Simba sasa ndo wanagundua kuwa Marefa wasio na beji za Fifa wabovu..

Anselm

JF-Expert Member
Nov 16, 2010
1,710
291
Baada ya kutoa droo mechi 3 mfululizo,team ya Simba sasa imekuja na kali nyingine baada ya kuitaka TFF kuwapangia kwenye mechi zao marefa wenye beji za FIFA kwa madai kuwa wale wasio na beji hawana viwango vya kuchezesha mechi zao, cha kushangaza type hiihii ya waamuzi(hawa wasio na beji za FIFA) ndo ambayo imekuwa ikichezesha mechi zao kuanzia zile zilizokuwa zinapigwa Uwanja wa Taifa ambapo Simba alikuwa akiibuka na ushindi huku kila mechi Simba akifaidi nafasi ya kupungua kwa mchezaji/wachezaji wa wapinzani wao na wakati mwingine ushindi wao ukichagizwa na penalt tata...jamani ndo maana soka letu halikui,siku zote team ikipata matokeo mazuri hata kama referee aliboronga kweli hawalamlamiki ngoja sasa wavune matokeo mabaya shutuma zisizo na vichwa wala miguu zitaibuka,haya droo ya 3 tu kelele kibao,hadi Kocha katukana(halafu yule Mzungu naye sijui wa Serbia ipi?!!!)...jamani soka ina matokeo ma'3 kushinda/kushindwa/kutoka sare tujifunze kukubaliana nayo.
 
Back
Top Bottom