wa kisasa...ni aina ya beki anae anzisha mashambulizi...tazama magoli yote ya Simba,Pass ya tatu inayo zalisha goli Mara nyingi ina toka kwake.Wewe una taka beki wa kizamani anae subiri kukaba tu,Kumbuka Simba ni timu inayo miliki sana Mpira hivyo mabeki nao wana kuwa sehemu ya kuchezesha timu.Kazi hii ya kuchezesha timu kuanzia ngazi ya beki Wawa ana ifanya kwa ukamilifu kabisa,Simba walimuacha Juuko ambae ana fahamu sana kukaba,unadhani walifanya makosa?
Juuko anajua kukaba ila muundo wa uchezaji wa Simba ulimnyima nafasi ya kucheza,Juuko sio mzuri kuanzisha mashambulizi kuanzia chini,yeye ni mzuri kukaba tu.
Mtazame Pique pale Barca uwezo wake wa kukaba sio mkubwa sana,ila angali build up ya timu kuanzia chini,utaona umuhimu wake.
Wawa ana tuonyesha soka la kisasa na mabeki wa kisasa wana takiwa kufanya nini.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa kukazia Wawa ni aina ya Rio Ferdinand na John Terry, VVD, Maguire, Koulibary, shambulizi linaanzia nyuma kwenda kiungo + striker
Mabeki wenye sifa hizi ulimwenguni ni wachache na ndio maana sokoni wanauzwa ghali sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna tetesi za kusajiliwa Mwamnyeto ila anabaki Cost union atakuja msimu ujao
Pia usajili wa yule mshambuliaji wa UD SONGO, huyu anakamilisha tu mambo madogo aje Msimbazi.
Kila la kheri Simba dhidi ya KMC leo
 
Asee hilo li tariq seif Kiakala kila pande ya uwanja lipo,hadi kwenye kufunga lipo. Hatari sana. Li Nchimbi sijui limejificha wapi,na kuna lile li ivory coast sijui kabeki ketu ka wawa na uzee wake katafanyaje siku hyo.
 
IMG_20200103_153716.jpg

Mabingwa wa nchi Simba tumemalizana rasmi na kiungo wa kimataifa wa Mozambique, Luis Jose Miquissone ambae alikuwa mchezaji wa Mabingwa wa nchi hiyo UD Songo. Kiungo huyo tayari amekabidhiwa jezi na kocha wetu mkuu Sven Vandenbroeck kama inavyoonekana pichani. #NguvuMoja Simba Sports Club on Twitter
 
Back
Top Bottom