Simba kwa kheri Afrika,blablabla zimezidi ktk soka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Simba kwa kheri Afrika,blablabla zimezidi ktk soka

Discussion in 'Sports' started by engmtolera, Apr 4, 2011.

 1. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #1
  Apr 4, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Sosthenes Nyoni
  NDOTO ya mabingwa wa Tanzania, Simba kusombe kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika imebaki hadithi baada kupokea kipigo cha mabao 3-2 kutoka kwa TP Mazembe jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

  Mabingwa hao mara mbili wa Afrika, waliuanza mchezo huo kwa kasi na kufanikiwa kupata bao la kuongoza dakika ya 18, kupitia mshambuliaji wake Given Singuluma aliyeunganisha vizuri mpira wa kona uliopigwa na Patou Kabangu.

  Shija Mkina aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Juma Jabu aliyeumia alipatia Simba bao la kusawazisha dakika 58, kufutia mpira wake wa krosi kwenda moja kwa moja wavuni na kumwacha Kidiaba Robert asijue la kufanya.

  Mshambuliaji Allan Kaluyituka alipatia Mazembe bao la pili dakika 63, baada ya kuwazidi ujanja mabeki wa Simba, kabla ya Mbwana Samatta kuisawazishia tena Simba dakika ya 65, akiunganisha kwa kichwa mpira wa kona wa Amri Maftah kufanya matokeo hayo kuwa 2-2.

  Nyota wa Zambia, Singuluma alimaliza ubishi kwa kupachika bao la tatu dakika 73, baada ya kupokea pasi nzuri ya Kaluyituka na kupiga shuti lilomshinda Juma Kaseja na kujaa wavuni.

  Simba watajilaumu wenye kwa kupoteza nafasi nyingi za kufunga katika kipindi cha kwanza baada ya washambuliaji wake Samatta, Emmanuel Okwi na Mussa Mgosi kupoteza nafasi nyingi za wazi.

  Dakika ya 3, Mgosi alishindwa kumalizia kona ya Okwi baada ya mpira wake wa kichwa kupaa juu, lakini mashabiki wa Simba wataikumbuka nafasi nzuri aliyokosa Samatta baada ya kumtoka beki wa Mazembe, Stopila Sunzu na kubaki yeye na kipa, lakini shuti lake lilidakwa na Robert Kidiaba.

  Katika mchezo huo Simba walitawala sana sehemu ya kiungo na kufanya mashambulizi mengi, huku wapinzani wao wakicheza kwa kujihami na kufanya mashambulizi ya kushitukiza na kupiga mashuti ya mbali.

  Awali mashabiki wanaodaiwa kuwa wa TP Mazembe walipambana na Polisi wakati wakijaribu kuingia kwenye jukwaa ambalo hakustahili kukaa.
  [​IMG]
   
 2. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #2
  Apr 4, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,974
  Likes Received: 726
  Trophy Points: 280
  Hii ilitarajiwa sana,tusidanganyane.Pole Ivuga,ngojeni la ndondo.
   
 3. CPU

  CPU JF Gold Member

  #3
  Apr 4, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Naweza kusema hizi kauli za ""Oooh wale wazembe tu, hela hazichezi, tunalingana kiwango nao, muziki wetu hawauwezi, mvua ikinyesha ndo wamekwisha, ooh walihonga refa ili washinde kule kwao, oooh mbona Zamalek tulimtoa, Sisi sio kama Yanga. . ." ndizo hasaaaa zinaitwa SOKA MIDOMO MIREEEEEFU.
  Nashangaa wanaweka nguvu kubwa ktk mechi moja tu, tena ya raundi ya kwanza kwa ahadi za mamilioni
  Wakati hao hao Simba wameshindwa kuwafunga hao Yanga ktk ligi msimu mzima, na juzi wamnusurika kichapo.
   
 4. NG'OTIMBEBEDZU

  NG'OTIMBEBEDZU JF-Expert Member

  #4
  Apr 5, 2011
  Joined: Aug 11, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Na hii nayo pia ni bla bla tupu(I mean hii post), wabongo ndivyo tulivyo bwana, si Yanga, Simba n.k, too much talking. Kuna mpaka NGO zinaitwa Twaweza, Tunajali n.k, wakati haziwezi na hazijali pia. Unamleta kocha unataka ajenge timu, from the base, huku tunamtaka atupeleke AFCON ndani ya miezi sita, na mashabiki wote wanakubaliana na hilo, so kuongea ni jadi yetu kwani hata uhuru tulipiga domo vilevile.
   
 5. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #5
  Apr 5, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  ulitaka tuweke nguvu kwenye mechi ya Simba na Yanga!? kama tumeshundwa kumfunga Yanga nyie mmesahau kama mlikaa miaka 8 bila kutufunga kwenye ligi......
   
 6. mi_mdau

  mi_mdau JF-Expert Member

  #6
  Apr 5, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 563
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  hii post nayo ni blah blah za washabiki wasioipenda Simba, hasa wa Yanga. Timu gani ya Tz ina mafanikio kwenye michuano ya kimataifa kama Simba? lakini walitaka Simba ikubali kichapo kabla haijacheza?? hata ulaya kwenye maendeleo ya soka, timu ikipangiwa barcelona watu wanaanza kuihesabia maumivu lakini haiwezi kukubali kufungwa kabla. Hongera simba kwa kiwango kizuri ambacho hata hao Mazembe wamevutiwa na simba ndo maana wakawapenda samata, okwi na ochan na hawakushinda kirahisi hapa dar. Ushindani ndo kitu tulichotaka kukiona. Sidhani kama ni mara ya kwanza kusikia timu ikijitamba kushinda na ikafungwa, na si ajabu, na si afrika peke yake. Hao Yanga walioikosakosa Simba mbona hawahacheza klabu bingwa. Simba ndo Bingwa wao watulize midomo vilevile. Waangalie mpira wao la sivyo wataishia kushangilia mazembe na timu nyingine za nje zikija kucheza na simba wao wakiwa wamepaki timu jangwani kusubiria ligi kuu
   
 7. mpingo

  mpingo Member

  #7
  Apr 5, 2011
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 64
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 15
  hahahahaaaaa.....kazi kweli kweli.
   
 8. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #8
  Apr 5, 2011
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  hahahaha si nasikia wamekata rufaa... wapate ushindi wa mezani
   
Loading...