Simba na Yanga ni uchawi unaotumiwa kupumbaza akili za vijana Watanzania

Miaka ya 1960s ushabiki wa mpira haukuwa na nguvu sana ndio maana ata uhuru ulipatikana kwa urahisi maana watu wengi walijihusisha na tatizo moja tu...mkoloni.

Leo hii mtu ana arsenal kichwani,simba,yanga nk.ukimuambia katiba mpya inatakiwa hakuelewi...tumerudi nyuma saana
 
Kama sasa hivi Simba tunachangamoto ya number 10, Bwalya bado haja adapt vizuri na Kibu Denis ana papara tungepata mtu dizaini ya Chama au tukizidi kumuamini Sakho tunaweza kufika mbali.

Kiufupi Mwl Pablo aelewe timu yake vizuri na kutuletea defensive midfielder mkata umeme mzuri wa kusaidiana na Mkude. Tutakua wa moto sana katika ligi na mashindano ya Kimataifa
Ukiwa kiongozi kwenye taifa lenye changamoto lukuki then vijana wenyewe mawazo yao ndio kama haya yaani utaongoza kwa raha sana yaani!!
 
Msipende kumsingizia kila kitu Magufuli. Why mpaka leo mnaishi kwa kivuli chake wakati mtu ameshajifia zake. Watu wameacha kujadili siasa baada ya kuona ni ulaghai mtupu.

Unakuta mwanasiasa wa upinzani anaipinga Serikali kila siku, lakini akipewa nafasi yeye hata ya ubunge tu, hakuna lolote analolifanya zaidi ya kujineemesha yeye na familia yake. Wengine tumewaona wamepata nafasi za kisiasa wanaweka ndugu na mahawara wao huku wananchi wakiendelea na shida zao. Ndo maana watu wameona ni bora wajadili vitu vinavyowapa furaha kama mpira kwasabbu wanasiasa siyo wakweli bali ni wachumia tumbo tu.
Jiwe ndiye alileta hii shida, acha kurukaruka kama headless chicken
 
Mleta mada hauko serious humu Jamii forums kuna majukwaa mbali mbali .
Hili ni jukwaa la kisports unataka watu wajadili siasa huoni kuwa hata hizo siasa huna unachokifahamu?

Nenda kaangalie dhima ya kila jukwaa ndipo uwe na hoja au ukose hoja ya kulaumu .
 
Upo sahihi Sana na ndio maana hata umeme ukatike vipi lakini siku ya mechi ya Simba na Yanga utakuta karibia sehemu yote ya nchi upo siku hiyo coz wanajua watawafumbua macho kujua umuhimu wa umeme. Ila siku nyingine hata mtu mwenye kiwanda chake umeme ukikatika Walaa husikii kelele za kutosha kama siku ya Simba na yanga
 
Back
Top Bottom