Simba kujenga uwanja wake bunju

matambo

JF-Expert Member
May 14, 2009
727
0
Ile hadithi ya klabu ya Simba kujenga uwanja wake imeaanza tena leo.

mwenyekiti wa klabu yetu hiyo mheshimiwa mbunge wa kuteuliwa Ismail Aden Rage amesema kamati ya utendaji ya klabu hiyo imeanza mchakato wa ujenzi wa kiwanja hicho kitakachokuwa huko Bunju, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam. amedai wameingia kwenye mazungumzo na kampuni ya kituruki itakayojenga uwanja huo utakaokuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji 30,000 waliokaa pia uwanja huo utazungukwa na maduka kadhaa ya biashara. uwanja huo unakadiriwa kuwa utakamilika baada ya miaka miwili

naamin i hizi zitakuwa ni habari njema kwa maendeleo ya soka la bongo iwapo jambo hili litakuwa kweli. shida moja mpaka michezo nayo ina ubabaishaji mwingi kama siasa zetu. hili jambo la simba kujenga uwanja wake huko bunju limeanza kujadiliwa takribani miaka mitano sasa lakini utekelezaji ulikuwa sifuri, ila kama kweli wameamka basi napenda niwapongeze mno na wajitahidi isiwe longolongo kama zamani na pia tumpige bao mtani anayeringia shamba lake la mabua na mbigiri pale jangwani lakini aliita uwanja.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom