Simba na TFF msimchezeshe Kibu Denis mechi za kimataifa kuepuka kujutia

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,233
12,508
Uraia alionao na tuliompa after the fact unaweza kupingwa kwenye mahakama za juu za mpira kama timu iliyofungwa na Simba au taifa stars ilimchezesha Kibu Denis kwenye mechi zake.

Kibu alisajiliwa na Simba kama raia wa Tanzania na kucheza mechi za ndani na nje ya Nchi kama raia wa tz wakati hakuwa raia.

Kibu, TFF na Simba walipaswa kuadhibiwa kwa kosa hili badala ya wao kumuombea uraia uhamiaji na hatimaye kupewa uraia wa fasta after the fact.

Kuna wakati inaweza kutolea timu zilizofungwa na Simba kwenye mechi za CAF champions na FIFA kutafuta pa kutolea. Yaaani watamkatia rufaa Denis na kupewa point tatu.

Kwanini tufike huko?⁵
 
Hili nalo ni neno, hasa kama hana hati ya kuukana uraia wake wa zamani, inaweza kuwa silaha ya kuchukuliwa Point 3 za mchezo ambao kachezeshwa na tukashinda

Kim Poulsen asijifanye kwamba huyo mchezaji ndo wa muhimu sana na hawa wapinzani wetu waka wanatuchora tufanye wrong step
 
Hii issue imeamuliwa kishabiki sana, itakuwa mtego kwa simba na stars
 
Kabla ya hapo alisajiliwa kama raia wa wapi?
Na baada ya hapo akatambulika kama raia wa wapi?
 
Uraia alionao na tuliompa after the fact unaweza kupingwa kwenye mahakama za juu za mpira kama timu iliyofungwa na Simba au taifa stars ilimchezesha Kibu Denis kwenye mechi zake...
Kwenye mashindano ya vilabu ya CAF, hawaulizani URAIA wa mchezaji mkuu.

Wanachouliza ni mchezaji awe amesajiliwa na klabu husika kwenye mashindano ya kimataifa basi. Tena siku hizi sio lazima wachezaji wote wawe wamesajiliwa kucheza ligi za ndani ili waweze kucheza mechi za CAF.

Utata wa Kibu ilikua ni je, atachezaje mechi za ndani endapo sio mtanzania na wakati tayari Simba ina wasio watanzania 12 (upper limit).
 
Kabila gani mkuu? Baba yake na mama yake wako wapi, babu na bibi zake, ndugu zake wengine wako wapi.
Kuna haja ya kukurudisha darasani mkuu ufundishwe tena aina za uraia.

Hayo unayotaka kuyajua happ juu ni matakwa ya uraia wa kuzaliwa.

Kibu sio raia kwa kuzaliwa. Sasa sijui hayo mambo ya kabila lake, wazazi n.k yanakujaje hapa.

NB: Raia yeyote (bila kujali uraia wake ni wa aina gani) anapata haki zote za "Raia wa Tanzania"

"Sisi" wahaya, wanyakyusa, wagogo, wazaramo, n.k tusijejiona kwamba eti sisi ni watanzania maradufu kuliko Kibu.
Hakuna kitu kama hicho.
 
Uraia alionao na tuliompa after the fact unaweza kupingwa kwenye mahakama za juu za mpira kama timu iliyofungwa na Simba au taifa stars ilimchezesha Kibu Denis kwenye mechi zake...
Bro your not reasoning properly. Kama Kibu tayari ameshakuwa cleared kuwa ni raia wa Tanzania hata akitumika na Simba kwenye CL haiwezi kuleta misunderstanding mwasababu tayari kula legal basis zimeshakuwa established kuwa ni raia.

Pili kama ingekuwa alishatumika kabla, na kama sheria ya idadi ya wachezaji wa kigeni ikawa ilikuwa imevunjwa basi klabu ingeweza kuingia matatizoni lakini kama hakutumika na sasa tayari ameshakuwa cleared na mamlaka za nchi ina maana ana passport ya TZ halali kabisa na Simba wanaweza kumtumia kama mchezaji mtanzania muda wowote wanaotaka.

Usitishe watu. Sheria watu tunajua.
 
Bro your not reasoning properly. Kama Kibu tayari ameshakuwa cleared kuwa ni raia wa Tanzania hata akitumika na Simba kwenye CL haiwezi kuleta misunderstanding mwasababu tayari kula legal basis zimeshakuwa established kuwa ni raia...
Tujibu hoja amepewa uraia wa Tanzania au wamedeclar ni raia wa Tanzania?
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom