Simba mrejesheni dimbani Jonas Mkude

Mimi ni shabiki kindakindaki wa Simba binafsi toka huyu jamaa awe nje ya uwanja pengo lake linaoneka na hata baada ya kusajili Thadey Lwanga. Namshauri kocha wangu wa simba amrejeshe dimbani shujaa wetu jonas mwana mkude.

Naomba kuwasilisha
Kuna mtu alisema Nguruwe usipomjua kwa sauti basi harufu itakujulisha huyu ni Nguruwe.
 
Mimi ni shabiki kindakindaki wa Simba binafsi toka huyu jamaa awe nje ya uwanja pengo lake linaoneka na hata baada ya kusajili Thadey Lwanga. Namshauri kocha wangu wa simba amrejeshe dimbani shujaa wetu jonas mwana mkude.

Naomba kuwasilisha

Hakuna mchezaji alie juu ya Club, next time ajaribu kuwa na nidhamu.

Natamani asichezeshwe mpaka mkataba wake utapofikia mwisho
 
Mimi ni shabiki kindakindaki wa Simba binafsi toka huyu jamaa awe nje ya uwanja pengo lake linaoneka na hata baada ya kusajili Thadey Lwanga. Namshauri kocha wangu wa simba amrejeshe dimbani shujaa wetu jonas mwana mkude.

Naomba kuwasilisha
Ameshaacha kupenda Kuvuta Bange, Kuwakuwadia Wenzake Mademu Mastaa Bongo na Kunywa Pombe hadi hajitambui?
 
Mimi ni shabiki kindakindaki wa Simba binafsi toka huyu jamaa awe nje ya uwanja pengo lake linaoneka na hata baada ya kusajili Thadey Lwanga. Namshauri kocha wangu wa simba amrejeshe dimbani shujaa wetu jonas mwana mkude.

Naomba kuwasilisha
Wewe badala ya kuuliza Simba na yanga wanacheza lini,unamtaka mkude?
Simba kashinda mechi mbili kibabe bila ya mkude,unatakiwa umpe moyo mchezaji wako
 
Mkude ajilaumu mwenyewe. Alichezea kazi yake kwa kuleta nyodo muda mrefu sana viongozi wakamletea Kotei wapambane akammudu. Akaletwa Fraga akapata majeraha. Sasa hapo kwa mwamba Lwanga viongozi ndio wamemkata nyodo zote kabakia na watetezi wachache mitandaoni. Vile vitisho vyake kila wakati eti anaenda Yanga avilete sasa hivi tena kama viongozi hawatampeleka Yanga bure kabisa. Na mbaya zaidi Fraga anaendelea vizuri na matibabu huko Brazil huku Doxa Djikanji yupo hapo Kongo anapiga jaramba na anataka namba dirisha kubwa la usajili litakapofunguliwa juni/julai mwaka huu. Muzamiru naye gari limeshawaka na mapafu nyake ya mbwa akijirekebisha tu kidogo kwenye kutoa pasi basi Mkude atakuwa na hali ngumu zaidi. Na hivi Mkude hajacheza muda mrefu itamchukua muda kiasi kurudisha kujiamini kwake kama mwanzo. Na mchezaji anajenga kujiamini pale anapocheza mara kwa mara kitu ambacho ni kigumu sana sasa hivi kucheza mara kwa mara kwa timu yenye kikosi kipana kama Simba.

Yote kwa yote Mkude alikuwa na mapungufu makubwa ; kukaba kwa macho, "square pass"" kwa mabeki wake wa pembeni muda wote wa mchezo badala ya kupeleka mpira mbele kwa haraka, faulo za kijinga akizidiwa, kuangalia chini muda mwingi anapokuwa na mpira badala ya kuinua macho ili apige pasi za mbali, kushindwa kucheza mipira ya 50/50 na viungo wa timu pinzani (hafiki maungoni kama anavyofika mwenzake Lwanga) na uwezo mdogo wa kunusa hatari pindi Simba inaposhambuliwa. Sasa hivi Wawa na Onyango wanaonekana uwezo wao halisi baada ya kuwa Lwanga anawalinda jinsi inavyotakiwa. Lakini kipindi Wawa na Onyango wakicheza na Mkude kila mtu alimuona Wawa kaisha na kazeeka. Lakini Mwangalie Wawa wa sasa hivi chini ya Lwanga kwenye mechi za As Vita na Alhaly utaona tofauti kubwa sana na Onyango ndio kawa bora kabisa. Makosa ya Mkude yalikuwa hayonekani kwa urahisi kwa sababu alikuwa anafanyia katikati ya uwanja matokeo yake lawama zilikuwa zinaenda kwa watu wa mwisho Wawa na Onyango.

Kwa nidhamu yake mbaya iliyopitiliza ilifika mahali mpaka wachezaji wenzake walimgomea asirejee kambini kwani atawavuruga. Kwa hali hiyo Mkude inabidi abadilishe mienendo yake nje na ndani ya uwanja vinginevyo inaweza kuwa ndio mwisho wa kucheza timu kubwa kwani sasa hivi hata akienda Yanga atakutana na mafundi Fei Toto na Mukoko kwa hiyo itabidi asubiri benchi kwanza mpaka mmoja wao aumie au awe na kadi.

Kwa ufupi Mkude amejipa kazi kubwa sana ambayo itambidi apambane hasa ili kurudi kwenye "first eleven"" na ni lazima akubali kubadilika na kujifunza kwa Lwanga namna ya kukaba na kikubwa zaidi ajifunze nidhamu kwa sababu nidhamu ndio mwanzo wa mafanikio yoyote yale mahali popote pale.
 
umeona kama mimi, moja ya sababu kubwa beki ya simba kuonekana uchochoro ni uwezo mdogo wa Mkude lakini bahati nzuri kwake alikuwa na watetezi wengi kiasi akajisahau lakini tangia asimamishwe badala ya Simba kuonekana dhaifu imezidi kuimarika.
Mechi tuliyofungwa na yanga goli la Morison uzembe ulianzia kwake lakini kabla alitokwa kuonywa na manula pale alipocheza rafu isiyo na sababu mpaka akapata kadi ya njano pia amekuwa akitoa maboko mengi sana bahati nzuri adhabu yake imekuja tukiwa na mwalimu mpya ambaye ameridhika na wachezaji alionao hivyo itabidi afanye kazi ya ziada ili mwalimu amwamini aweze kupata namba.
 
Tukatae tukubali Mkude ana bahati sana na ana nyota ya kupendwa na mashabiki na wanachama wa Simba. Sasa kupendwa huko kumemfanya masikio yakazidi kichwa na shida ndipo ilipoanzia hapo. Mkude hata atoe maboko matano mfululizo bado atapigiwa kelele kidogo na ataendelea kuimbwa midomoni mwa mashabiki wa Simba. Lakini maajabu ya mwaka kuna mtu anaitwa Muzamiru Yasin "shujaa asiyeimbwa" Yaani huyu jamaa atakaba, atashambulia, utamuona golini kwake anaokoa ghafla yupo mbele kule anashambulia, atakimbia uwanja mzima dakika zote 90+ za mchezo lakini sasa atoe boko moja tu utasikia toa huyo, usimpange tena huyo na hilo boko litazungumziwa mwaka mzima mpaka ligi iishe.

Yote kwa yote Mkude hana wa kumlaumu amejipa kazi nzito sana yeye mwenyewe na wa kuifanya hiyo kazi ni yeye mwenyewe kwani kukosekana kwake kutokana na utovu wa nidhamu amerudi amemkuta mbabe Lwanga ameweka viwango vipya vya kiungo mkabaji anatakiwa acheze vipi. Itampasa sasa MKUDE walau avikaribie hivyo viwango vipya ili aweze kucheza mara kwa mara kama zamani.
 
Mkude avunjiwe Mkataba Aondoke ndani ya Simba maaana tayari mashabiki hatumtaki, Uwepo wake ndani ya Simba utahatarisha upigwaji wa Misumari kwa LWANGA na GIKANJI kama alivyomfanyia FRAGA. The Guy is empty Set na jitu la ovyo ovyo, na nikiri kwamba kama ni Limbwata kwa mashabiki, basi mkude alituweza wengi lkn ujio wa Lwanga namuona Mkude kama mchezaji mwenye Kiwango cha Majimaji FC
 
Tukatae tukubali Mkude ana bahati sana na ana nyota ya kupendwa na mashabiki na wanachama wa Simba. Sasa kupendwa huko kumemfanya masikio yakazidi kichwa na shida ndipo ilipoanzia hapo. Mkude hata atoe maboko matano mfululizo bado atapigiwa kelele kidogo na ataendelea kuimbwa midomoni mwa mashabiki wa Simba. Lakini maajabu ya mwaka kuna mtu anaitwa Muzamiru Yasin "shujaa asiyeimbwa" Yaani huyu jamaa atakaba, atashambulia, utamuona golini kwake anaokoa ghafla yupo mbele kule anashambulia, atakimbia uwanja mzima dakika zote 90+ za mchezo lakini sasa atoe boko moja tu utasikia toa huyo, usimpange tena huyo na hilo boko litazungumziwa mwaka mzima mpaka ligi iishe.

Yote kwa yote Mkude hana wa kumlaumu amejipa kazi nzito sana yeye mwenyewe na wa kuifanya hiyo kazi ni yeye mwenyewe kwani kukosekana kwake kutokana na utovu wa nidhamu amerudi amemkuta mbabe Lwanga ameweka viwango vipya vya kiungo mkabaji anatakiwa acheze vipi. Itampasa sasa MKUDE walau avikaribie hivyo viwango vipya ili aweze kucheza mara kwa mara kama zamani.
Ila kitendo cha huyu kocha kukubali mzamiru na dilunga,inaonyesha kabisa kuna jambo halikuwa sawa hapo awali, unawaweka bench wachezaji wazuri halafu ukifungwa unalalamika, ila sass wakaze buti, ila inavyoonekana huyu kocha anasikiliza ushauri wa matola yaani mwenyeji wake vizuri, na ndio maana yuko makini na anavimbua vile vitu ambavyo kocha hawakuviona.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom