Simba inaniacha hoi sana

Baba yenu

JF-Expert Member
Jun 17, 2016
1,053
1,417
Iv simba viongozi ilionao ndo mambumbumbu au? Walimuacha Tambwe akiwa ametoka kuwa mfungaji bora sasa hivi wanajutia

Sasa wanamuacha Kiza kwa kejeli kibaa o kuwa walimuokota vijiweni!!! Jaman iv Kiza huyu huyu aliyefunga magoli mengi vile na kuwa wa pili nyuma ya Tambwe???

yaani unaacha mke uliyenaye akiwa anajua kupika vzr kwa sababu umepata mke mwingine ambaye hata hujamjaribu kama anajua kupika!!

Iv hao iliowasajiri ina uhakika watafikisha japo magoli 15 kwa msimu huu?

Basi japo hata unampa mtu thaman yake kakusaidia ndo umuache kwaaneno ya shombo?


Nilikuwaga shabiki wa Simba zaman ila 2008 nikaona mpira wa Tanzania ni umiza kichwa nikahamia kushabikia nje ila hizi drama zinanishangaza sana
 
Uliacha kushabikia ila bado inakuumiza kimoyomoyo pole sn mkuu hamia kwa wakimataifa no stress pale kwa mpira wetu wa mchangani
 
simba wamebaki kusema yanga hatutaweza kuludisha zile goli 5,,wamebaki na stori za kale wakati dunia inakuwa update kila mda
 
Hamna klabu ya kipumbavu kama simba, viongozi mpk mashabiki walio wengi wamepumbaa sana, viongozi wao akiili zao zipo kwny sajili za wachezaji na makocha wabovu huku wakipandisha thamani zao ili kujipatia ulaji na kukuza matumbo huku dhumuni la timu likiwa halipo mbele yao kabisa, kwa ufupi ni kijiwe cha wababaishaji.
 
Duuuh Simba ni klabu ya wahuni

Simba sio klabuya wahuni plz. Tatizo ni kuwa wamechagua viongozi wapiga dili. Wao wanachofanya ni kuwadanganya wanachama wa SSC kuwa wameleta wachezaji bomba kuliko waliopo na kuwafanya wajione washindi ila ikifika ligi imeanza timu ikifungwa sababu za kiajabu ajabu zitatolewa. Nina hakina miaka 4 ya kina Aveva na Dewji SSC daima itakuwa chini ya Yanga ns Azam
 
Kiiza kaachwa kwa sababu za nje ya uwanja ambazo viongozi wa simba ndio wanazijua na hawajataka kuziweka hadharani kwa sababu wanazozijua wao. kama ningekuwa kiongozi wa simba nisingemwacha kiiza mwaka huu ila ningemletea straika mmoja matata wapambane kwani mke akikuzingua na bado ana faida kwako haumwachi unamwolea mwenzake ili ajirekebishe na huku unatazama ufanisi wa mwenzake mwisho wa siku utapata nafasi nzuri ya kuamua ubaki na yupi kati yao au ubaki nao wote. mpira ni mchezo wa ajabu sana timu inaweza kusajili mchezaji bora kabisa lakini akashindwa kuonyesha uwezo kutokana na mfumo wa timu husika lakini mchezaji huyo huyo akaenda kusajiliwa na timu nyigine na akafanya vizuri. kwa hiyo hata hao mastraika waliosajiliwa na simba badala ya kiiza wanaweza kuwa bora kabisa huko walikotoka lakini wakashindwa kufanya vizuri simba. heri ndege mmoja uliyemshika kuliko wawili walioko porini unaokwenda kuwawinda!
 
Chongeni tu,maana ndiyo kazi yenu.Kiiza hajaanza kuachwa na simba.Hata nyinyi yanga mulimwacha.Hivyo suala la nani acheze simba ni la wanasimba na si Yanga.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom