Simba na Yanga mara 81 kwenye ligi, nani atasherehekea Jumamosi hii?

Daniel Mbega

JF-Expert Member
Mar 20, 2013
338
180
SIMBA-V-YANGA-8.gif

UMAMOSI hii Februari 20, 2016 bingwa wa ‘kucheka na nyavu’ wa miaka yote Uingereza, James Peter ‘Jimmy’ Greaves, atakuwa anasherehekea miaka 76 ya kuzaliwa kwake, lakini kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kutakuwa na habari nyingine wakati mahasimu wakuu wa soka Tanzania, Yanga na Simba watakapokuwa wakivaana kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Timu hizo zinapambana katika siku ya 51 ya mwaka, lakini ni baada ya siku 112 tangu zilipopambana mara ya mwisho – katika mchezo wa kwanza wa msimu wa 2015/2016 – Septemba 26, 2015 kwenye uwanja huo huo na Yanga wakaibuka washindi kwa mabao 2-0 wakilipa kisasi cha kufungwa ‘bao la kizembe’ na pekee Machi 8, mwaka huo lililopachikwa kimiani na Emmanuel Okwi.

Achana na akina Alan Shearer, Wayne Rooney na Thierry Henry, mkongwe Greaves aliyechezea Chelsea, AC Milan, Tottenham na West Ham, ndiye mchezaji pekee aliyefunga mabao mengi zaidi kwenye ligi ya juu (top flight) wakati huo ikiwa Ligi Daraja la Kwanza, ambapo alipachika wavuni mabao 357 dhidi ya 260 ya Shearer.
ZAIDI INGIA HAPA...
 
Back
Top Bottom