Simba SC hamna uwezo wa kugomea mechi kama Yanga SC tulivyofanya

demigod

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
8,250
15,116
Ukubwa wa Simba SC haujai hata kiganjani ukilinganisha na Yanga SC.

Nasema haya nikimaanisha namna ambayo Yanga ilivyo more influencial kuliko Simba.

Kama Simba ikigomea mechi kuna uwezekano mkubwa sana rungu la kukatwa point likàwashukia kwasababu hawana watu makini wa kutafsiri kanuni za soka kama ilivyo kwa Yanga SC.

Ikumbukwe Derby ya mwisho Yanga aligoma kuingiza timu uwanjani kwa madai ya kanuni zimeyumbishwa.

Yanga iliweza kusimamia msimamo wake na hakuna mbuzi iliyojaribu hata kuwakata alama.

Nina waonya Simba SC ole wenu mkubali kupotoshwa na wataalamu wenu wa kutafsiri kanuni waliosoma Diploma za Online.

Uwanja ni lazima yawepo Mabango Makubwa ya Chapa GSM. Mkigoma kuingiza timu tutawafuata huko huko Mo Arena tukipige cha kirafiki.

FGPPQL4XwAgbvT1.jpeg
 
Sheria zinasema Logo iwe katika rangi zake halisi. NBC wakakubali Yanga watumie Photocopied NBC Logo
Na ujinga ulianzia hapa watu wakishindwa kusimamia sheria ndio haya kesho akija Coastal union akasema na mimi nataka rangi yangu akaja mbeya city akasema na mimi rangi hii sitaki.

Real Madrid weupe lakini kuvaa nyeusi, blue wala sio shida mpaka pink wanavaa huku Liver wekundu lakini mpaka njano wanapiga rangi inabaki kwenye logo ya team na identity ya team lakini huwezi kusikia wamegomea brand ya mdhamini.

Ukianza kupindisha sheria basi ujuwe ndio umepotea
 
Yanga ingekuwa ina watu makini wasinge shauri kupeleka kesi ya morison CAS

Yanga ingekuwa na watu makini ingeweka mikakati yao kwenye kuchukua ubingwa na kufuzu kimataifa kuliko kujizatiti kwenye derby

Yanga ingekuwa ina watu makini isinge ruhusu kumuajiri mtu ambaye amewatukana kwa zaidi ya miaka 7

Yanga ingekuwa na watu makini isinge msajili mayele na hata baada ya kumsajili wangeweza kusawazisha makosa yao kwa kumtimua kwenye dirisha dogo

Ni hayo tu
 
Hakuna timu inayotamani kucheza na Yanga kila mara sitoshangaa Simba ikila kona mchezo wa kesho
 
Mnaongea mtu asiyejua kinachoendelea atadhani Kuna ugomvi kati ya Simba na Utopolo kumbe ni Simba na hao magumashi Tff.
 
More influencial kwa kucheza ligi ya mchangani miaka nenda miaka rudi, ujilinganishe na mnyama anaye kwea pipa day in day out
Kwani yanga na simba nani kapanda ndege mara nyingi?(kushiriki mashindano ya kimataifa)
 
Kesho tuonyesha ukubwa wetu..tutagoma na hakuna Cha kutufanya zaidi ya faini ya milioni tatu..
Tapeli GSM ajikite kwa yanga..japo amegundua yanga kimataifa Ni hovyo..anataka kutumia mgongo wetu Simba kujitangaza kimataifa..
Hatutakubali..!
 
Na ujinga ulianzia hapa watu wakishindwa kusimamia sheria ndio haya kesho akija Coastal union akasema na mimi nataka rangi yangu akaja mbeya city akasema na mimi rangi hii sitaki. Real Madrid weupe lakini kuvaa nyeusi, blue wala sio shida mpaka pink wanavaa huku Liver wekundu lakini mpaka njano wanapiga rangi inabaki kwenye logo ya team na identity ya team lakini huwezi kusikia wamegomea brand ya mdhamini. ukianza kupindisha sheria basi ujuwe ndio umepotea
Uhuni kama huo utaukuta Tanzania pekee.
 
Yanga ingekuwa ina watu makini wasinge shauri kupeleka kesi ya morison CAS

Yanga ingekuwa na watu makini ingeweka mikakati yao kwenye kuchukua ubingwa na kufuzu kimataifa kuliko kujizatiti kwenye derby

Yanga ingekuwa ina watu makini isinge ruhusu kumuajiri mtu ambaye amewatukana kwa zaidi ya miaka 7

Yanga ingekuwa na watu makini isinge msajili mayele na hata baada ya kumsajili wangeweza kusawazisha makosa yao kwa kumtimua kwenye dirisha dogo

Ni hayo tu
Yaani timu nzima ya Yanga unamwogopa Mayele tu?
 
Back
Top Bottom