Simba ilivyotolewa wana cha kujifunza toka Chelsea?

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,885
6,885
s.JPG


Chelsea baada ya kutambua kuwa uwezo wa kuchukua ubingwa nchini Uingereza imeshindikana, wakaamua kupoteza hata nafasi za kuingia nne bora ingawa wangekazana wengeweza. Walichoamua ni kuelekeza nguvu zao zote kwenye ubingwa wa Ulaya, na kweli wamefanikiwa. Kwani wapinzani wao walikuwa na mawili ya kugombea ubingwa nchini mwao na kugombea ubingwa wa ulaya wakati huo huo. Chelsea wamefanikiwa kuchukua ubingwa huo kwa sababu nguvu zote walielekeza huko, ndio maana siku za karibuni wameweza kufungwa au kutoka sare na timu dhaifu za ligi ambazo hazikuwa na nguvu ya kuifunga Chelsea.

Simba licha ya kuvimba vichwa kuchukua ubingwa mapema, lakini walivyokomalia Yanga kwa nguvu zote nilishangaa wakati huo huo wameshajihakikishia ubingwa. Mchezo wa mwisho haukuwa na umuhimu kwa simba ila kutimiza ratiba tu. Wangeweza kuchezesha zaidi kikosi cha pili ili kuwapumzisha kikosi cha kwanza kwa ajili ya mchezo mgumu wa Sudan. Tatizo la wazi ni kwamba soka letu si la kisayansi, ila ni la mfumo wa mitaani kutambiana.
 
we have nothing to learn from Chelsea. Unataka kuchanganya mafuta na maji.

Hatupambanui sifa na mafanikio. Kuifunga yanga ndio sifa kubwa kwa simba kuliko kuchukua kombe la challenge au kombe la Afrika. Kwa mwendo huu tutafika?
 
Imefika wakati usimba na yanga upunguzwe.Nashangaaga kusikia kiongozi wa simba au yanga anapoomba kura kwa kuahidi kumfunga mpinzani. Juzi wazee wa yanga waliomba timu kwa ajili ya mchezo na simba tu! Inachekesha !
 
Imefika wakati usimba na yanga upunguzwe.Nashangaaga kusikia kiongozi wa simba au yanga anapoomba kura kwa kuahidi kumfunga mpinzani. Juzi wazee wa yanga waliomba timu kwa ajili ya mchezo na simba tu! Inachekesha !

Ndio mpira wa bongo ulivyo, badala ya kuzamilia kombe la Afrika ambalo wangeshinda wangeibuka na donge nono la kuendeshea timu, wao wanakaza buti mpira wa kutambiana mitaani ambao haukuwa na umuhimu kwao.
 
nasikia hata mourinho hawampendi Real Madrid kwa kufungwafungwa na Barcelona.
 
Hatupambanui sifa na mafanikio. Kuifunga yanga ndio sifa kubwa kwa simba kuliko kuchukua kombe la challenge au kombe la Afrika. Kwa mwendo huu tutafika?
wenye uwezo wa kupambanua mambo ni wale wenye akili na uelewa ila sisi inawezekana tunashindwa kufanya hivyo kutokana na kukosa hizo sifa mkuu!

Juzi nilimuona kwenye ITV Mzee Akilimali na Bakali Malima 'akifukuza' uongozi wa Yanga, kusema kweli kama nilisikitika sana kama Mtanzania kuona baadhi yetu wanakosa hata uelewa wa kuanzia (basics)!

Sidhani kama kuna Mtanzania (hasa hawa simba/yanga) atajifunza lolote. Tutabakia tu kuongelea 800m za kusajili wachezaji na kuendeleza klabu wakati tukiishi kwenye vyumba vya kupanga.

 

Similar Discussions

Back
Top Bottom