Simba SC msipokuwa makini na hii 'Mind Game' ya Yanga SC kuwa hawatoleta Timu 03 Julai, 2021 tunaenda kuumbuka kwa kufungwa nao

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,516
108,795
Nauonya Uongozi wa Simba SC na Wanachama mpaka Mashabiki wa Simba SC kuwa tuweni makini mno na hii Mbinu ya Nje ya Kisaikolojia ya Mchezo (Mind Game) inayofanywa na Yanga SC hasa kuelekea Mechi yetu nao tarehe 3 July, 2021 kwani tukienda nayo na tukaiamini na Kuwaamini Yanga SC naona Simba SC tunaenda Kufungwa nao.

Msiamini huu Uwongo wao kuwa sijui hawatoleta Timu au hawatocheza bali Benchi la Ufundi na Uongozi wa Simba SC ijipange vilivyo kuelekea Mechi hii kwani na Simba SC nao ' wakibweteka ' na ' wakiwaamini ' Yanga SC Siku hiyo ya Mechi Mchezo utakuwa Mgumu sana Kwetu na huenda hata Simba SC ikafungwa na akina GENTAMYCINE tukaanza Kuumbuka na Kuchekwa.

Naomba Maandalizi yale yale makubwa tuliyoyafanya Kipindi kile yarejee na ikibidi yaongezwe kwani kwa Hasira ambazo GENTAMYCINE ninazo kwa Yanga SC natamani hivi sasa tuwafunge Yanga SC Magoli hata 11 kwa 0 tofauti na zile Goli 8 kwa 0 ambazo ndizo walikuwa wanaenda Kufungwa Siku ile Mechi ' ilivyoahirishwa ' na Serikali kwa sababu ambazo wanazijua Wao.
 
Back
Top Bottom