Simba SC Vs Azam FC: Mechi imemalizika kwa sare ya mabao Mawili kwa Mawili

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara Vodacom Premier League VPL kuendelea kutimua vumbi leo January 7, 2021 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo Mnyama Mkali Simba SC wanaonyesha kazi na Wana lamba lamba Azam FC.

Mchezo huu wa aina yake utakuwa mkali na burudani ya kutosha ndani ya muda wote wa dakika 90 na kila timu kuhitaji ushindi na kujikusanyia alama tatu muhimu ili kuweza kujimarisha kwenye msimamo wa VPL, pia kutokana na timu zote mbili kusheheni nyota wenye vipaji.

Nani kubaki nafasi ile ile? Simba SC au Azam FC? Kumbuka mtanange huu wa VPL ni kuanzia saa 10: 00 jioni....Usikose Ukasimuliwa

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana


Screenshot_20210207-152035.jpg
Screenshot_20210207-152020.jpg
 
Wachezaji wa kibongo wa tatu tu Simba. Vijana wetu inabidi wajitahidi au hatuzalishi vipaji kama zamani?
 
Simba Mnyama mkali Nyikani. Point 3 Muhimu.

Huyu Zimbwe Jr hajui hata kujieleza tunampaje Kitambaa cha unahodha? Kuongea na Wachezaji kuwapa Moyo na kuwapa maelekezo Muhimu hawezi. Timu inapoonewa hawezi hata Kuongea na Mwamuzi halafu tunampa Unahodha?

Hiii HAPANA, maaana tangu mechi ya Prison Sumbawanga akiwa nahodha alionyesha mapungufu tukaomba Aondolewe ikawa hivyo, lkn anarudishwa tena HOW??? Zimbwe ni Mtoto wa Nani hapo Klabuni?? HANA ELEMENT YOYOTE YA UONGOZI MTUELEWE PLS?
 
5' kwenye mchezo huu wa VPL Simba SC Vs Azam FC Kagereeeee anapiga shutiiiiii
 
8' Majaribio mawili kwa upande wa Simba kuelekea lango la Azam FC

Simba SC 0-0 Azam FC
 
Back
Top Bottom