Simba Sports Club katika hili mnanikwaza na nina uhakika kuwa mnawakwza na wengineo wengi tu

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,468
108,621
Niliwahi kusema hapa hapa kuwa kwa Tanzania ya sasa hakuna na sijaona Kiungo bora wa nyuma kama Mdogo wangu mwenye wa Kinondoni Biafra na Muslim Jonas Gerald Mkude ambaye Mimi hupenda Kumuita na Kumfananisha Kiuchezaji na Kiungo wa Kireno Deco de Souza na nakumbuka sikueleweka lakini kwa ' Mavitu ' ya Mkude sasa na jinsi alivyobadilika na Kukomaa Kimpira naanza Kueleweka.

Kama Jicho langu lilivyoona kwa Jonas Mkude na leo nasema tena hapa hapa kuwa kama kuna Beki ambaye Simba Sports Club itamuamini, itamsaidia Kisaikolojia na kumpa nafasi Kikosini atatusaidia mno katika nafasi ya Ulinzi ( Defence ) ya Simba SC ambayo sasa ndiyo ' inapwaya ' sana basi ni Mdogo wangu wa Kitangiri na Mitaa ya Ghana Mkoani Mwanza Yusuph Mlipili.

Nakumbuka hata wakati alipokuwa akicheza Soka lake hapa Tanzania Beki ' Katili ' wa Uganda ' Mtoto wa Mjini ' Juuko Murshid kuna Siku nikiwa napiga nae Stori mbili tatu aliwahi kusema kuwa huwa akipangwa na Beki Yusuph Mlipili huwa anajisikia vyema sana kwakuwa ' Dogo ' anajua mno Majukumu yake na anakaba ' Kiakili ' mno na kwamba hata Uchezaji wa 'Kisela ' nao anaujua vile vile halafu ni Beki 'Mjanja Mjanja ' hivi.

Haijapita hata Wiki moja sasa tokea nikutane na Beki ' Gaidi 'wa Yanga Sports Club Kelvin Patrick Yondan ambapo sikutaka hata Kumchelewesha na nikamuuliza Kimpira je, tatizo la Simba SC sasa lipo wapi na Yeye bila Kuficha akasema kuwa ni upande wa Beki ya Kati. Kelvin akaenda mbele na kusema kuwa kama kuna Beki mwenye Uwezo na Kipaji Kikubwa ndani ya Simba SC basi ni Yusuph Mlipili na anashangaa kwanini Simba SC ni kama vile imemtupa na hata Kumsusia.

Kwenu Uongozi wa Simba SC hasa Benchi la Ufundi chonde chonde kama mna tatizo lolote na huyo Dogo Yusuph Mlipili naomba mmalizane nae haraka ili aanze Kutumika ( Kucheza ) na huu ndiyo nafasi yake sasa. Tukiendelea na hawa ' Vibabu ' na ' Vikongwe ' akina Erasto Nyoni na Pascal Wawa tujiandae kuwa tunashinda Goli 4 kwa 3 au 5 kwa 4 au 3 kwa 2 au 2 kwa 1. Na kama tukiendelea Kuwaamini hawa ' Wazee ' kwa Uchezaji wa Fundi wa Yanga SC Benard Morrison Siku ya Mechi yetu ya marudiano nao huenda Yanga SC ikapata Penati nyingi mno kwakuwa akina Nyoni na Wawa watamshindwa na wataishia Kumchezea Rafu tu za Kijinga ( Kingumbaru ) kama siyo za Kipumbavu ( Kipopoma )

Naomba Beki Yusuph Mlipili ( Kitasa Chuma ) arudishwe haraka Kikosini na awe sehemu ya Kikosi cha Kwanza cha Simba SC.
 
Sawa lakini kwa mfano goli la pili alilofungwa Simba ilikuwa ni kosa na ukabaji pale kati, jamaa kapata muda mwingi wa kujikunja na kujikunjua kitu nyavu....na ukizingatia makipa wa Simba ukitaka kuwafunga we agizia kombola kali la kati wote wabovu.

Hata mimi nina concern kwa nini hawampagi kijana machachari Mzamiru pale kati? Ni mwepesi, anakaba na anatumia akili sana awapo uwanjani.
 
Genta umerudi tulimisi sana ...habari zako kutoka Pemba,pale ilipokaribia Januari 4!
Upo sahihi ,hali ilivyo sasa ukikutana na washambuliaji wenye kasi kama huyo mayenu wa Yanga au hata Pastor Atanas ,...tutaishia kususa kama MO!
hATA MIMI SIELEWI TATIZO LA MLIPILI NI NINI!
Na huu mtindo wa kocha kutobadilisha kikosi hata kama mazingira ya ushindi ni magumu inashangaza! Juzi lile goli lilitokana na kazi mujarabu ya John Boko! Inakuwaje kila siku aanzie Benchi,yuko wapi Muzamir,Miraj,Keneddy Juma, Kanda !!!? Mfano juzi wakati timu ina mazingira magumu ilimhitaji mtu wa kukimbiza na kukaa na mpira na Dogo alikuwepo pale benchi.
Tukitoa mawazo mazuri mnasema kila Mtanzania ni kocha wa soka ilhali vitu vipo wazi kabisa!
Siamini kamam Matola ni msaidizi wa huyu Mzungu....siamini!
 
Tatizo la beki pale simba ni la mda mrefu sana,hasa kwenye upande wa center half,
Tangia alipotoka "nampoka nyumba" balaa likaanzia hapo,Angalau kidoogo Jurko Murshid wkt wake palikua na combination ya kueleweka,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
tatizo simba misumari, mlipili anapigwa misumari na akina tshabalala, wawa mpaka kocha hamuoni kabisa, ona manula ameshaanza kumpiga misumari kakolanya
 
Back
Top Bottom