Simba SC kuandamana tarehe 25 mwezi huu, Sababu kuu ikitajwa ni uonevu wa TFF dhidi yao.

demigod

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
8,288
15,238
Baada ya siku chache zilizopita kuonekana kwa wasanii wa tasnia ya maigizo wakipaza sauti kutumia maandamano.

Mabingwa wa Ligi Kuu wa Tanzania Bara wa mwaka/msimu 2011/12 leo wamemua kuandaa maandamano ya kudai haki kutoka Shirikisho la mpra wa miguu Tanzania TFF. Uthibiitisho wa Barua hiyo unaonyesha kuwa lengo kuu la maandamano hayo ni kuonyosha kutoridhishwa kwa utendajia kazi wa TFF dhidi ya klabu hiyo kwa madai kuwa imekuwa ikifanyiwa uonevu kwenye masuala mbalimbali ya soka.

Pia sababu kuu ya pili ni kuonyesha kutoridhika kwa kitenda cha msemaji wake Haji Manara kufikishwa katika chombo maalamu cha shirikisho hilo kinachousika na masuala ya nidhamu kwenye soka, ili kujibu mashtaka yanayomkabili kuhusu kurushia maneno makali chombo hiko.

Ikumbukwe kuwa mnamo kuelekea mwishoni mwa mwaka 2016 msemaji wa Yanga SC alifungiwa kwa sababu ya kukisemea chombo hicho maneno machafu.

lolo.jpg
 
Ilikuwa zamu ya Bongo Movie kuandamana, wiki ijayo ni zamu ya simba sc kuandamana. Points za bure za mezani wapewe ,kuonewa ionekane wanaonewa wao!

Au wanataka wapewe ubingwa kabla ligi haijaisha, maana si kwa ukame huo wa miaka zaidi ya 6 bila ndoo ya ligi Kuu.
 
Hawa ndo wanatuharibia soka letu la Tanzania.

Mpira walikuwa wanacheza uwanjani WAKASHINDWA....


wakahamia MEZANI na sasa mpira unaelekea BARABARANI..


Tanzania ikiendelea kuwa na wahuni wa soka wa aina hii ..kombe la dunia tutalisikia kwenye bomba tu.
 
Simba na wasanii wa bongo movie hawana tofauti.....Acha waandamane tu wamekaa kimaigizoigizo si kimchezo
 
laana hiiiiii itawarudia ; kuzungusha mikono; mungu anawazungusha kichwa

upload_2017-4-22_14-5-35.jpeg
 
Back
Top Bottom