Simba Sports Club achaneni na nia yenu ya kumfukuza kocha wetu Patrick Aussems kwani tutakuja kujuta na kulia akiondoka

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,544
108,873
Nimezifuatilia sababu za baadhi ya Viongozi wa Simba SC na Mashabiki ' Wapuuzi ' wachache juu ya sababu zao kutaka Kocha Mkuu wa Simba SC Patrick Aussems aondoke na Kugundua kuwa zote ni za Kipopoma. Moja ya sababu ambayo hadi hivi sasa imeniacha hoi ni kwamba baadhi ya Viongozi hawamtaki Kocha Patrick Aussems kwakuwa huwa hataki Wachezaji wakae Kambini muda wote na badala yake huwa anataka Timu ikusanyike Siku mbili kabla ya Mechi.

Sasa kama Simba SC tumeshakubaliana Kuingia katika Mfumo wa Kisasa ni kwanini tena tunakuwa na Mawazo ya Kiswahili Kiswahili hivi? Hivi Vilabu vikubwa na vyenye Maendeleo makubwa duniani Wachezaji wao huwa wanashinda tu Kambini Msimu mzima wa Ligi kama wako Shule za ' Bodingi ' ambazo wengi wetu tumepita huko?

Maoni yangu kama GENTAMYCINE na naomba mnisikie Kiumakini kabisa ni kwamba kama kuna Kocha ambaye Simba SC tunaweza kuwa tumepata bahati ya kuwa nae basi ni huyu Patrick Aussems. Nina Wachezaji Waandamizi kabisa wa Simba SC na mwingine sasa anacheza nchi nyingine wote kila ninapozungumza nao wanasema hawajaona tatizo la Kocha Aussems hasa Kimbinu na Kiufundi na Kuondoka Kwake kutaiathiri Klabu kwa Kiasi kikubwa mno.

Sikatai Aussems kama Binadamu anaweza akawa na Matatizo ( Mapungufu ) yake ila tukisema tumfanyie ' Assessment ' hakuna Mtu ambaye anaujua vyema Mpira na amewahi pia Kuucheza anaweza kukubali Kocha Aussems afukuzwe Klabuni. Moja ya Sifa Kuu ya Kocha japo zipo nyingi ni Kocha kuwa na Upendo na Ukaribu hasa wa Kiurafiki na Wachezaji wake kwani hii husaidia Yeye kuweza Kupitisha Mafunzo yake Kiurahisi kabisa na akafanikiwa. Hili Kocha Aussems amefanikiwa nalo kwa 100% ndani ya Klabu ya Simba.

Hivi Kocha ambaye hadi hivi sasa ameifanya Simba SC iongoze Ligi, Timu inacheza vizuri na hata kama huwa inafungwa au inatoka Sare nayo ni sehemu ya Mchezo kwani Falsafa ya Mpira duniani kote inasema kuwa Mpira ni Mchezo wa Kushinda, Kufungwa na Kutoka Sare. Simba SC isifungwe au isitoke Sare yenyewe ni nani? Ni Timu ya Mungu? Kama ni sababu za Kiufundi Kocha Aussems hana tatizo ndani ya Simba SC ila kama Kocha Aussems anafukuzwa pengine kwakuwa hapendi Ujinga, Utoto na Upumbavu tena ule wa Kupangiwa Kikosi au wa kutoa 10% kwa baadhi ya Watu wa karibu wa Simba SC na Viongozi basi ni sawa afukuzwe tu na Mimi GENTAMYCINE nitapiga Goti kwa Mungu ili niiombee ' Laana ' Klabu yangu hii pendwa ya Simba SC.

Mwisho najua na nina uhakika kuwa ' Mwekezaji ' wa Simba SC ' Tajiri ' Mohammed Mo Dewji ni Mdau mzuri na mkubwa wa huu Mtandao wa JamiiForums, tunae hapa 24/7 japo huwa hakai muda mwingi kutokana na Ratiba zake lakini pia ni Mtu ambaye huwa anapenda Kunisoma GENTAMYCINE. Hivyo basi namwomba ( nakuomba ) Mohammed Dewji hebu na Wewe acha Kuingizwa katika huu ' Uswahili ' wa baadhi ya Viongozi wa Simba SC na Mashabiki ' Wapuuzi ' ambao wanakudanganya kuhusu Kocha Patrick Aussems na Wewe unawaamini na Kukubali kuwa atimuliwe.

Nina uhakika tena wa 100% kama Kocha Patrick Aussems atabaki Simba SC, akiaminiwa zaidi, akipewa Ushirikiano, Uweledi ukitawala ndani ya Uendeshaji wa Timu yetu ya Simba, akaongozewa Wachezaji Wawili au Watatu tu ( hasa Washambuliaji ), tukaachana na hawa Wabrazili wa ' Madili ' huku tukijitahidi Kuwarudisha akina James Kotei na Emanuel Okwi Simba SC itafanya vyema si tu katika Ligi Kuu yetu y VPL bali hata katika Mashindano ya Kimataifa ya Barani Afrika.

GENTAMYCINE nakataa na nasema Kocha Patrick Aussems asifukuzwe ndani ya Klabu yetu ya Simba kwani tutakuja Kujuta.
 
Ukweli usiokuwa na shaka, kuna tatizo labda kocha kaishiwa mipango, nikiitizama simba inacheza km si timu vile, wanashinda kwa uwezo wa mchezaji mmoja mmoja.

Nadhani kagere kachoka, ama ni mzuri zaidi akicheza na pacha wake(double strikers) labda kocha hajaliona hili, ila mie naona timu inacheza kwa uwezo binafsi wa wachezaji, ila coach km mipango imemuishia hivi.
 
Unalosema laeza kuwa sahihi, mimi nahisi kuna kimgogoro fulani kinaendelea kati ya kocha na uongozi, Simba tunajua kabsa tatizo letu lipo pale mbele kwene ushambuliaji but walichofanya kwene usajili wanajua wao kwakweli, yaani hakuna haja ya kumfukuza kocha ila tuongeze uweledi zaidi, tusikilize maoni ya kocha, ili timu iende kisasa zaidi, !! Ushauri wangu tuondoe ile brazilians yote, na tuongezefowards matata mbele, na kiungo mkata umeme kusaidiana na mzamiru, na mkude!!
 
Hao Wachezaji wako unaosema kuwa ni Uchezaji wao wa Kibinafsi unaoisaidia Simba SC isingekuwa Kuunganishwa na Kupangwa katika Mechi na Kocha ambaye anawajua vyema na anakaa nao muda mwingi Simba SC ingefanikiwa? Na kama Kocha huwa hana mchango ni kwanini sasa huwa anasimama katika ' Touchline ' muda wote wa Mchezo? Je, pale huwa anakuwa anatoa Maelekezo kwa Wachezaji wake au wa Timu Pinzani? Mafanikio ya Simba SC hii ya sasa 50% ni Kocha Patrick Aussems na 50% iliyobaki ni Mwekezaji, Uongozi, Wanachama, Mashabiki na Waganga wa Kienyeji.
 
Na Ameshasimamishwa Tiari! Tunasubiri Ahadi Yako Yakuikacha Timu Pendwa Hapa Afrika! Kama Walimtimua Pierre Rechantre Itakua Huyu Ambae Hana Away Game Plan Yakuzuia Timu Isiruhusu Magoli Lundo?
 
Unalosema laeza kuwa sahihi, mimi nahisi kuna kimgogoro fulani kinaendelea kati ya kocha na uongozi, Simba tunajua kabsa tatizo letu lipo pale mbele kwene ushambuliaji but walichofanya kwene usajili wanajua wao kwakweli, yaani hakuna haja ya kumfukuza kocha ila tuongeze uweledi zaidi, tusikilize maoni ya kocha, ili timu iende kisasa zaidi, !! Ushauri wangu tuondoe ile brazilians yote, na tuongezefowards matata mbele, na kiungo mkata umeme kusaidiana na mzamiru, na mkude!!
Simba ilianza kuvurugika katika usajili hilo nakubaliana na wewe 100%

Ila sasa naona kocha kashindwa kuwaunganisha hawa wachezaji waliopo na kuwatumia vizuri, ukiitizam timu haichezi kimuunganiko vizuri, ni mchezaji mmoja mmoja na uwezo binafsi, muda mwingi simba linapigwa show game, wakat mwingine wanafanya mambo kuonekana na jukwaa ila sio ya msingi kwa faida ya timu. Rudia kutizama game chache kadha z hivi karibuni, kisha utaona hili suala.
 
Hao Wachezaji wako unaosema kuwa ni Uchezaji wao wa Kibinafsi unaoisaidia Simba SC isingekuwa Kuunganishwa na Kupangwa katika Mechi na Kocha ambaye anawajua vyema na anakaa nao muda mwingi Simba SC ingefanikiwa? Na kama Kocha huwa hana mchango ni kwanini sasa huwa anasimama katika ' Touchline ' muda wote wa Mchezo? Je, pale huwa anakuwa anatoa Maelekezo kwa Wachezaji wake au wa Timu Pinzani? Mafanikio ya Simba SC hii ya sasa 50% ni Kocha Patrick Aussems na 50% iliyobaki ni Mwekezaji, Uongozi, Wanachama, Mashabiki na Waganga wa Kienyeji.

Mzee kusimama katika touchline sio sababu, unai emery anasimama katika touchline kuna kipi cha ajabu, kwani pale huwa hatoi maelezo pale, unaweza kutoa maelezo yakawa ya hovyo.
Kwenye timu kocha ana nafasi na wachezaji wana nafasi, chukua simba ikacheze na timu mbovu kama arsenal utaona matokeo yake, unadhani kitakachowafunga simba ni nini!?

Tizama tena simba ikicheza angalia vizuri utagundua hili.
 
Mwina Kaduguda anaongea EFM RADIO, 20 billions tzs zimeshaingia tiari kwene account ya simba, hapa tukifanikiwa kuuza na hisa kwa wanachama, waow, sipati picha simba ya baada ya miaka mitatu au minne huko mbele
 
Simba ilivurugwa na waswahili ila mzigo anataka kuangushiwa Patrick Aussems.

Ukiangalia kikosi cha simba 75% wako above 30 unategemea timu ya ushindani kwa hao veterans?

Timu imetwaa ubingwa unawaacha key players unaenda kukusanya lundo la average players na kuanza kutamba kwenye media kuwa utafanya vizuri ?

Hivi kweli Simba hawakumuona Bakary Nondo Mwamnyeto au Timothy Awany kama replacement ya Juuko Murshid badala yake wakaenda kuleta hiyo mizigo ya kibrazil na yule rasta wa Singida United ?

Hivi kweli Simba hawakumuona Allan Okello wa KCCA ya Uganda kama replacement ya Emanuel Okwi badala yake wanaenda kutuletea huyo mzee Deo Kanda na Wilker ?

Hivi Simba hawakumuona Tadeo Muwanga wa Vipers ya Uganda kama replacement ya Kotei badala yake wakaenda kutuletea Fraga asiye na uwezo wa kuhold hata mpira ?

Kama waliweza kumuona Kahata walishindwa kumuona Fred Kulembe kwenye mashindano ya Afcon kama back up ya chama na replacement ya Niyonzima?

Hivi walimsajili Ibrahim Ajib wa nini wakati hana matumizi na hana msaada wowote kwa timu kwanini wasingeweka pesa walau kwa Eliud Ambokile wa Mbeya city badala ya huyu jackal of all trades but master of none ?

Hivi Haruna Shamte na Gadiel waliwasajili wa nini wakati uwezo wao ni mdogo kwanini wasingeenda kubomoa fullback zote za Azam na kuzihamishia simba tu badala ya kuanza kuhangaika na hao wavuta bangi ?

Simba kama wanamfukuza Aussems basi watakuwa wametukosea sana sisi mashabiki wao.
Simba ilianza kuvurugika katika usajili hilo nakubaliana na wewe 100%

Ila sasa naona kocha kashindwa kuwaunganisha hawa wachezaji waliopo na kuwatumia vizuri, ukiitizam timu haichezi kimuunganiko vizuri, ni mchezaji mmoja mmoja na uwezo binafsi, muda mwingi simba linapigwa show game, wakat mwingine wanafanya mambo kuonekana na jukwaa ila sio ya msingi kwa faida ya timu. Rudia kutizama game chache kadha z hivi karibuni, kisha utaona hili suala.
 
Simba ilianza kuvurugika katika usajili hilo nakubaliana na wewe 100%

Ila sasa naona kocha kashindwa kuwaunganisha hawa wachezaji waliopo na kuwatumia vizuri, ukiitizam timu haichezi kimuunganiko vizuri, ni mchezaji mmoja mmoja na uwezo binafsi, muda mwingi simba linapigwa show game, wakat mwingine wanafanya mambo kuonekana na jukwaa ila sio ya msingi kwa faida ya timu. Rudia kutizama game chache kadha z hivi karibuni, kisha utaona hili suala.
Sioni kama suluhisho ni kumuondoa kocha.
Hii timu kwa kiasi kikubwa imeleta wachezaji wapya. Wakati ya msimu uliopita ilishakuwa imekaa muda mrefu. Kwangu ni mapema na ujinga kumuondoa kocha. Ndio tutapotea mazima.
Kingine sajili za kibongo ni mbovu mno. Usajili unafanywa na viongozi. Hata Ajib sidhani kama kocha alimuhitaji ni mahaba tu ya viongozi.
 
After all hiyo timu iliyofanya vizuri ilianza kuandaliwa misimu mitatu iliyopita sasa hii waliyokusanya wao kama national team wanataka ifanye vizuri all of a sudden ?
Sioni kama suluhisho ni kumuondoa kocha.
Hii timu kwa kiasi kikubwa imeleta wachezaji wapya. Wakati ya msimu uliopita ilishakuwa imekaa muda mrefu. Kwangu ni mapema na ujinga kumuondoa kocha. Ndio tutapotea mazima.
Kingine sajili za kibongo ni mbovu mno. Usajili unafanywa na viongozi. Hata Ajib sidhani kama kocha alimuhitaji ni mahaba tu ya viongozi.
 
Aondoke zake hana adabu. Anaondoka kwenda kutafuta timu nyingine kihunihuni. Atuachie timu yetu. Wanakuja wenye weledi zaidi. Simba tuna pesa za Mo. Mtu akilete ujinga tunatimua tu.
 
Simba ilivurugwa na waswahili ila mzigo anataka kuangushiwa Patrick Aussems.

Ukiangalia kikosi cha simba 75% wako above 30 unategemea timu ya ushindani kwa hao veterans?

Timu imetwaa ubingwa unawaacha key players unaenda kukusanya lundo la average players na kuanza kutamba kwenye media kuwa utafanya vizuri ?

Hivi kweli Simba hawakumuona Bakary Nondo Mwamnyeto au Timothy Awany kama replacement ya Juuko Murshid badala yake wakaenda kuleta hiyo mizigo ya kibrazil na yule rasta wa Singida United ?

Hivi kweli Simba hawakumuona Allan Okello wa KCCA ya Uganda kama replacement ya Emanuel Okwi badala yake wanaenda kutuletea huyo mzee Deo Kanda na Wilker ?

Hivi Simba hawakumuona Tadeo Muwanga wa Vipers ya Uganda kama replacement ya Kotei badala yake wakaenda kutuletea Fraga asiye na uwezo wa kuhold hata mpira ?

Kama waliweza kumuona Kahata walishindwa kumuona Fred Kulembe kwenye mashindano ya Afcon kama back up ya chama na replacement ya Niyonzima?

Hivi walimsajili Ibrahim Ajib wa nini wakati hana matumizi na hana msaada wowote kwa timu kwanini wasingeweka pesa walau kwa Eliud Ambokile wa Mbeya city badala ya huyu jackal of all trades but master of none ?

Hivi Haruna Shamte na Gadiel waliwasajili wa nini wakati uwezo wao ni mdogo kwanini wasingeenda kubomoa fullback zote za Azam na kuzihamishia simba tu badala ya kuanza kuhangaika na hao wavuta bangi ?

Simba kama wanamfukuza Aussems basi watakuwa wametukosea sana sisi mashabiki wao.
Kula like kwanza, sikukatalii mzee kwenye usajili waliboronga tena mnoo.

Wewe sasa ndio umeongea point kwamba viongozi wanamsukumia mzigo wa lawama coach, tukubali kuwa timu haichezi vizuri sasa hapa inategemea na mbinu za coach na wachezaji aliokuwa nao, so simba haichezi kitimu ila tatizo lilianzia kwenye usajili. Toka game na u.d songo simba tunaruka ruka tu uwanjani, hakuna mipango kabambe kabisa ya kitimu, na simba ikikutana na timu imeshiba mbinu za mwalimu wanacheza kitimu huwa tunapata tabu, tunashinda sababu uwezo wa wachezaji wetu ni zaidi yao kwa mbali ila tunakuwa tunaruka ruka tu.
 
Aondoke zake hana adabu. Anaondoka kwenda kutafuta timu nyingine kihunihuni. Atuachie timu yetu. Wanakuja wenye weledi zaidi. Simba tuna pesa za Mo. Mtu akilete ujinga tunatimua tu.
Kocha kuondoka sio suluhisho kabsa, kiukweli usajili wetu haukufanywa kiweledi zaidi, mimi nachohisi itakuwa uongozi uliogopa gharama kubwa , labda kutokana na hii program ya ujenzi wa viwanja inaeza punguza ukubwa wa matumizi!! Tusubiri usajili ujao tuone nini watafanya , nategemea kuona damu changa zikiwa nyingi zaidi, vipaji maridhawa vikiwa vinatisha pale simba!! Ila ile mibrazil hapana kwakweli mimi bado sijapata ushawishi kabsaa
 
Back
Top Bottom