Simba SC 3 - 1 Dodoma Jiji FC | Vodacom Premier League | Benjamin Mkapa

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
21,306
2,000
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara Vodacom Premier League VPL' kuvurumishwa leo Aprili 27, 2021 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo Vinara wa Ligi, Mnyama Mkali Simba SC anapepetana na Dodoma Jiji FC.

Mchezo inatarajiwa kuwa kali na wa kusisimua kwa muda wote wa dakika 90 huku kila timu ikihitaji alama tatu muhimu ili kuweza kujiweka sawa kwenye msimamo wa VPL.

Katika mchezo mzunguko wa kwanza February 4, 2021 Simba SC waliweza kuibuka na ushindi wa mabao mawili kwa moja

Je Mnyama Mkali Simba ataendeleza ushindi na kuendelea kuwa juu zaidi? Au Dodoma Jiji FC wataweza kuisimamisha Simba SC kwenye wimbi lake la ushindi?

Kumbuka mtanange huu ni kuanzia saa 1:00 Usiku. Gumzo Hapo Ndipo.

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana.


=========

Wakati wowote mpira utaanza uwanja wa Mkapa.

00' Naaaam mpira umeanza ni vita vya VPL Simba SC dhidi ya Dodoma Jiji.

08' Mugalu Goooooooooooooooooooooal

Kope Mutshimba Mugalu anaipatia Simba SC bao la kwanza akipokea pasi safi kutoka kwa Bwalya

Simba SC 1-0 Dodoma Jiji FC

Baada ya kushambulia Dodoma Jiji walipoteza mpira na wakawahi Simba na kuwa katika miliki yao.

Mkandala anaonyeshwa Kadi ya Njano baada ya kumfanyia faulo Miquissone.

20' Simba SC 1-0 Dodoma Jiji FC

Inapigwa kuelekea Simba SC golikipa Manula anadaka na anatema mpira

29' Goooooooooooooooooooooal

Dodoma Jiji FC wanasawazisha kupitia kwa Mkandala

Simba SC 1-1 Dodoma Jiji FC

Kwa wakati huu mpira una mashambulizi kwa pande zote mbili, lakini mabeki wanakuwa makini

Mzamir anapoteza nafasi bomba ya kufunga, ilikuwa Hatari sana lango la Dodoma Jiji FC

45+2' Kuelekea kuwa mapumziko uwanja wa Mkapa.

Naaaam mpira ni mapumziko ambapo Timu zinatoka kwa kufungana bao moja kwa moja

HT, VPL; Simba SC 1-1 Dodoma Jiji FC

Kipindi cha pili kimeanza uwanja wa Mkapa, huku Simba wakijaribu kwa kupenya ngome ya Dodoma Jiji.

51' Ametoka Mzamir na nafasi yake imechukuliwa na Morrison, upande wa Simba SC

55' Miquissone Goooooooooooooooooooooal

Luis Miquissone anaipatia Simba SC bao la pili akipokea pasi safi kutoka kwa Chama

Simba SC 2-1 Dodoma Jiji FC


60' Ametoka Mtegeta na ameingia Mapunda upande wa Dodoma Jiji FC

Mugalu Goooooooooooooooooooooal Gooooal

Kope Mutshimba Mugalu anaipatia Simba bao la tatu kwa kazi nzuri ya Chama

Simba SC 3-1 Dodoma Jiji FC


71' Ametoka Miquissone na ameingia Ajibu upande wa Simba SC

81'' Dodoma Jiji wanafanya mabadiliko, ametoka Mganga na ameingia Nkosi huku Simba SC wakimtoa Mugalu na ameingia Kagere.

90+3' Kuelekea kumalizika kwa mchezo wa VPL

Naaaam mpira umekwishaaa ambapo Simba SC wameibuka na ushindi wa mabao matatu kwa moja dhidi ya Dodoma Jiji FC

FT, VPL: Simba SC 3 - 1 Dodoma Jiji FC

Ghazwat
 

Donnie Charlie

JF-Expert Member
Sep 16, 2009
10,187
2,000
20210427_174500.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom