News Alert: Simba SC yaachana na Kocha Mkuu Didier Gomes da Rosa, Thierry Hitimana kuwa kocha kipindi cha mpito

Kocha analipwa mshahara was dollar 15000 wakati Hana vyeti

Halafu pesa ya kumlipa inatoka kwenye mashindano ambayo Kwanza Hana vyeti vya kuyashiriki pili katolewa kipumbavu.

Mo hapa yupo sahihi 100%

Ila tatizo la Simba Ni kubwa wachezaji wamezeeka Sana Sana timu inahitaji kufumuliwa.
Pamoja na kuzeeka kuna wachezaji pale wameshajihakikishia namba ,wanajiona mafaza ,ningekuwa kocha ningeandaa kikosi na wachezaji wapya na wale ambao hawapati namba halafu hao mafaza wanatokea sub hadi akili iwakae
 
Huyu walompa ukocho mkuu binafsi nina mashaka nae ingawa anaweza kuwa na vyeti vya elimu ya kutosha juu ya taaluma yake. Lkn kuwa na cheti na nin unachokifanya kulingana na taaluma yako ni vitu viwili tofauti.

Simuoni kama ni kocha anaweza kuivusha simba na sioni kama ana mbinu zaid za kuisaisia timuz lkn pia sioni kama ni aina ya makocha ambao ana hamasa kwa wachezaji ili kuwahimiza zaidi hasa timu inapokuwa inacheza na ikawa inahitaji matokeo kwa udi na uvumba.

Na hili tuliliona sote wakati wa mechi na wa-Botswana, jamaa alikuwa kasimana tu ni kimya hakuna chochote anachowahimiza wachezaj kufanya hii ilikuwa tofauti na alivyokuwa akifanya kocha wa Wa-Botswana.

Kwa huyu kocha binafsi bado naona pengo.
Mtagongwa tu
 
Usinge sema Bakhressa Hana Kadi au sio mwanachama wa Simba!!..Usinge sema Mo hajaweka 20B kwasababu vyombo vya serikali vyote vinaonyesha ndio Mwekezaji wa Simba!!..Na ungejua sheria zetu za ligi kuu hata za Baraza la Michezo!!.. Lakini wewe unajua kila kitu
We nae tulia uyo bakhressa kawekeza kwenye club ya Azam iyo azam Ina maajabu gani ? Angewekeza simba si ndio angeifanya kibogoyo
 
Huyu bibie CEO mbona yuko nyuma ya pazia tu. Hana contribution yake kwenye muundo wa timu ilivyo kwa sasa...
Nina mashaka na mambo yanayokwenda mbeleni...
Tukamsikiliza Manara at late hours..
 
Back
Top Bottom