Simba SC 3-0 JKT Tanzania FC | Uwanja wa Benjamin Mkapa | Vodacom Premier League VPL

Wachezaji wa Simba washakubaliana hata wakipata Penati wanaipiga nje ya Lango, hivyo usiulize magoli ya penati.
1614624414401.png
 
Hapo kapombe anacheza Kama wiga wa kulia yaani 7 alafu Kennedy anacheza beki wa kulia no 2 kisha Nyoni na Wawa wanacheza katikati kama ma central defenders ndio maana unamuona chikwende na Bwalya wako nje.

Kuna muda anaweza kutoka Kennedy kisha kapombe akarudi no 2 alafu akaingia Chikwende kwanda kucheza wiga wa kulia au akaingia Bwalya kisha akaenda kucheza kushoto alafu Konde Boy akaja kucheza upande wa kulia.

Huyu kocha ni mjanja sana huyu.
Mkuu Simba ilicheza na back three, yaani

Wawa. Kennedy. Nyoni

Kapombe. Lwanga. Mzamiru. Zimbwe

Miquesson. Chama

Mugalu

Ila inaposhambulia Nyoni alikua anaongezeka ndani anacheza na Lwanga ,kisha mzamiru anasogea juu zaidi kuwa connect ya Mugalu ,Chama na luis

Wakati huo pale nyuma anabaki Wawa na Kennedy.Kennedy jana alikua kama stopper ndamana uliona jana Kennedy aliinjoi sana maana kazi zote zilifanywa na Nyoni na Wawa yeye alikua anaokota tu anapiga kulia anapiga kushoto.

Kapombe na zimbwe walikua ma wingbacks wakianzia kwenye mstari wa kati kati ya uwanja.
 
Back
Top Bottom