News Alert: Simba SC yaachana na Kocha Mkuu Didier Gomes da Rosa, Thierry Hitimana kuwa kocha kipindi cha mpito

Wakati huu ndg zangu sio wakulaumiana maana yameshatokea chamsingi tukae kupanga timu yetu upya na uzuri zaidi tumeshaelewa tatizo liko wapi.
 
Yanga wamchangamkie kocha huyo
Benchi la ufundi la Yanga limekamilika kila idara! Tuna shida gani sisi mpaka tufikie hatua ya kumchukua kocha wa kukaa jukwaani wakati wa mechi za kimataifa, kutokana na elimu yake ya kuunga unga!!
 
Timu zote duniani zikifanya vibaya anayehusika kutolewa kafara ni kocha,Kocha anaajiriwa ili kuitengeneza timu ipate matokeo mazuri uwanjani, Pryamids walimfukuza kocha aliyepoteza fainali within 24 hour tu ,Giant Al Ahly juzi hapa walitaka kumfukuza Psto........Who is Gomez asifukuzwe yeye ni nani ,Simba ina shida ya kimfumo na makosa ya kimfumo yanaanguka kwa kocha moja kwa moja.
 
Huyu walompa ukocho mkuu binafsi nina mashaka nae ingawa anaweza kuwa na vyeti vya elimu ya kutosha juu ya taaluma yake. Lkn kuwa na cheti na nin unachokifanya kulingana na taaluma yako ni vitu viwili tofauti.

Simuoni kama ni kocha anaweza kuivusha simba na sioni kama ana mbinu zaid za kuisaisia timuz lkn pia sioni kama ni aina ya makocha ambao ana hamasa kwa wachezaji ili kuwahimiza zaidi hasa timu inapokuwa inacheza na ikawa inahitaji matokeo kwa udi na uvumba.

Na hili tuliliona sote wakati wa mechi na wa-Botswana, jamaa alikuwa kasimana tu ni kimya hakuna chochote anachowahimiza wachezaj kufanya hii ilikuwa tofauti na alivyokuwa akifanya kocha wa Wa-Botswana.

Kwa huyu kocha binafsi bado naona pengo.
100%
 
Ila wakati mwingine kukaa kimya ni busara sana kuliko kujianika,fikiri kabla hujajianika
Timu haiwezi kuvuna pesa kama ingeingia makundi na MUDI kapiga hesabu za kocha mkuu Gomez, kocha wa makipa na kocha wa viungo mishahara yao mikubwa na hawezi kuendesha kwa hasara kiasi hicho. Hivyo kaamua kupitia mlango wa nyuma kumtimua Gomez ambae hata kwenye benchi la ufundi kwenye club bingwa hayupo?? Sasa je Gomez kafukuzwa kwa kosa la mechi ipi?? Why asingefukuzwa kocha ambae alisimama kwa sifa za CAF??

MUDI kwaani ukisema ukweli kwamba unapunguza gharama za kuendesha timu kuna nani angekuhoji , umeuza Konde boy na Chama ukaleta Banda na kanoute kwenye michezo ya wanaume ulidhani utavuna nn?? Muogopeni Mungu wenu. Hata Uchebe ulimtoa kihivyo
 
Kocha mkuu huwa anakuja na timu yake, mara nyingi huja na mtaalamu wa viungo, kocha wa makipa, mtaalamu wa saikolojia n.k

Hivyo kocha mkuu akiachia ngazi ni wazi hata jopo lake litaondoka tu...
Pale kila mtu alikuja kivyake.......kumbuka
 
Yeye ni mtunisia na Nabi ni mtunisia huoni ndio alikuwa lango la GSM?

Hukuona wachezaji walikata Moto dakika 45 za mwisho?

Alifeli Sana na ndie alieshauri wachezaji waende kupokea tuzo JKNC
kocha wa viungo ni Mmisri na sio Mtunisia
 
Hakuna chombo chochote cha Serikali kiliwahi kusema Mo kaweka bil 20 Simba, labda Serikali ya huko uliko. Kilichokuwepo ni tume ya ushindani kupitia utaratibu wa uwekezaji wa club ya Simba ili kujiridhisha kuwa taratibu za ushindani zimefuatwa ili baada ya hapo mchakato uendelee.
We piga kelele, ila ndiyo kashatimuliwa. Kocha amepewa pre season ya kutosha kuliko makocha wote Bongo, kacheza zaidi ya mechi kumi, kashinda mbili tu! Tena kwa papatu papatu! Mbaya zaidi timu inacheza hovyo kuliko kipindi chochote ndani ya miaka minne! Yaani kuondoka wachezaji wawili tu, ndiyo amepata wenge?! Hana mbinu za maana, alikuwa anatembelea gia ya kishingo! Atupishe tu!
 
Kwa kauli aliyoitoa ni Mo Dewji baada ya simba kufungwa nilijua tu Gomes hawezi kupona

Nakumbuka kabla hajawa muwekezaji simba alitoa kauli kama hiyo Omog ambaye kwa sasa ni kocha wa Mtibwa Sugar nae akafungasha

Bado Ole Guna Sosha sasa ili niwe na amani ya moyo.

View attachment 1987249
Huu si ushuzi mkubwa.......
kama kumbu kumbu zangu zipo sawa huyu jamaa alifungiwa kwa ukosefu wa vyeti
 
Kocha mkuu huwa anakuja na timu yake, mara nyingi huja na mtaalamu wa viungo, kocha wa makipa, mtaalamu wa saikolojia n.k

Hivyo kocha mkuu akiachia ngazi ni wazi hata jopo lake litaondoka tu...
Adel Zrane aliachwa na Pierre Lechantre.

Gomes Da Rosa hakuja na benchi lake la ufundi
 
Back
Top Bottom