Simba na Yanga ndio chanzo cha kuzorota kwa soka Tanzania??


Sajenti

Sajenti

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2008
Messages
3,671
Likes
36
Points
0
Sajenti

Sajenti

JF-Expert Member
Joined Apr 24, 2008
3,671 36 0
Nimekuwa nikifatilia kwa karibu mwenendo wa soka latu hapa Tz, kwa muda mrefu nimekuwa nikiona kabisa (kwa mtazamo wangu) kuwa hizi timu mbili za Simba na Yanga huenda zinachangia sana kudidimia kwa mchezo huo. Nasema hivyo kwa nini? Nguvu nyingi katika uwekezaji katika soka kwenye ngazi ya club zaidi kufanyika katika timu hizi mbili. Nakumbuka mwaka jana tu TBL walitoa udhamini kwa Simba na Yanga na kuzipatia mabasi madogo mawili kila timu. Juzi TBL walitoa vifaa vya michezo kwa timu hizi eti ikiwa ni maandalizi ya mzunguko wa pili wa ligi. Najiuliza hivi hawa wadhamini/wafadhili hawawezi kwenda kuwekeza kwenye timu nyingine tofauti na Simba au Yanga? Huko mikoani kuna timu zenye wachezaji wazuri sana lakini nyingi hufikia kufutika ramani ya soka Tz kwa kukosa uwezo. TFF kama vinara wa soka nchini hebu jaribuni kuwashauri hao wafadhili basi wabadirike basi na kufadhili na timu nyingine ili kuweza ku-balance rasilimali na hatimaye kukuza soka letu......
 
Sipo

Sipo

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2008
Messages
2,146
Likes
41
Points
0
Sipo

Sipo

JF-Expert Member
Joined Jul 25, 2008
2,146 41 0
Wafadhili wanaangalia sana ni wapi pa kutangazia biashara yao kwenye nchi husika ndio maana wanaenda Simba na Yanga. Nina uhakika hawawezi kwenda kwenye klabu za chini wakati wanajua washabiki wanaokwenda kutazama timu hizo ni sawa na hakuna.

Ila pointi yako ya hizi timu kubwa kuua soka nchini ipo na ni ya msingi ila inahitaji hoja zaidi kwenye nyanja nyingine zaidi ya hiyo ya ufadhili
 
Sajenti

Sajenti

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2008
Messages
3,671
Likes
36
Points
0
Sajenti

Sajenti

JF-Expert Member
Joined Apr 24, 2008
3,671 36 0
Sipo,
unachosema na kubaliana na wewe kuwe wa wafadhili wako kibiashara zaidi na ndio maana nikadhani hawa TFF watafute mechanism itakayoweza kuwabana hao wanaiotwa wafadhili ili kupanua wigo wa ufadhili wao. Ukiangalia nchi kama uingereza udhamini kwa timu za Premier league haujalenga eti Man Utd, Chelsea, Liverpool au Arsenal tu. Hata timu zilizoko kwenye madaraja ya chini wanapata udhamini na ndio maana hata kiwango cha timu za madaraja ya chini zinapiga soka nzuri. Kwa kufanya hivyo, hata hizi za chini zitanyuka na hatimaye kupanda kimataifa na hatimaye kutangaza hizo biashara. Umesikia kenya timu ya Mathare United jana imepata ufadhili wa $ 200,000 lazima itaongeza hamasa huku sio kung'ang'ani matimu haya makubwa tu.
 
Sipo

Sipo

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2008
Messages
2,146
Likes
41
Points
0
Sipo

Sipo

JF-Expert Member
Joined Jul 25, 2008
2,146 41 0
Mkuu Laligeni
Umekuja na hoja nzito na yenye mifano ya UK na Kenya. Ni kweli kuwa tunahitaji kubadilika ila hili inabidi lianzie kwa viongozi wa klabu hizi wenyewe manake TFF wakichukua jukumu hili hiyo sapoti haitadumu kama wenyewe wenye timu hawafeel kuona timu yao inasonga mbele
 
leseiyo

leseiyo

Senior Member
Joined
Oct 25, 2007
Messages
116
Likes
1
Points
0
leseiyo

leseiyo

Senior Member
Joined Oct 25, 2007
116 1 0
Ni kweli,msingi wa soka la Taifa lolote uko kwenye vilabu.Huko tunategemea uleaji wa vipaji vya watoto,ambao watakuzwa kwenye nidhamu ya soka hadi kufika hatua ya kuliwakilisha taifa.Lakini ukizicheki Simba na Yanga haya huyapati, hata viongozi wenyewe unakuta hawana visheni ya kukuza soka.
 
Sipo

Sipo

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2008
Messages
2,146
Likes
41
Points
0
Sipo

Sipo

JF-Expert Member
Joined Jul 25, 2008
2,146 41 0
Ndugu Leseiyo
Msingi wa soka la nchi yeyote ni klabu na sio timu ya taifa na ndio maana sisi tumeelemea zaidi kuwalaumu makocha wa national timu lakini hatuangalii mfumo wetu. Sasa tatizo la soka la vilabu vyetu manthalani Simba na Yanga ni kuwa wao wanataka kutengeneza pesa kupitia wachezaji ambao hawahangaiki kuwapika na kuwakuza. Jiulize maswali kwanini kuna friends of Ynaga na Simba na sio friends of Majimaji au Ashanti wale pale wako kwa maslahi binafsi kama sio ya kibiashara basi ya kisiasa na ndio maana wanataka soka la vilabu hivyo liendelee kuwategemea wao tu na sio vilabu visimame vyenyewe
 
leseiyo

leseiyo

Senior Member
Joined
Oct 25, 2007
Messages
116
Likes
1
Points
0
leseiyo

leseiyo

Senior Member
Joined Oct 25, 2007
116 1 0
Ndugu Leseiyo
Msingi wa soka la nchi yeyote ni klabu na sio timu ya taifa na ndio maana sisi tumeelemea zaidi kuwalaumu makocha wa national timu lakini hatuangalii mfumo wetu. Sasa tatizo la soka la vilabu vyetu manthalani Simba na Yanga ni kuwa wao wanataka kutengeneza pesa kupitia wachezaji ambao hawahangaiki kuwapika na kuwakuza. Jiulize maswali kwanini kuna friends of Ynaga na Simba na sio friends of Majimaji au Ashanti wale pale wako kwa maslahi binafsi kama sio ya kibiashara basi ya kisiasa na ndio maana wanataka soka la vilabu hivyo liendelee kuwategemea wao tu na sio vilabu visimame vyenyewe
Mzee heshima juu.naona hujanisoma vizuri.Nimesema kwamba msingi wa soka uko kwenye vilabu,huko ndiko tunategemea malezi ya watoto kisoka hadi kufikia level ya kung,aa kwaenye ligi zetu na hatimaye timu ya Taifa.Simba na Yanga ni kama vijiwe vya kunywea kahawa na vijana kwenda kujifunza kuvuta bangi tu.Waone wachezaji afya zao pia macho yalivyo mekundu.
 
Shedafa

Shedafa

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2008
Messages
802
Likes
26
Points
35
Shedafa

Shedafa

JF-Expert Member
Joined May 21, 2008
802 26 35
Nakubaliana nawe kuwa hivi vilabu viwili vya SIMBA na YANGA ni kikwazo kikubwa cha kukua kwa mpira hapa nchini, ila si sababu ya wafadhili. Wafadhili kama wafadhili wanawekeza wanapoona watapata faida na wala si hisani. Ila kuna sababu nyingi baadhi ni hizi

1. Hawajui kutunza wachezaji. Tazama wachezaji wengi waliotoka na kwenda kucheza nje ya nchi bado wanacheza, wakati wale waliowaacha katika hizi timu tayari wamekuwa ni historia.

2. Hazipendi kufungwa, kama ikitokea timu ikazifunga msimu huu ujue msimu ujao watawachukulia wachezaji wao wote.

3. Zinalazimisha ushindi hata wa kununua, hii inazifanya timu zinazofanya bidii zikate tamaa.

4. Hawana program nzuri za mazoezi. Muda mwingi utakuta wachezaji wao wapo kwenye anasa tu na kujiona wao ni mastaa, kitu kinachofanya hata wachezaji wapya wasione umuhimu wa mazoezi.

5. Hawatoi mchango wowote wa kuendeleza soka la vijana, kama kuwa na timu za watoto. Wakati wao wanamtiririko mzuri tu wa mapato. Wao kazi yao ni kuanagalia timu gani ina mchezaji mzuri wakamchukue.

Sababu ziko nyingi, mawazo yangu ni kuwa ingekuwa vyema zingepata matajiri wakazinunua. Ingesaidiwa kuwa na mipango ya maendeleo, au zife kama zilivyokufa Abaluya na Gor.
 
Sipo

Sipo

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2008
Messages
2,146
Likes
41
Points
0
Sipo

Sipo

JF-Expert Member
Joined Jul 25, 2008
2,146 41 0
Mzee heshima juu.naona hujanisoma vizuri.Nimesema kwamba msingi wa soka uko kwenye vilabu,huko ndiko tunategemea malezi ya watoto kisoka hadi kufikia level ya kung,aa kwaenye ligi zetu na hatimaye timu ya Taifa.Simba na Yanga ni kama vijiwe vya kunywea kahawa na vijana kwenda kujifunza kuvuta bangi tu.Waone wachezaji afya zao pia macho yalivyo mekundu.
Mimi naamini nimekuelewa na niko upande wako kuwa kwa Tanzania bado vilabu havijajua kuwa ndio vimebeba hatima ya mpira wote ikiwa ni pamoja na national team. Ndio maana mimi binafsi uwa nawashangaa viongozi wa vilabu wanapokuwa wa kwanza kumlaumu kocha wa timu ya taifa wakati wao ndio wana mfumo mbaya kwenye vilabu vyao
 
K

Konaball

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2009
Messages
2,451
Likes
1,016
Points
280
K

Konaball

JF-Expert Member
Joined Mar 11, 2009
2,451 1,016 280
Oyaa nyie wote mliochangia hapo juu niambieni mnashabikia au wanachama wa timu hapo BONGO kama sio SIMBA na YANGA
 
Sipo

Sipo

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2008
Messages
2,146
Likes
41
Points
0
Sipo

Sipo

JF-Expert Member
Joined Jul 25, 2008
2,146 41 0
Oyaa nyie wote mliochangia hapo juu niambieni mnashabikia au wanachama wa timu hapo BONGO kama sio SIMBA na YANGA
Haijalishi hata kama tu washabiki wa timu hizi lakini tuko huru kuzungumza ukweli pale panapobidi
 

Forum statistics

Threads 1,250,865
Members 481,514
Posts 29,748,687