Simba na Yanga waigeni Barcelona na Real Madrid katika mapato

Mars 12

JF-Expert Member
Feb 25, 2021
221
349
Hapa nchini timu mbili tu ndizo zinazowapa jeuri Azam tv,TFF. Yaani Simba fc na Young Africans (Yanga). Kwa kuwa viongozi wa timu hizi mbili wanachaguliwa na wanachama ni sawa na Barcelona na Real Madrid.

Sasa ushauri kwangu kama ilivyo Hispania,viongozi wa timu mbili hizi wadai kuwa na mikataba minono tofauti na timu nyingine. Walipwe zaidi, kama wanalipwa milioni 500 basi iwe bilioni moja na nusu.

Ukweli kama La Liga ya Hispania,bila Simba na Yanga hakuna ushabiki nchini. Hivyo Azam tv wanatudandanya kwa kuingiza mabilioni ya pesa kupitia migongo ya Simba na Yanga.

Ni wachache mno wataonunua vingamuzi (decorder) za Azam kama hawapo Simba na Yanga. TFF nayo inategemea timu hizi mbili.

Ni wakati muafaka kwa viongozi wa Simba na Yanga kuamka na kudai halali yao. Pia wanaweza kujitoa katika mkataba wa Azam na TFF nawakatengeneza vingamuzi vyao.Vitanunuliwa kama njugu tena nao watauza na kuwa na haki miliki.

Dewji,GSM,viongozi wa Simba na Yanga amkeni. Nowadays football is golden business.
 
Au kama vipi tugomee tu..mechi zetu kuonyeshwa na azam TV.. mwananchi
 
Au kama vipi tugomee tu..mechi zetu kuonyeshwa na azam TV.. mwananchi

Tungekuwa na chanel zetu independent kama Mutv,Lfctv n.k kwenye ving'amuzi vya zuku,dstv,startimes n.k tungeweza kugomea
ila tumejitajidi kuwa na Simba tv na Yanga tv ndani ya king'amuzi cha azam tv tena coverage yake kwa wiki ni mara moja tu utagomea vipi mzee?
 
Manji alikuwa na mawazo hayo, lakini timu hizi mbili zina jukumu la kujenga timu nyingine za mikoani. Hapo ndiyo tunapokwama.
Na kila siku unasikia watu wasiojua historia ya mpira wa miguu hapa Tanzania kuwa timu hizi zinaharibu mpira wa nchi hii.
 
Back
Top Bottom