Simba kuchukua ubingwa mbele ya Yanga Julai 3?!

Usher-smith MD

JF-Expert Member
Jul 7, 2015
9,493
12,153
Baada ya ushindi wa leo wa goli 1 bila mbele ya Polisi TZ, na kufikisha pointi 70 , ni wazi kuwa Simba Sc wanahitaji point 6 tu yaani ushindi wa mechi 2 ili wawe mabingwa wa msimu huu VPL 2020/2021.
Kwani Young Africans Sc wana point 64 na mechi 4 mkononi maana yake kama wakishinda hizo watafikisha point 76 , ila moja ya mechi zao ni dhidi ya watani wao Simba Sc
Hivyo basi nadhani unaelewa kwanini mwashabiki wa Yanga sasa hawataki kata kata kucheza na Simba Sc hiyo Julai 3 maana walishapiga Hesabu na kuona balaa hilo

Screenshot_20210619-190500.jpg
Screenshot_20210619-190529.jpg
 
Tarehe 3 Simba atachezea kipigo atake asitake.safari hii sidhani Kama yule aliye waokoa tarehe 8 kwa kulazimisha mchezo uchezwe saa moja Kama atathubutu Tena.
 
Yanga hata ukiwashikia bastola hawawezi kuleta timu uwanjani hiyo july 3!! Wanakuambia ni bora lawama kuliko fedheha!! Ya nini kujipeleka kwenye kipigo??
 
Yanga hata ukiwashikia bastola hawawezi kuleta timu uwanjani hiyo july 3!! Wanakuambia ni bora lawama kuliko fedheha!! Ya nini kujipeleka kwenye kipigo??
Sasa upeleke timu uwanjani uchapwe goli 5 au usipeleke timu mwenzio apewe goli 3 kipi bora?
 
Tarehe 3 Simba atachezea kipigo atake asitake.safari hii sidhani Kama yule aliye waokoa tarehe 8 kwa kulazimisha mchezo uchezwe saa moja Kama atathubutu Tena.
Lakini bingwa sio?
 
Yule mzee wa nyuklia mzee Mpili kasema hivi"mtu atakaejaribu kupeleka timu uwanjani ntamvisha sanda"
 
Bodi ya Ligi wana lao jambo
Yanga tushastukia mchezo.
Hatuingizi Timu tarehe 3 hadi Simba iwe imecheza Viporo vyake. Kumbe TFF wanataka mechi ichezwe kabla ya Simba kuwa Bingwa ili isikose mapato mengi.

Simba inaachaje kupangiwa mechi wiki nzima wakati ina viporo?.
 
kufumba na kufumbua Mwadui kamganda Uto,baasi July 3 wanatupigia saluti vidume

Ilitakiwa tucheze na Yanga tukiwa tumeshachukua ubingwa ila hawa Dole la Kati Fc watupigie gwaride.

Yanaweza kujifungisha au kudroo kwa mwadui ili tar 3 tuingie kwenye mechi ya kukamilisha ratiba ya ligi isiyo na ushindani wala faida yoyote. Kila mganga anawaambia ninachoweza kufanya ni kupunguza idadi ya magoli tu
 
Wao wafanye watakavyo ila itapendeza tuende kwenye mechi yetu na wao tumeshatwaa ubingwa ili watupigie gwaride.
 
Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom