AMARIDONG
JF-Expert Member
- Jun 24, 2010
- 2,501
- 183
VIGOGO wa soka hapa nchini Simba na Yanga za jijini Dar es Salaam leo zinatarajiwa kuanza kujinoa kwa ajili ya kukabili mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara unaoanza kutimua vumbi Januari 15 mwakani.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam, maofisa habari wa klabu hizo walithibitisha timu zao kuanza programu za mazoezi leo kwa kuanzia na gym.
Ofisa Habari wa mabingwa watetezi Simba, Clifford Mario Ndimbo, alisema, mazoezi yatakayoanza leo yatakuwa chini ya kocha msaidizi Amri Said Jap Stam, huku akisubiriwa kocha mkuu, Mzambia Patrick Phiri.
Kwa upande wake, Ofisa Habari wa Yanga Louis Sendeu, alisema, pia nao wataanza na gym chini ya kocha mkuu, Mserbia Kostadin Papic huku wakiwasubiri nyota wao walioko timu za taifa za bara na visiwani ambao wanashiriki michuano ya Chalenji inayoendelea jijini Dar es Salaam.
Klabu hizo zimeimarisha vikosi vyao wakati wa dirisha dogo kwa kusajili nyota wawili kila moja, ambapo Simba imemnyakua mshambuliaji Ali Ahmed Shiboli kutoka KMKM ya Zanzibar na kumrejesha kundini beki wake Meshack Abel aliyekuwa kwa mkopo African Lyon huku Yanga ikimtwaa Davies Mwape na Juma Seif Kijiko kutoka JKT Ruvu ya Pwani.