Simba Sport Club: Yanga angekuwa Na fedha Simba kombe mngelisikia!

The hammer

JF-Expert Member
May 17, 2011
2,381
1,760
Hivi Omog angekuwa Na kikosi Kama cha Yanga ingekuwaje.Omog aende Yanga.

MTU anashindwa kuwatumia wachezaji wazuri ni wanini Simba.Ajib kaenda Yanga Na sasa ndo STAR pale Yanga ila Simba alionekana kana kwamba hajui.

Niyonzima alivyokuwa Yanga alikuwa kiungo Wa kumuogopa kwa jinsi alivyokuwa anagawa mipira ila hii Leo muda sio mrefu ataanza kuzomewa uwanjani.

Mudhamiru naye anaanza kupotea kwa kasi.

Gyan alikuwa mfungaji mzuri huko Ghana ila amekuja hapa Simba ligi inamshinda Kama inavyomshinda Mavugo.Inawezekana vipi ligi ya Tanzania ikawa bora kuliko ya Ghana?

Kuna kiungo mchezaji yupo vyema Sana ila hadi kelele zipigwe ndo anaanza kucheza.Mohamed Ibrahimu.Huyu anatatizo gani Na Omog.

SlKama nilivyosema awali tatizo ni Omog basi Leo uwanja nautanua.Uongozi Wa Simba wote ni mamluki.Haiwezekani....Hawawezi kumfukuza kocha mzuri Mserbia Milovan kopovic Kama sijakosea Na kumvumilia Omog Wa kila Leo ushindi wa wasiwasi Siku nenda rudi.Kila mwaka yeye anachojua ni kupanga ulinzi imara ila ushambuliaji ni Sifuri kabisa.

Milovan alikuwa akiichezesha timu hadi unafurahi.Leo hii Sijui Simba wanachezaje no penetration pass Na wanacheza Kama wanarendemka Kama milenda.Sijui mafunzo gani ya Omog.

Nasikia viongozi wanataka kusajili tena dirisha dogo.Sijui Kama wanajielewa.Mtaleta wachezaji 100 Na hakutakuwa Na mabadiliko yoyote Kama Omog ataendelea kuhudumu pale.Wamuondoe kisha tuone Kama Mavugo sio mchezaji mzuri,kama Mo naye ni mchezaji Wa hovyo? Kama Gyan Naye ni garasa?Na Pia kama Niyonzima,Ndemla Na Mudhamiru wanachuja? Au ni Omog ndo atakuwa amepauka Sana?
 
The hammer hizo ni stori za unazi tu, mbona msimu uliopita Simba aliongoza muda wote hadi alipopoteza pointi mbili muhimu huko Kagera? Au pesa za Yanga ndizo zolizoiua Simba kwa Kagera?

Kumbuka ligi haijafika hata katikati ya msimu.

Vv
 
Simba Ina viongozi Wa ajabu Sana.Kumvumilia Omg wakati Kopovic ali-coach vizuri Sana pale
Klabu zetu hizi zinaongozwa na mihemko na njaa. Usidhani ni Simba tu, huku ng'ambo ya pili nako yale yale. Pluijm alishaipa Yanga standard, alibakiza phase II tuanze kuchapa nje ya mipaka, akazuka wa kuzuka na mihemko yake tukaletewa huyo jamaa mkubwa kama mcheza rugby, imebaki sasa tunacheza mubwa dawa.

Hata hamu na mpira wa Yanga imenitoka.
 
The hammer hizo ni stori za unazi tu, mbona msimu uliopita Simba aliongoza muda wote hadi alipopoteza pointi mbili muhimu huko Kagera? Au pesa za Yanga ndizo zolizoiua Simba kwa Kagera?

Kumbuka ligi haijafika hata katikati ya msimu.

Vv
Labda hujanielewa nilivyosema Yanga angekuwa Na fedha Simba asingechukua kombe.Ni kwamba fedha ingekuwepo Yanga ingesajili zaidi ya hawa tunaowaona,Na hats usajili wao ulisua sua mwanzoni.

Kupoteza point mbili ndilo ninalolisema Na sio mbili tu,ilianza 8,zikapungua hadi tukalingana tukaja kuipita tena hadi point 5 zikapunguzwa Nazo hadi point 2.

Na ninachozungumzia hapa zaidi ni vipaji vya wachezaji vinakufa kwa aina yake ya uchezashaji.Ndo maana nimetolea mifano ya Niyonzima alivyokuwa Yanga Na huyuhuyu tunayemuana Simba.Ajib Wa Simba Na Ajib Wa Yanga.Gyan mfungaji bora no.3 Ghana Na huyu Wa Simba.Mavugo tulivyokuwa tunamsikia Na huyu anayetuonesha maajabu ya mwaka hapa Msimbazi.Je, wote hao walisajiliwa Na hawakuwa wachezaji wazuri? Au Omog mwenyewe ndo mbovu? Timu inacheza Kama wachezaji wanaupungufu Wa madini mwilini.
 
Mkuu hili povu la leo umelitendea haki .chukua fanta kwa mangi ntalipia
 
Klabu zetu hizi zinaongozwa na mihemko na njaa. Usidhani ni Simba tu, huku ng'ambo ya pili nako yale yale. Pluijm alishaipa Yanga standard, alibakiza phase II tuanze kuchapa nje ya mipaka, akazuka wa kuzuka na mihemko yake tukaletewa huyo jamaa mkubwa kama mcheza rugby, imebaki sasa tunacheza mubwa dawa.

Hata hamu na mpira wa Yanga imenitoka.
Mkuu pole sana. Ubingwa wa nne palepale!!
 
Hiyo team ni gari la mkaa, unasajii team nzima mpaka usajili majeruhi alafu unategemea kupata kombe

Tatizo ni viongozi wenu na sio Omog
 
Viongozi wanachagua wachezaji wa kuwasajili na viongozi wanapanga timu halafu lawama anapewa kocha.Asilimia kubwa ya wachezaji waliosajiliwa na Simba hawakupaswa kusajiliwa
 
Klabu zetu hizi zinaongozwa na mihemko na njaa. Usidhani ni Simba tu, huku ng'ambo ya pili nako yale yale. Pluijm alishaipa Yanga standard, alibakiza phase II tuanze kuchapa nje ya mipaka, akazuka wa kuzuka na mihemko yake tukaletewa huyo jamaa mkubwa kama mcheza rugby, imebaki sasa tunacheza mubwa dawa.

Hata hamu na mpira wa Yanga imenitoka.
Yaan hv vilabu ni shida, huwa sielewe sababu ya kutolewa ukocha kwa pluijm, maana timu ilikuwa inaenda vzr na kandanda safi, viongozi nao wakafanya yao nyambafu kabisa
 
Mleta mada umejenga hisia mbaya, ninyi ndio aina ya mashabiki mnaoyumbisha viongozi. Kila msimu ni lazima Simba itimue kocha? Kila tatizo la timu kucheza vibaya litakuwa linatatuliwa kwa kufukuza viongozi? Hivi kwa mfano ni sahihi kusema Yanga inacheza vizuri kuliko Simba? Ni kocha gani ndani ya miaka 5 aliyefikisha Simba ktk kiwango cha Omog? Ajib akiwa Simba alikuwa mchezaji mzuri , na ndio maana akaonekana na Yanga. Amefunga magoli mengi tu ya video.

Timu inaongoza mnapiga kelele hivi kama ingekuwa nafasi kama Real Madrid dhidi ya Barcelona ingekuwaje?
 
Kiwango ni uoni wa mtu (subjective opinion), hakuna namna itayokubalika na wote ya kupima kiwango cha timu. Lakini kuna vigezo kuntu (objective measures) ambavyo kila mmoja analazimika kuvikubali kuhusu uwezo wa timu. Hivyo ni pamoja na nafasi ya timu kwenye msimamo wa ligi kwa kuzingatia kwanza tofauti ya pointi na timu nyengine, idadi ya magoli ya kufunga na kufungwa, n.k. Hebu tumia vigezo hivyo kwa misimu mitatu hii mfululizo uone iwapo timu ya Omog ya msimu huu ndio bora kuliko za misimu miwili iliyotangulia.
 
Ajib hakuweza kuonekana star simba kwa sababu simba ina mafundi wengi na aliposikia okwi anakuja ikabidi asepe, Nyozima alionekana star yanga kwa sababu wachezaji wengi wa yanga ni wa kawaida simba unayosema aina pesa bado ilikuwa inawafunga wakati manji anawamwagia mamilioni
ila nakubaliana na wewe Omog sio kocha mzuri kwa aina ya wachezaji alionao na mpira wanaocheza haviendani
 
Basi kwa nini Simba wakamnunua mchezaji wa kawaida tu (Niyonzima) kwa pesa nyingi zaidi ya wachezaji wote hao wazuri iliyokuwa nao? Ni akili za wapi hizo?
 
mleta uzi nakuunga mkono. ukweli mchungu ambao watu hawaupendi kuusikia ni kuwa simba walipaswa kumfukuza omog na timu wampe mayanja. badala yake wakafanya vice versa. mayanja alikuwa na wachezaji wa kawaida sana lakini simba ilicheza mpira mzuri na timu ilikuwa na stamina. simba ya sasa haina stamina kabisa wanacheza vizuri ndani ya dakika 60 baada ya hapo wanapoteana na usiombe wakutane na timu yenye staminna na nguvu kama prison yaani ni shida. na mbaya zaidi Omog huwa hana plan B timu inapozidiwa na upangaji wake wa timu anaujua yeye mwenyewe. watu wansema mbona inongoza ligi, lakini kiukweli kinachosadia mpaka sasa ni kuwa na kikosi kipana chenye wachezaji wenye uzoefu na uwezo binafsi vinginevyo ingekuwa balaa. kama omog angepewa yanga ya sasa hivi yenye kikosi finyu kutokana na majeruhi angetimuliwa kesho yake.

Na huyu hanspope naye ajulishwe sasa hivi hili dirisha dogo asajili tu mshambuliaji mmoja na kocha mpya huyu omog aachwe aende zake. sio kila ikifika kipindi cha usajili basi anatimua wachezaji zaidi ya nane anasijili wapya. sasa hivi timu imeshaenea kila idara aongeze tu mshambuliaji mmoja anayejua kufunga tu pale mbele basi.
 
Back
Top Bottom